Malalamiko ya Dulla Mbabe na Ibra Class kwa kupoteza pambano dhidi ya Katompa ni sawa na mfa maji

Hivi hata kina Matumla nao walikuwa wanaongea utumbo hadharani? Mimi nilidhani ni Mwakinyo tu ndio hupuyanga kwenye media, kumbe wapo na wengine!
 
Mimi hili pambano nimeanza kuliangalia round ya 6 kiukweli mpaka niluanza kuona aibu namna Dulla anavyolicheza pambano. Hizi fani zinavamiwa na watu wa ajabu ndio matokeo yake haya. Kuna mazingira hata ukibebwa haina shida ila kwa uchezaji ule ni aibu kubwa kwa tasnia ya ngumi. Inawezekana kwa sababu wanabebwa ndio maana hawajitumi, hawafanyi mazoezi na kadhalika.
 
Katompa ata warudiane na Dula mara 10 Bado Dula atapigwa tu. Nime mshangaa Ibra classic kujiingiza kwenye upuuzi wa Dula.
Bondia pekee anayeweza kumtandika Katompa bila shaka youote ni Selemani Kidunda kwakua jamaa ni Boxer mwenye akili na nguvu.
Ibra nae sijui kawaje! mtu kachezea hivyo halafu anataka mbeleko.
 
Namshukuru sana Mungu kwa kuniumba Mtanzania,na naipenda Tanzania na watu wake.Dullah mbabe ulipigwa kama unapiga.Huo ndio ukweli na msijidhalilishe Tena kwenye kadamnasi,nenda kajikande maumivu.
 
Dulah mbabe wala sio bondia wa kumtafutia mapambano nje ya nchi anapigana sababu ya njaa tu lkn ameshuka sn kimedani ndio maana mara kwa mara anaomba pambano na anaishia kubondwa tu.

Dula ajikite kupiga ngoma za mchiriku au kama kuna mashamba kwao ajikite kwenye kilimo lkn ngumi zimeshamshinda....

Na akiendekeza njaa atakuja kufia uliongoni

Asijekusema hajaambiawa, shauri yake.
 
Anamkumbatia katompa kama vile anaitaka cha2!
 
Bora anayejifariji kwa kauli mbiu ya"Kupigwa kama umepiga na kupiga kama umepigwa.
 
Dulla pombe na bangi nyingi akiwa maskani kwao na masela wenzake ndo maana hata pumzi hana yaani round ya 4 tuuh upepo umekata
 
Bondia gani hana nidhamu na professional yake!! pombe yeye sigara yeye anategemea nini zaidi kichapo.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…