Malalamiko ya kuendelea mgao wa Umeme! Kumbe shida sio January Makamba?

Makamba na Maharage walikuwa waswahili tu wapiga dili. Wenye maneno mengi yasiyokuwa na tija.

Huyu kijana hana porojo za uswahili swahili. Atatuvusha, msikilize vizuri kwenye hii video clip fupi utaelewa alivyo tofauti na hao wapiga dili waliotufikisha hapa kuwa nchi ya mgawo wa umeme.


View: https://youtu.be/38_STolJjzE?si=bt-Ir0Pvi3pv8GWm
 
Tatizo unaloliona sasa limeletwa na kipara na bendi yake ya kutupiga.
 
Kwanini usifiche upumbavu wako kwakutoandika mashudu mtandaoni?
Sasa wewe unaye jisifia kuwa ni kijambio cha sa100 wewe ni mzima kichwani kweli [emoji16][emoji16] wewe endelea tu kugawa kwa mparange hapo sisiemu maana yake tunajua kazi zenu chamani
 
Msikilize Dotto Mashine za umeme miaka miwili hazifanyiwa matengenezo miaka miwili iliyopita Waziri wa Nishati alikuwa nani?
 
Nov 16, 2023
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dkt. Doto Biteko ameitaka TANESCO kutojificha kwenye kichaka cha taratibu za manunuzi ambacho kimepelekea mtambo mmoja wa umeme mkoani Mtwara kutofanya kazi kwa miaka miwili na kuongeza kuwa Serikali inaiangalia menejimenti ya TANESCO lakini kwa sasa ijitathmini na ijikite kwenye kupelekea watu umeme na wawe kimbilio la wananchi.Aidha, Dkt Biteko ameitaka TANESCO Makao Makuu kutojilundikia majukumu ikiwemo ya manunuzi ambayo yanarudisha nyuma shughuli za shirika na kuleta urasimu.
 
Umekurupuka tatizo la umeme aliloliacha January haliwezi kutatulika kwa mwezi mmoja. Labda kama aliyeingia ataleta umeme wa radi
Mfafanulie vizuri huyo kiazi sidhani kama amekuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…