data
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 26,858
- 23,768
Nchi ngumu sana hii... Inakuaje!?? Yani mshahara unakuwa kama hisani...Hello Wadau!!
Tumekuwa na tatizo la upatikanaji wa Kilipia Mshahara (Salary Slip) kwa miezi kama miwili mfululizo
Hatimae mwezi June Salary Slip zinapatikana kwa mtandao
Nilichokiona ni kuongezeka kwa deni la Bodi ya Mikopo (HESLB) kwa zaidi ya 100%
Hiki kinanifanya nijiulize
Mosi, ni kwangu tu au na kwa wanufaika wengine?
Mbili, hivi bodi si walisema 6% ya rentation fee wameiondoa, sasa mbona deni limeongezeja kutoka milioni tatu mpaka milioni 6?
Tatu, hivi hizi sio pesa za dhuruma bodi inazikusanya kutoka kwa walipa kodi tena watumishi wa Umma?
Mwisho, wadau hivi ndio hasa vitu vinavyotufanya tuzichukie hata kazi tunazofanya za umma. Licha ya kuwa na mshahara mdogo taasisi inakuongezea deni mara mbili zaidi. Hivi sisi tumewakosea nini nyie Bodi???
Naombeni ushauri jamani lakini sio vibaya wanufaika wenzangu mnaokatwa na Bodi hebu angalieni kwenu
Nawasilisha
Mambo yanakera sana hayaa..