Malalamiko ya Makato ya Deni la Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Mwezi Juni, 2021

Malalamiko ya Makato ya Deni la Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Mwezi Juni, 2021

Mheshimiwa mtukufu, Mama yangu mpendwa, Rais wangu nakuja kwako nikiwa natambaa kwa magoti, nakupa taarifa tu, Bodi ya MIKOPO inatuangamiza wanao, kwa makato ya uonevu kabisaaa, yani wananikata hela yao ya Kila mwezi lakini deni halipungui.

Nimekosa usingizi na nimepoteza hata ujasiri na nguvu ya kuendelea na kazi hii kwa uonevu ambao bodi ya mkopo ya elimu ya juu inayonifanyia na mpaka inafikia wakati nakufulu, kwanini mungu hawashushii dhoruba Hawa wakaondoka moja kwa moja kama gharika ya nuu.

Mama naomba tutetee wanao,.mana wewe ndie kiongozi wetu wa juu ambae sauti yako inasikika kuliko za binadam wengine.

BODI YA MIKOPO INATUANGAMIZA [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Leo hii katiba ingekua iko huru mmngefunguz madai na kesi ingekua huru kusikilizwa kuhusu ujinga wa utawala wa awamu ile
 
Salary slip Kuna shida, baada ya kukuona uzi huu, deni la mwezi Mei na juni tofauti ni Sh.19 tu, licha ya salary slip kuonesha nimekatwa kama kawaida.Inshort mwezi huu nimekatwa sh.19 na takehome imebaki ileile kama ya mwezi Mei.Hivi Hazina imehamia Dodoma au ipo Dar?
 
Kwangu deni limepungua tsh19 tu lakini wamekata zaidi ya tsh180k. Huu ni uhuni!
 
Hapa wa kulalamikiwa naona ni hazina kwanza, bodi baadae. Hazina ndio wanaoandaa malipo na kupeleka makato sehemu mbalimbali mfano bank, heslb nk.

Sasa, hazina wamezingua na bodi watapokea hela zetu. Kikubwa ni kutunza salary slip na kuomba refund huko bodi. Nimeona sehemu ya refund kwenye ule mfumo wao wa bodi japo bado haujaanza kufanya kazi.

Kuna kipindi nilisikia serikali sijui inaunganisha mifumo ya malipo. Labda ndiyo imeleta hii shida.

Hazina njooni mjibu hoja za wadau. Mmetibua mfumo mwisho wa mwaka wa fedha. Angalieni salary slip za Juni mmekata deni la bodi lakini halijapungua.

NB. Kwa nini hazina huwa mnazingua kwenye deni la bodi tu na siyo la benki? Je, ni makusudi au ni kweli mlikuwa mnahamia mfumo mpya?
 
Halafu bodi walisema wao ndio wana deni halisi. Tuwasubiri kuanzia kesho mfumo wao wa kuangalia deni ukikaa sawa tutaona tu, na kama mtifuano ndo utaanzia hapo.

NB. Bodi, kumbukeni VRF ililetwa mwaka 2013. Hivyo, chonde chonde muiondoe yote kwa wale wakopaji wa kabla ya 2013 kwa sababu haikuwepo kwenye mkataba. Pia, hata wakopaji wa baada ya 2013 muiondoe yote kwa sababu serikali hutoa elimu kama huduma na si biashara.

Nimesikia mmeanza janja janja yenu kwamba, mnatoa VRF baada ya 1st May 2021 baada ya mama President kutamka.

Kumbukeni kuna watu walisaini mkataba huko nyuma ukiwa hauna VRF, na nakala tunazo, tukienda mahakamani msije kulaumu.
 
Wanufaika bodi ya mikopo elimu ya juu HESLB kwa mwezi June wamejikuta wamekatwa kiasi wanachokatwa na deni halisi limebaki Kama lilivyokuwa linasomeka mwezi may, na kilichopungua ni tsh 150/=tu, na deni kubaki lilivyo.

Huu ni wizi wa wazi kabisa na wahusika wanatakiwa kujitathimini na kujiuzulu wenyewe bila shinikizo kwani ni aibu kubwa kukata katika mshahara 141000 halafu upunguze Deni kwa sh. 150/=. tu.

Inawezekana serikali imeishiwa hela na imekata kwa makusudi ili kupata fedha ya kupandisha madaraja.

Kama ni hivyo ingekopa huko bodi ya mikopo na si kikata fedha bila mkopo kupungua.

Wanasheria na wanaharakati lisemeeni hilo kwa pamoja ili haki za msingi za wanufaika bodi ziweze kuzingatiwa.
 
Back
Top Bottom