Malalamiko ya Makato ya Deni la Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Mwezi Juni, 2021

Ni deni stahimilivu, hata nchi inalipa madeni kila mwezi ila deni la taifa likisomwa linakuwa limeongezeka🤣🤸🐒
 
Mimi nilishasema humu hiyo bodi ifutiliwe mbali, kazi ya kuratibu mikopo ya wanafunzi irudi wizarani.......sasa kwa sababu kuna watu wana vichwa vigumu kuelewa shida kama hizi unakuta haziishi....
 
Ni kweli nimeona wamekata hela na deni halijapungua itabidi bodi watoe ufafanuzi, maana wanaumiza watu
 
Daah aisee Mimi wamekata na deni lipo vile vile [emoji24][emoji24]

Hii nchi Hii?!! Basi tu
 
Mimi nahisi kuna tatizo kati mifumo yao na naamini watarekebisha maana karibia wanufaika wote wamekumbwa na balaa hilo
 
Habar wana JF,

Kupitia ukurasa huu napenda kutoa dukuduku langu na kama kuna wanaohusika bas hatua zichukuliwe

Bodi ya mikopo katika makato yao ya mwezi huu wa sita, makato yao hayaeleweki

Kwenye salary slip makato yao wameonesha kiwango walichokata lakini cha ajabu deni la msingi kiwango kilichokatwa hakiendani na kiwango kilichoandikwa

Kwa mfano:
Deni la bodi mwezi wa tano lilibaki 1050390/=
Kwa hyo baada ya makato ya tsh 141000/= ilitakiwa deni libaki 909,390/=
Lakini cha ajabu wameandika deni limebaki 1019325/=

Kwa hyo inamaana bodi wamekata shiling elf thelathin tu lakin kiuhalisia wamekata laki moja na elfu arobaini na moja

Huu wizi mnaotufanyia bodi sio uungwana kwa kweli.

Mnachofanya ni kuchonganisha serikali yetu yenye nia njema ya kuwakomboa watumishi wake.

Haki itendeke.

HaiwezekanI mshahara unakatwa zaidi ya 35%.
 
Mimi pia nimeona wamekata ila kiwango hakijapungua hata kidogo

Inamaana hela wamechukua ilaa deni limebaki pale pale

Uzembe huu urekebishwe Mara moja maana kuna wengi wanalalamika pia

HESLB OR HAZINA REKEBISHENI TAARIFA ZENU DENI LIPUNGUE
 
Habarini wadau, nauliza waliokwenda kuhakiki mikopo bodi ya elimu, ukitia retantion fee, je yapo makato mengine yaliyotoka kati ya penalt na administration fees?
 
Wafanyakazi wanahitaji vyama imara vya wafanyakazi kupambana na ukandamizaji kama huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…