Malalamiko ya Simba yangeweza kujadiliwa hata baada ya mechi na adhabu stahiki ingetolewa!

Malalamiko ya Simba yangeweza kujadiliwa hata baada ya mechi na adhabu stahiki ingetolewa!

Wewe hufuatilii mpira bila shaka.

Wanaume wako (Yanga) waliwahi kugomea mechi ya derby dhidi ya Simba kisa muda umebadilishwa na bodi kinyume na kanuni.(Yaliongezwa "masaa" tu wala siyo hata siku)

Simba ilikubali kucheza dhidi ya Pamba Jiji juzi tu hapa pamoja na vurugu walizofanyiwa kwa maelekezo ya RC mwanayanga wakati wa mazoezi ya mwisho pale CCM Kirumba.
 
Hivi malalamiko baada ya kupoteza mechi kufuatia kukosa proper fitness iliyosababishwa na wapinzani, unadhani consequences yoyote kwenye hayo malalamiko yatampa faida Simba kwenye race ya Ubingwa?
mkuu umenufaika na kadi nyekundu mbona hakuna kelele
 
Mechi 4 mfululizo mlizokua na iyo poper fitness mbona mlikandwa? proper fitness lazima ufanyie mazoezi kwa mkapa? Sema tu simba mna inferiority complex mbele ya yanga.
Shangaa sasa!

Yani wiki nzima haijawatosha kupata fitness ila wanaamini masaa yasiyozidi sita yatawapa fitness ya kuifunga Yanga!

Simba wakubali tu wameiogopa Yanga.

Nyingine ni visababu visivyokuwa na kichwa wala miguu.
 
Mimi sio shabiki kindaki ndaki wa mpira lakini kwenye hili suala mashabiki inabidi na wao waoneshe msimamo wao. Wanachotakiwa kufanya ni kutokuingia uwanjani siku mpya ya mechi (itakayopangwa na bodi). Naamini kuna viongozi wa mashabiki wa hivi vilabu viwili, watoe msimamo wao kuwa pesa walizolipia kwenye mchezo huu zitumike kwenye michezo mingine ila sio mchezo mpya wa Yanga ya Simba. Wacheze wenyewe uwanjani bila mashabiki na mapato ya uwanjani ili liwe funzo waache kucheza na akili na pesa za mashabiki. Tofauti na hivyo hivi vilabu na hao TFF/Bodi hawataacha huu ujinga kamwe!
 
Katika management structure ya yanga hakuna department yoyote inayoitambua cheo cha baunsa wa yanga
Lakini kwenye logo wapo
markup_17414458367127428007539665003501.png
 
Waliotia aibu ni waanzilishi wa tatizo.

Usiangalie wapi umeangukia, angalia wapi ulipo jikwaa.
Mkuu una gubu...
Mtu akiamua kukutafutia kasoro atakupata tu.

Mmelitafuta tatizo mmelipata. Furahini basi.

Nauliza tena... Mlienda usiku ili mgundue nini!?

GUBU...
 
Mkuu una gubu...
Mtu akiamua kukutafutia kasoro atakupata tu.

Mmelitafuta tatizo mmelipata. Furahini basi.

Nauliza tena... Mlienda usiku ili mgundue nini!?

GUBU...
Hujui taratibu za kimpira kuhusu muda wa kufanya mazoezi unazingatia kitu gani ndio maana unaona kama kuna shida.

Simba imefika uwanjani saa 12 jioni. Kanuni zinasema timu inapaswa kufanya mazoezi muda sawa na ule muda ambao mechi itachezwa.

Muda wa mechi ilikuwa ni saa 19:15 kwa maana hiyo Simba walitakiwa kufanya mazoezi kuanzia muda huo.

Ila kwasababu wewe hujui hii sheria ndio maana unaendelea kuweka mawazo kuhusu ushirikina.
 
Kama mnaamini mngeweza kuifunga Yanga kwa mara nyingine simply mngefungua mageti tu bassss
 
Bodi ya ligi ilipaswa kutulia na kuyajadili malalamiko ya Simba kwa mujibu wa kanuni.
Aidha ingethibitika kuna ukweli Yanga au mashabiki wake wamefanya ndivyo sivyo adhabu stahiki ingetolewa ikiwemo kupokwa points kama kanuni za adhabu zinataka hivyo.

Bodi ni lazima itoe tamko la kikanuni kuonesha kuwa Kuna sababu ya kikanuni iliyopelekea mechi kuhairishwa.

Yanga ilivyoenda Congo kuikabili Mazembe ilifanyiwa figisu sana ila wanaume hawa waliingiza timu na wakapata matokeo.
Ulitaka wacheze bila mazoezi
 
Fujo za DRC zilifanyika baada ya mechi kumalizika ni tofauti na huu ujinga uliofanyika siku moja kabla ya mechi.

Inashangaza kumsikia shabiki wa Yanga akilalamika waliyofanyiwa kule Congo halafu wanashangilia upuuzi unaofanywa na makomandoo wao wanaofumbiwa macho na bodi ya ligi.

Ujinga ulianzia kule Mwanza kwenye mechi ya Pamba wakati makocha wakiswekwa ndani na Mkuu wa Mkoa. Yanga wanajidanganya kwamba wao ni serikali kwa hiyo upuuzi wowote wakiufanya ni sawa tu kwa mujibu wa fikra zao wenyewe!.

Kuna dhana potofu wanaihubiri kwamba Yanga ilipigania uhuru.

Ali Sykes mwanachama wa TANU kadi namba 2 alikuwa shabiki wa Simba.
Abduwahib Sykes kadi namba 3 ya TANU alikuwa shabiki wa Simba.
Mzee Rupia aliyekuwa na ghorofa Kariakoo alikuwa shabiki wa Simba
Rashid Kawawa waziri mkuu wa kwanza alikuwa shabiki wa Simba.

Ujinga huu wa kuitumia vibaya na kuichafua serikali kisa uhusiano ilionao na klabu ya Yanga unaichafua sana awamu ya sita. Samia hawezi kuona kwamba amezungukwa na wapuuzi wengi wenye ushamba wa madaraka na tunapoelekea zile milioni tano anazozitoa kwenye mechi za kimataifa zinakwenda kumharibia heshima yake badala ya kumjenga.
 
Mechi 4 mfululizo mlizokua na iyo poper fitness mbona mlikandwa? proper fitness lazima ufanyie mazoezi kwa mkapa? Sema tu simba mna inferiority complex mbele ya yanga.
Kinachotafutwa ni uhalali wa huo ushindi wa mfululizo.
 
Hivi malalamiko baada ya kupoteza mechi kufuatia kukosa proper fitness iliyosababishwa na wapinzani, unadhani consequences yoyote kwenye hayo malalamiko yatampa faida Simba kwenye race ya Ubingwa?
Proper fitness!? Training ya mwisho huwani kwa ajili ya proper fitness au kuuzoea uwanja?
 
Back
Top Bottom