Malalamiko ya Sheria Kandamizi: Rais Samia asema Serikali ipo tayari kupokea Mapendekezo kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Habari

Malalamiko ya Sheria Kandamizi: Rais Samia asema Serikali ipo tayari kupokea Mapendekezo kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Habari

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
1645173963242.png

Picha: Rais Samia akihojiwa na DW
Akiulizwa ikiwa Vyombo vya Habari kufungiwa kutategemea Hisani ya Kiongozi mmoja hadi mwingine au upo utaratibu wa kuhakikisha vinafanya kazi kama taratibu zinavyoelekeza, Rais Samia amesema Vyombo vya Habari vitafanya kazi kwa Mujibu wa Sheria

Katika Mahojiano Maalum na DW, Rais Samia ameeleza, "Vyombo vikikiuka Sheria vinafungiwa, ndiyo maana Sheria ipo. Hakuna Nchi ambayo ina Vyombo vya Habari vinafanya vinavyotaka bila kufuata Sheria"

Amesema Serikali ipo tayari kupokea Mapendekezo kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, ambapo baadhi ya vipengele vimekuwa vikilalamikiwa kuwa kandamizi
 
Sheria zinazotakiwa kurekebisha mfano Spika, mwanasheria mkuu na mwendesha mashitaka kutoshitakiwa zifutwe kabisa.
 
Back
Top Bottom