A
Anonymous
Guest
Nilikata tiketi online tarehe 08 Mei 2026 kwa ajili ya safari ya tarehe 09 Mei 2026 kutoka Dar es Salaam kwenda Kahama. Kituo nilichopangiwa kupandia ni Mlandizi.
Nilifika kituoni mapema saa 14:15 nikisubiri basi, lakini basi lilichelewa kufika na lilifika baada ya saa 1:30. Cha kusikitisha, baada ya kufika eneo la kituo, basi halikusimama kabisa. Lilikuwa linatembea taratibu sana, takribani 5 km/h, likionekana kukwepa faini kwa kuwa tayari lilikuwa limevuka mataa ya Mlandizi kuelekea Morogoro.
Kutokana na hali hiyo, niliachwa wakati nikikimbilia barabarani maana nilikuwa pembezoni mwa barabara kwa ajili ya usalama maana kulikuwa na gari nyingi sana zikipita barabarani, licha ya kuwahi kituoni kwa muda sahihi. Nilijaribu hata kulifuata kwa pikipiki lakini sikuweza kulifikia.
Naomba kampuni husika inipe mrejesho pamoja na kurejeshewa nauli yangu kwa kuwa kosa halikuwa upande wangu.
Asanteni.