Malalamiko ya Simba yangeweza kujadiliwa hata baada ya mechi na adhabu stahiki ingetolewa!

Yanga hao hao wanaringia uhusiano wao na serikali kiasi cha kuwa sawa na malimbukeni wa mpira.

Kunifunga mara nne mfululizo sio hoja nzito ikiwa wewe ni mtu wa mpira. 2004-2005 tuliwafunga mechi tano mfululizo mpaka tukawapa jina la yeboyebo. Nyuma mwiko taabu sana.
 
View attachment 3263914
Tatizo unafuatilia habari za vijiweni
Sheria haisemi upige simu kutoa taarifa.

Simba wangekuja asubuhi kweli wakihitaji kupiga simu kwasababu wapo nje ya taratibu.

Sheria inataja wazi kuwa muda tajwa hapo ni muda ambao uwanja unakuwa kwenye umiliki wa timu ngeni kwa ajili ya kufanya mazoezi.

Maana yake nyinyi mlipaswa kufanya mambo yenu katika uke muda ambao ni halali kwenu halafu baada ya hapo msepe waje Simba kutimiza wajibu wao kisheria.
 
Walichotaka Simba ni heshima. Simba kupeleka timu tafsiri yake ni kuwa Yanga wanaweza kufanya chochote mbele ya Simba. Mara nyingi Simba wanakuwa wastaarabu sana ila kwa kile kilichotokea Jana ni dharau sana. Mambo Yale tumezoea kufanyiwa na timu za kaskazin tena miaka 90 huko.
 
Taratibu zinalazimisha timu kutoa taarifa kwa wasimamizi wa uwanja ili taratibu zifanyike. Sio kujikurupukia tu kwenda uwanjani.

Lakini pia, uwanja wa mpira sio kilinge cha wachawi. Timu inaingia na mabasi mawili ya nini?

Halafu kuna KANUNI zinazoongoza ligi. Iwapo timu mwenyeji itazuia mazoezi ya timu nyingine kanuni zinasemaje? Unadhani ni sahihi Simba kugomea mchezo kwa sababu za kitoto namna hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…