neo1, post: 25232719, member: 167873 ahsante kwa maelezo yako mkuu,
kutokana na hali inayoendelea Syria ikiwa kwa asilimia kubwa utawala wa Al Assad umefanikiwa kubaki madarakani,na wameweza kukomboa eneo kubwa toka mikononi mwa waasi na wanamgambo.Ila Marekani wamegoma kuondoka
nini Syria anaweza kufanya kulazimisha Marekani aondoke.
Mkuu hili swali ni gumu na refu kidogo.
Sisi watu wa nje ni watazamaji tu na tunajaribu kuunganisha matukio na mwishowe kujaribu kutabiri nini kitatokea.
Lakini Marekani hawezi kuondoka Syria leo au kesho kwasababu itakuwa ni hatari sana kwa Usalama wa Israel na maslahi yake. Hasa hasa kipindi hiki ambacho Mrusi kasema ana mpango wa kutaka kuitanua kambi yake ya Jeshi iliyoko nchini Syria ili ifanye kazi kama ilivyokuwa kipindi cha Soviet Union.
Marekani hawezi kuondoka kwasababu ya kitu kinaitwa Balance of Power,
Uwepo wa Urusi na Iran umekuwa ni mkubwa sana pale Syria hivyo kupelekea ushawishi wake kukua kwa kasi hasa baada ya hiki kipindi cha Ushindi huu mzito ulio wadhalilisha Wamarekani. Hivyo kuzua kuendelea kwa huu ushawishi wa Urusi ni lazima Marekani atafute njia yoyote kubaki na hili Urusi analijua ndiyo maana yeye na Syria hawafanyi vurugu.
Pia upande wa pili,
Uwepo wa kambi ya jeshi ya Urusi nchini Syria unampa uwezo Urusi kufanya kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya maaduia zake ambao wako kwenye ule Ukanda. Kibaya zaidi Marekeni anaogopa kwamba uwepo wa Urusi eneo lile unaamanisha kwamba Iran na Hezbollah watakuwa wanapata Free Passage and The Right to Roam. Hivyo watakuwa wanapata silaha kwa urahisi na wanapigana kisha wanajificha chini ya mgongo wa Urusi kama kipindi hiki.
Iran na Hezbollah wakiwa na nguvu inamaanisha,
Israel, Yemen, Saudi Arabia na Jordan itakula kwao kabisa.
Ukitazama ndiyo utaona kabisa Marekani baada ya kuona Ushawishi wa Iran unakuwa mkubwa akaamua kuongeza vikosi vyake kwenye mpaka wa Iran pale Afghanistan, kutokea wanajeshi 11000 mwezi hadi mwezi Agosti 2017 kufikia wanajeshi 14000 hadi 15000 mwaka huuu. (Anatuma ujumbe)
NB: Taarifa nyingine zinasema Pentagon wana mpango mwingine kabisa wa kutaka kukata kipande cha Syria na kutengeneza nchi ya Wakurdi ambayo kwa namna moja au nyingine itakuwa Client au Satellite State ya Marekani.
Lakini ili kufanya hivi anahitaji support kubwa sana ya Kidiplomasia ya nchi za Ulaya na Mashariki ya kati. Ili iwe kama ilivyokuwa kule Yugoslavia.
Bahati mbaya sana Ulaya hawataki kulisikia kabisa hili,
Hasahasa nchi ya Uturuki hataki kabisa kuwasikia Wakurdi wakipewa nchi.
Anahofia usalama wake.............
Pia elezea nini kinaendelea Iran na maandamano yake...je kwa maoni yako kuna dalili za kuanguka kwa utawala wa Iran
kama tawala za Iraq na Libya???
Mpaka jana Usiku Serikali ya Tehran ilikuwa imefanikiwa kuyathibiti yale maandamano kwa Asiliamia 80%
Mkuu wa Iran Revolutionary Guard kasema wamefanikiwa kuzuia mamluki waliotaka kuleta vurugu.
Kulikuwa na massive imprisonment, shutdown of the Internet, crackdown of foreign media na counter protest.
Hii iliwahi kutokea miaka ya nyuma kipindi cha Ahmedinejad,
Watu waliandamana na Iran Revolutionary Guard ikaandaa Counter Protest kubwa sana nchini.
Kukawa na makundi mawili yanayoandamana yenye mlengo tofauti, hivyo majasusi ya Iran yakafanya fujo na kuanza kuua watu yakisingizia ni waandamanaji. (Iran is very sophisticated tofauti kabisa na Libya)
NB: Lengo la Marekani katika hili lilikuwa ni kutaka kutumia kwanza Diplomasia kabla ya kutumia jeshi au vikwazo.
Juzi ya tarehe 5 kulikuwa na kika cha Dharura cha Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa mataifa na Agenda kuu ilikuwa ni vurugu za Iran. Marekani alipeleka pendekezo kwamba Umoja wa Mataifa Ulaani yale mauaji na Uchukue hatua Stahiki kama kuongezea Iran vikwazo vya kiuchumi. Kwasababu lile dili la Obama Trump anashindwa kulivunja kirahisi kwasababu linahusisha nchi kibao hivyo akaamua kependekeza vikwazo ili kuzorotesha maendeleo ya Iran.
Urusi na nchi nyingine walikataa Ule mswada kwasababu walisema zile vurugu ni very Sporadic,
Hazijafikia Threshold ya kuweza kuhatarisha Usalama wa dunia hadi kupelekea Umoja wa mataifa kuchukua hatua nzito.
Hivyo wakasema kama kuna Uvunjifu wa haki za binadamu, sehemu sahihi ya Kupeleka ni kwenye Human Rights Commission na siyo Security Council. Hivyo Muswada ukafa.
Kikubwa zaidi ni kwamba,
Ripoti ya Katibu Mkuu Msaidizi ilisema kwamba "Wanasikia" kwamba watu wamekufa lakini wale Specila Rapporteurs hawajapata nafasi ya kuthibitisha haya madai mbele ya Baraza hivyo wanaendelea kufanya Uchunguzi.
Mpango wote Ukapingwa na Wajumbe wa Baraza wakiwemo Ethiopia na Bolivia.
Iran bado kainuka kidete....
Tafuta mtandaoni ile Session Utaelewa kila kitu ninachokisema hapa......
NB: Iran siyo Libya wala Iraq, wale ni watu wengine kabisaaaa.
CC:
neo1