Malalamiko ya kuendelea mgao wa Umeme! Kumbe shida sio January Makamba?

"niueni" [emoji23] [emoji23]
 
Leo Wauza mafuta Wenye madepo wanatafuta wanunuzi kwa simu, discount mpka shil 200 kwa Lita nje ya Bei elekezi ya EWURA. Angalau tunaona mwanga mbele.
 
Maendeleo ya taifa lolote duniani hufanywa na raia/wananchi wenyewe.

Jasho la wananchi ndilo hutumika kuendesha maisha ya wananchi wenyewe, kuendesha serikali ( kuwahudumia viongozi na watumishi wengine, pia shughuli za maendeleo).

Serikali za nchi masikini hazijui hili, hushirikiana na wageni kula jasho la wananchi wao na hivyo kukosekana maendeleo.

Serikali za nchi zilizoendelea husaidia wananchi wao kwenda katika nchi ambazo hazijaendelea, kuwaghilibu viongozi ili waingie mikataba ya kuwaendeleza na kuzifanya nchi masikini kuwa masikini zaidi.
 
Aliacha tatizo kubwa siyo la kumaliza Leo wala Kesho jiulize nini alifanya wizarani
 
Tuambie pia makamba mkataba aliyosain na ile kampuni kule South Africa akiwa waziri wa umeme Chief.
 
Tanzania shida ya iumeme haitakwisha mpaka shirika likatwe vipande vipande, kila mkoa uwe na shirika lake la umeme.

Hata bwawa na nyerere na mawawa yote ya kufua umeme yaanze kazi leo na tuwe na umeme wa ziada, shida ya umeme haitokwisha.

Kuendesha mashirika ya umeme ni zaidi ya tunavyofikiria. Haiwzekani kabisa kuliendesha shirika la umeme kama idara ya serikali. tutadondokea pua tu, hata aje nani.
 
Hii nakumbuka utadhani jamaa walikuwa na ukame wa kulamba asali , jpm alipofariki tu wakaileta hii kampuni ya kihoni wakalamba mabillion, yaan hats mfumo ule wa NMb hauna gharma hiyo
 
Huyu bib kila siku kiguu na njia eti anatafuta wawekezaji
 
Mwezi wa kwanza ni jambazi usilitetee kabisa hata beanz ni wanafiki sana. Uzuri Mama anawalia time tu hawa wezi. Waliharibu mfumo wote wa umeme huku wanamdanganya Mama, uzuri Mama alinilishwa kwa njia zote za JF, na ushauri kabisa achana na group la Makamba maana wao wanatfuta urais wanamharibia Mama ni kama ilivyo Mwigulu yaani anafanya character assassination ya Mama kuonekana wizi uchumi mbaya yaani natamani aniteue mi niwe waziri wa fedha aone nitakavyosimamia, yaani nitabana mpaka shs hamsini iwe hela
 
Tatizo alitengeneza makamba, litachukua muda kuisha
 
Toka kaondoka January na Maharage. Sasa hivi hata emergency ya Tanesco simu yao imekuwa na shida sana kupatikana na ukibahatika kuipata hakuna anayeijibu.
Makamba na Maharage walikua ni failure pale Tanesco hilo liko wazi. Miaka 2 yote wameitumia kwenye publicity tu lakini hakuna cha maana walichokifanya.

Ukiacha tuhuma za wizi, hao jamaa kwa miaka 2 hawajakamilisha ama kufanikisha chochote cha maana, hakuna mpango ama mradi wowote waliouanzisha na kuumaliza.

Walikua wamejificha kwenye publicity na media coverage tu. Porojo nyingi utendaji sifuri.

Wakasingizia mitambo haikufanyiwa matengenezo kwa miaka 5, hata mtu asie na akili anajiuliza, mtambo una running hours, bila matengenezo utaharibika tu, huwezi kuulazimisha ufanye kazi lakini kwa maelezo yao ni kwamba mitambo ililazzimishwa kufanya kazi kwa miaka 5 bila matengenezo na bila kuharibika, hii haiingii akilini hata kidogo.

Wao wakasema wanafanya matengenezo, miaka 2 mgao kila siku. Juzi Biteko anasema miaka 2 mitambo Mtwara haina matengenezo hata kidogo, sasa wao walikua wanafanya matengenezo yapi?
 
Mama mwenyewe ana udhaifu ktk usimamizi. Anawalia timing hao mafisadi mpaka lini wakati wanazidi kumharibia?
Piga chini hao wote, weka watu wengine ili kazi unatotaka ifanyike iendelee. Ataendelea kulea wazembe na wezi mpaka lini?
 
Hakuna ataekwemdq kuishughulikiw tanesco asionekane "failure" kwa mfumo mbovu wa utawala uliopo.

Ushauri wangu likatwe katwe na kila mkoa wa Tanzania uwe na mashirika yake ya umeme.
 
Wewe bado hujajua tatizo la umeme Tanzania.

Tatuzo la umeme Tanzania halihusiani na shirika kuwa moja ama kugawanywa ama nini.

Tatizo la umeme Tanzania ni investment, hatujafanya uwekezaji wa maana kwenye umeme kwa zaidi ya miaka 30, vyanzo vya umeme tulivyonavyo ni vya enzi za Nyerere.

Tungekua tumewekeza kwenye umeme, tunazalisha umeme wa kutosha kusingekua na tatizo lolote.

Sasa hata ugawe shirika ama uwe na shirika kila kijiji ama kitongoji inasadia nini kama hakuna umeme wa kutosha?

Kwa hiyo suluhisho ni kua na umeme wa kutosha na sio kua na mashirika mengi ya umeme huku hakuna umeme.

Angalia Zesco Zambia ama Eskom ya South, bado ni shirika moja moja, zesco wana umeme mara 2 na ushee ya Tanzania, wana megawati 3800+ huku Tanzania tukiwa na megawati 1600.

Zesco wasingekua wamesaini PPA na South Africa wangekua na umeme mwingi sana. Na wao kutokana na tamaa ya hela, wakasaini mikataba ya PPA na South Africa hivyo umeme mwingi wanauza South wanaishia kua na mgao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…