Malalamiko ya Makato ya Deni la Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Mwezi Juni, 2021

Malalamiko ya Makato ya Deni la Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Mwezi Juni, 2021

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
7,743
Reaction score
13,657
Hello Wadau!!

Tumekuwa na tatizo la upatikanaji wa Kilipia Mshahara (Salary Slip) kwa miezi kama miwili mfululizo

Hatimae mwezi June Salary Slip zinapatikana kwa mtandao

Nilichokiona ni kuongezeka kwa deni la Bodi ya Mikopo (HESLB) kwa zaidi ya 100%

Hiki kinanifanya nijiulize

Mosi, ni kwangu tu au na kwa wanufaika wengine?

Mbili, hivi bodi si walisema 6% ya rentation fee wameiondoa, sasa mbona deni limeongezeja kutoka milioni tatu mpaka milioni 6?

Tatu, hivi hizi sio pesa za dhuruma bodi inazikusanya kutoka kwa walipa kodi tena watumishi wa Umma?

Mwisho, wadau hivi ndio hasa vitu vinavyotufanya tuzichukie hata kazi tunazofanya za umma. Licha ya kuwa na mshahara mdogo taasisi inakuongezea deni mara mbili zaidi. Hivi sisi tumewakosea nini nyie Bodi???

Naombeni ushauri jamani lakini sio vibaya wanufaika wenzangu mnaokatwa na Bodi hebu angalieni kwenu

Nawasilisha

====
Habari wadau,

Kwa yeyote anayekwata na Bodi ya mkopo. Linganisha deni lako la mwezi may na deni lako la mwezi june kwenye salary slip yako utagundua.

Wamekata pesa ya mwezi June lakini deni limebaki lile lile la mwezi may. Pia kuna wengine wamekatwa pesa mwezi Juni mfano mtu amekatwa laki na elfu nane lakini ukicheki kwenye deni husika imepungua elfu kumi Tu pesa nyingine wamechukua kimya kimya.

Nadhani hii ni lengo maalum la Bodi ya mkopo kuhakikisha watumishi wasimalize deni lao mpaka wanaastaafu ili mugawane pension

Wanafanya wizi kwenye salary slip Kwa vile wanajua watumishi wengi hawasomi deni husika kwenye salary slip.
Mheshimiwa mtukufu, Mama yangu mpendwa, Rais wangu nakuja kwako nikiwa natambaa kwa magoti, nakupa taarifa tu, Bodi ya MIKOPO inatuangamiza wanao, kwa makato ya uonevu kabisaaa, yani wananikata hela yao ya Kila mwezi lakini deni halipungui.

Nimekosa usingizi na nimepoteza hata ujasiri na nguvu ya kuendelea na kazi hii kwa uonevu ambao bodi ya mkopo ya elimu ya juu inayonifanyia na mpaka inafikia wakati nakufulu, kwanini mungu hawashushii dhoruba Hawa wakaondoka moja kwa moja kama gharika ya nuu.

Mama naomba tutetee wanao,.mana wewe ndie kiongozi wetu wa juu ambae sauti yako inasikika kuliko za binadam wengine.

BODI YA MIKOPO INATUANGAMIZA [emoji120][emoji120][emoji120]
TAHADHARI KWENU NDUGU ZANGUNI MNAOKATWA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWENYE MISHAHARA YENU
KUNA SUALA INAWEZEKANA HAMJALIGUNDUA KAMA HAMJACHUNGUZA KWENYE SALARY SLIPS ZENU ZA MWEZI MAY NA MWEZI JUNI 2021

Kuna wale ambao deni la Mwezi Juni kwenye salary slip limekuja kama lilivyo kwenye Salary slip ya Mwezi Mei 20121 yaani deni halijapungua ukilinganisha na mshahara uliopita, na kuna wengine ambao deni lao limeji-double yaani kama Mwezi Mei ilionekana unadaiwa Mil 2 basi Mwezi Juni waweza kuta unadaiwa Mil 4, pia kuna wengine ambao Salary slip zao zinaonesha labda Mwezi Mei amekatwa Laki na 41 elfu lakini ukichukua deni la Mwezi Mei ukatoa Deni la Mwezi Juni utapata makato ni kama elfu 31 kitu ambacho sio kweli Kimahesabu.

