Malalamiko ya Makato ya Deni la Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Mwezi Juni, 2021

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
7,743
Reaction score
13,657
Hello Wadau!!

Tumekuwa na tatizo la upatikanaji wa Kilipia Mshahara (Salary Slip) kwa miezi kama miwili mfululizo

Hatimae mwezi June Salary Slip zinapatikana kwa mtandao

Nilichokiona ni kuongezeka kwa deni la Bodi ya Mikopo (HESLB) kwa zaidi ya 100%

Hiki kinanifanya nijiulize

Mosi, ni kwangu tu au na kwa wanufaika wengine?

Mbili, hivi bodi si walisema 6% ya rentation fee wameiondoa, sasa mbona deni limeongezeja kutoka milioni tatu mpaka milioni 6?

Tatu, hivi hizi sio pesa za dhuruma bodi inazikusanya kutoka kwa walipa kodi tena watumishi wa Umma?

Mwisho, wadau hivi ndio hasa vitu vinavyotufanya tuzichukie hata kazi tunazofanya za umma. Licha ya kuwa na mshahara mdogo taasisi inakuongezea deni mara mbili zaidi. Hivi sisi tumewakosea nini nyie Bodi???

Naombeni ushauri jamani lakini sio vibaya wanufaika wenzangu mnaokatwa na Bodi hebu angalieni kwenu

Nawasilisha

====

PIA, SOMA:
- Mrejesho: Bodi ya Mikopo(HESLB) yasema haihusiki na changamoto iliyojitokeza kwenye Salary slip mwezi Juni
 
Hilo deni, bodi ni as if hawataki liishe. Hata ukimaliza kulipa na ukapewa barua ya kumaliza kulipa, siku moja ukijifanya kwenda kucheki tena unashangaa unadaiwa mamilioni. [emoji16]
Sasa Mkuu kama ulishamaliza na barua wakakupa unapelekwa Nini tena bodi, lazima wakupige hata laki sita hivi za kuwasumbua[emoji2][emoji2][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Hawa jamaa ni wezi, kuna jamaa yangu alianza kukatwa akiwa TGTS B, lakini Mwezi huu kapanda daraja. Baada ya uzi huu nimempigia akaniambia wamekata pesa ndefu ya TGTS C lakini kwenye salary slip, deni limepungua kwa elfu 16 tu badala ya kupunguza walichokata.

HESLB ni majipu
 
Mimi pia nina shida hiyo..

Tupate maelezo tafadhali.

Huu ni ujambazi kabisaa
 
Habari hii inabidi isambae kwenye mitandao yote ya kijamii
 
Ni uhuni juu ya uhuni, wizi juu ya wizi, kila mtu na kilio chake. Kuna mtu deni limepungua kwa sh. 19, yaani tofauti ya deni mwezi Mei na June ni sh.19, makato yameoneshwa kama ya mwez Mei. Wengine wamekatwa kiwango kikubwa zaidi ya makato ya awali, wengine deni limekuwa kubwa mara mbili zaidi ya hapo awali.

Huu ni uhuni wa kutisha, tunahitaji maelezo ya kina toka Bodi ya mikopo juu ya wizi huu na jinsi ya kuzipata hela za watu
 
Duhh. Mkuu embu naomba msaada wa number zao.
Mimi nimekatwa 173K

Ila kwenye deni inaonekana wamekata 50.
Hiyo 120 imeenda wapi?

Kuna uhuni hapaa.
Jaribu hii 0736 665 533
Pia watafute kupitia mitandao ya kijamii(FB, Twitter n.k) huko utapata namba zao zaidi hadi za WhatsApp
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…