Wanufaika bodi ya mikopo elimu ya juu HESLB kwa mwezi June wamejikuta wamekatwa kiasi wanachokatwa na deni halisi limebaki Kama lilivyokuwa linasomeka mwezi may, na kilichopungua ni tsh 150/=tu, na deni kubaki lilivyo.
Huu ni wizi wa wazi kabisa na wahusika wanatakiwa kujitathimini na kujiuzulu wenyewe bila shinikizo kwani ni aibu kubwa kukata katika mshahara 141000 halafu upunguze Deni kwa sh. 150/=. tu.
Inawezekana serikali imeishiwa hela na imekata kwa makusudi ili kupata fedha ya kupandisha madaraja.
Kama ni hivyo ingekopa huko bodi ya mikopo na si kikata fedha bila mkopo kupungua.
Wanasheria na wanaharakati lisemeeni hilo kwa pamoja ili haki za msingi za wanufaika bodi ziweze kuzingatiwa.