Binafsi sijafanya mawasiliano na HESLB Kujua shida ni nini, ila nimeona niwastue ndugu zangu ili kila mtu achunguze salary slip yake ili kama na wewe yamekukuta kama mimi basi uchukue hatua as soon as possible_. Inawezekana hii hali imetokea siku nyingi ila kwa sababu hatudadisi vizuri kwenye hati zetu za mishahara tunajikuta tunalipa kila mwezi mpaka miaka 10 lakini bado deni haliishi

NAWATAKIA UDADISI MWEMA

CC: HESLB Kwa taarifa
CC: BENKI KUU KWA UFUATILIAJI
Nisamehewe kama Sikutafsiri vizuri nilichokiona kwangu na kwa Wenzangu


Copy $ paste
Habar wana JF,

Kupitia ukurasa huu napenda kutoa dukuduku langu na kama kuna wanaohusika bas hatua zichukuliwe

Bodi ya mikopo katika makato yao ya mwezi huu wa sita, makato yao hayaeleweki

Kwenye salary slip makato yao wameonesha kiwango walichokata lakini cha ajabu deni la msingi kiwango kilichokatwa hakiendani na kiwango kilichoandikwa

Kwa mfano:
Deni la bodi mwezi wa tano lilibaki 1050390/=
Kwa hyo baada ya makato ya tsh 141000/= ilitakiwa deni libaki 909,390/=
Lakini cha ajabu wameandika deni limebaki 1019325/=

Kwa hyo inamaana bodi wamekata shiling elf thelathin tu lakin kiuhalisia wamekata laki moja na elfu arobaini na moja

Huu wizi mnaotufanyia bodi sio uungwana kwa kweli.

Mnachofanya ni kuchonganisha serikali yetu yenye nia njema ya kuwakomboa watumishi wake.

Haki itendeke.

HaiwezekanI mshahara unakatwa zaidi ya 35%.

PIA, SOMA:
- Mrejesho: Bodi ya Mikopo(HESLB) yasema haihusiki na changamoto iliyojitokeza kwenye Salary slip mwezi Juni
 
Hilo deni, bodi ni as if hawataki liishe. Hata ukimaliza kulipa na ukapewa barua ya kumaliza kulipa, siku moja ukijifanya kwenda kucheki tena unashangaa unadaiwa mamilioni. [emoji16]
Sasa Mkuu kama ulishamaliza na barua wakakupa unapelekwa Nini tena bodi, lazima wakupige hata laki sita hivi za kuwasumbua[emoji2][emoji2][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Hawa jamaa ni wezi, kuna jamaa yangu alianza kukatwa akiwa TGTS B, lakini Mwezi huu kapanda daraja. Baada ya uzi huu nimempigia akaniambia wamekata pesa ndefu ya TGTS C lakini kwenye salary slip, deni limepungua kwa elfu 16 tu badala ya kupunguza walichokata.

HESLB ni majipu
 
Hawa jamaa ni wezi, kuna jamaa yangu alianza kukatwa akiwa TGTS B, lakini Mwezi huu kapanda daraja. Baada ya uzi huu nimempigia akaniambia wamekata pesa ndefu ya TGTS C lakini kwenye salary slip, deni limepungua kwa elfu 16 tu badala ya kupunguza walichokata.

HESLB ni majipu
Mimi pia nina shida hiyo..

Tupate maelezo tafadhali.

Huu ni ujambazi kabisaa
 
Duhh. Mkuu embu naomba msaada wa number zao..
Mimi nimekatwa 173K

Ila kwenye deni inaonekana wamekata 50...
Hiyo 120 imeenda wapi!??

Kuna uhuni hapaa..
Screenshot_20210630-174410.png
 
Salary slip Kuna shida, baada ya kukuona uzi huu, deni la mwezi Mei na juni tofauti ni Sh.19 tu, licha ya salary slip kuonesha nimekatwa kama kawaida.Inshort mwezi huu nimekatwa sh.19 na takehome imebaki ileile kama ya mwezi Mei.Hivi Hazina imehamia Dodoma au ipo Dar?
Habari hii inabidi isambae kwenye mitandao yote ya kijamii
 
Ni uhuni juu ya uhuni, wizi juu ya wizi, kila mtu na kilio chake. Kuna mtu deni limepungua kwa sh. 19, yaani tofauti ya deni mwezi Mei na June ni sh.19, makato yameoneshwa kama ya mwez Mei. Wengine wamekatwa kiwango kikubwa zaidi ya makato ya awali, wengine deni limekuwa kubwa mara mbili zaidi ya hapo awali.

Huu ni uhuni wa kutisha, tunahitaji maelezo ya kina toka Bodi ya mikopo juu ya wizi huu na jinsi ya kuzipata hela za watu
 
Duhh. Mkuu embu naomba msaada wa number zao.
Mimi nimekatwa 173K

Ila kwenye deni inaonekana wamekata 50.
Hiyo 120 imeenda wapi?

Kuna uhuni hapaa.
Jaribu hii 0736 665 533
Pia watafute kupitia mitandao ya kijamii(FB, Twitter n.k) huko utapata namba zao zaidi hadi za WhatsApp
 
Back
Top Bottom