Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

neo1, post: 25232719, member: 167873 ahsante kwa maelezo yako mkuu,

kutokana na hali inayoendelea Syria ikiwa kwa asilimia kubwa utawala wa Al Assad umefanikiwa kubaki madarakani,na wameweza kukomboa eneo kubwa toka mikononi mwa waasi na wanamgambo.Ila Marekani wamegoma kuondoka
nini Syria anaweza kufanya kulazimisha Marekani aondoke.

Mkuu hili swali ni gumu na refu kidogo.
Sisi watu wa nje ni watazamaji tu na tunajaribu kuunganisha matukio na mwishowe kujaribu kutabiri nini kitatokea.
Lakini Marekani hawezi kuondoka Syria leo au kesho kwasababu itakuwa ni hatari sana kwa Usalama wa Israel na maslahi yake. Hasa hasa kipindi hiki ambacho Mrusi kasema ana mpango wa kutaka kuitanua kambi yake ya Jeshi iliyoko nchini Syria ili ifanye kazi kama ilivyokuwa kipindi cha Soviet Union.

Marekani hawezi kuondoka kwasababu ya kitu kinaitwa Balance of Power,
Uwepo wa Urusi na Iran umekuwa ni mkubwa sana pale Syria hivyo kupelekea ushawishi wake kukua kwa kasi hasa baada ya hiki kipindi cha Ushindi huu mzito ulio wadhalilisha Wamarekani. Hivyo kuzua kuendelea kwa huu ushawishi wa Urusi ni lazima Marekani atafute njia yoyote kubaki na hili Urusi analijua ndiyo maana yeye na Syria hawafanyi vurugu.

Pia upande wa pili,
Uwepo wa kambi ya jeshi ya Urusi nchini Syria unampa uwezo Urusi kufanya kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya maaduia zake ambao wako kwenye ule Ukanda. Kibaya zaidi Marekeni anaogopa kwamba uwepo wa Urusi eneo lile unaamanisha kwamba Iran na Hezbollah watakuwa wanapata Free Passage and The Right to Roam. Hivyo watakuwa wanapata silaha kwa urahisi na wanapigana kisha wanajificha chini ya mgongo wa Urusi kama kipindi hiki.

Iran na Hezbollah wakiwa na nguvu inamaanisha,
Israel, Yemen, Saudi Arabia na Jordan itakula kwao kabisa.
Ukitazama ndiyo utaona kabisa Marekani baada ya kuona Ushawishi wa Iran unakuwa mkubwa akaamua kuongeza vikosi vyake kwenye mpaka wa Iran pale Afghanistan, kutokea wanajeshi 11000 mwezi hadi mwezi Agosti 2017 kufikia wanajeshi 14000 hadi 15000 mwaka huuu. (Anatuma ujumbe)

NB: Taarifa nyingine zinasema Pentagon wana mpango mwingine kabisa wa kutaka kukata kipande cha Syria na kutengeneza nchi ya Wakurdi ambayo kwa namna moja au nyingine itakuwa Client au Satellite State ya Marekani.
Lakini ili kufanya hivi anahitaji support kubwa sana ya Kidiplomasia ya nchi za Ulaya na Mashariki ya kati. Ili iwe kama ilivyokuwa kule Yugoslavia.

Bahati mbaya sana Ulaya hawataki kulisikia kabisa hili,
Hasahasa nchi ya Uturuki hataki kabisa kuwasikia Wakurdi wakipewa nchi.
Anahofia usalama wake.............

Pia elezea nini kinaendelea Iran na maandamano yake...je kwa maoni yako kuna dalili za kuanguka kwa utawala wa Iran
kama tawala za Iraq na Libya???

Mpaka jana Usiku Serikali ya Tehran ilikuwa imefanikiwa kuyathibiti yale maandamano kwa Asiliamia 80%
Mkuu wa Iran Revolutionary Guard kasema wamefanikiwa kuzuia mamluki waliotaka kuleta vurugu.
Kulikuwa na massive imprisonment, shutdown of the Internet, crackdown of foreign media na counter protest.

Hii iliwahi kutokea miaka ya nyuma kipindi cha Ahmedinejad,
Watu waliandamana na Iran Revolutionary Guard ikaandaa Counter Protest kubwa sana nchini.
Kukawa na makundi mawili yanayoandamana yenye mlengo tofauti, hivyo majasusi ya Iran yakafanya fujo na kuanza kuua watu yakisingizia ni waandamanaji. (Iran is very sophisticated tofauti kabisa na Libya)

NB: Lengo la Marekani katika hili lilikuwa ni kutaka kutumia kwanza Diplomasia kabla ya kutumia jeshi au vikwazo.
Juzi ya tarehe 5 kulikuwa na kika cha Dharura cha Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa mataifa na Agenda kuu ilikuwa ni vurugu za Iran. Marekani alipeleka pendekezo kwamba Umoja wa Mataifa Ulaani yale mauaji na Uchukue hatua Stahiki kama kuongezea Iran vikwazo vya kiuchumi. Kwasababu lile dili la Obama Trump anashindwa kulivunja kirahisi kwasababu linahusisha nchi kibao hivyo akaamua kependekeza vikwazo ili kuzorotesha maendeleo ya Iran.

Urusi na nchi nyingine walikataa Ule mswada kwasababu walisema zile vurugu ni very Sporadic,
Hazijafikia Threshold ya kuweza kuhatarisha Usalama wa dunia hadi kupelekea Umoja wa mataifa kuchukua hatua nzito.
Hivyo wakasema kama kuna Uvunjifu wa haki za binadamu, sehemu sahihi ya Kupeleka ni kwenye Human Rights Commission na siyo Security Council. Hivyo Muswada ukafa.

Kikubwa zaidi ni kwamba,
Ripoti ya Katibu Mkuu Msaidizi ilisema kwamba "Wanasikia" kwamba watu wamekufa lakini wale Specila Rapporteurs hawajapata nafasi ya kuthibitisha haya madai mbele ya Baraza hivyo wanaendelea kufanya Uchunguzi.
Mpango wote Ukapingwa na Wajumbe wa Baraza wakiwemo Ethiopia na Bolivia.
Iran bado kainuka kidete....

Tafuta mtandaoni ile Session Utaelewa kila kitu ninachokisema hapa......

NB: Iran siyo Libya wala Iraq, wale ni watu wengine kabisaaaa.

CC: neo1
 
Habari Mkuu.

Heri ya Mwaka mpya.

Nina maswali mengi sana sana. Nataka nikueulize lakini mm naomba nifungue uzi wa Interview yako ili na wengine wakuulize.
Wasalaam ndugu zangu,
Heri ya mwaka mpya 2018.
Binafsi nashukuru kudra za Mwenyezi Mungu kunifanya niuone huu mwaka mpya.

Dhumuni la kuanzisha uzi huu ni kutaka tufahamiane zaidi, tukosoane na turekebishane ili mwaka huu wa 2018 tulifanye jukwaa hili liende sawia kwa michango mbali mbali ambayo tutakiwa tunatoa.

Binafsi mimi naipenda sana JF,
Hili ni tanuli za fikra na natumaini mchango wetu ni mkubwa sana katika jamii ya Tanzania hata kama Serikali, vyombo vya habari na mashirika ya mbali mbali hawaukubali huu ukweli.

Humu ndani tunaishi kama ndugu,
Tunakosoana, tunasifiana, tunakashifiana na hata kutukanana lakini mwisho wa siku UKWELI UTABAKI kwamba KILA MWANA CHAMA ANAMHITAJI MWENZAKE, haijalishi ni tajiri, maskini, msomi au mtu ambaye hajasoma.

Binafsi naishukuru sana JF na wanachama wote. Mimi kama mwanachama nitaendelea kuipenda sana JF na ntazidi kuchangia kwasababu natumai kwa hichi kidogo nilicho nacho naweza kuwagusa watu wawili watatu ndani ya jamii yetu.......

NB1: Baada ya kusema haya yote naruhusu maswali na maoni mbalimbali kuhusu MALCOM LUMUMBA pamoja na maandishi yake humu ndani ya Jukwaa hasa hasa kule SIASANI, JAMII INTELLIGENCE na INTERNATIONAL FORUMS.....

Pia wale wenye madukuduku au kero naomba waseme hapa ili niwaombe msamaha na tuanze huu mwaka vizuri..........

NB2: Unaweza kuuliza swali lolote lile kuhusu MALCOM LUMUMBA lakini naomba lisilenge kumkashifu mtu yeyote yule.

Natanguliza shukrani zangu......
Young Malcom........

CC: Consigliere, cognition, hearly, MSEZA MKULU, mngony, ze kokuyo, espy, Dragoon, Baazigar, RRONDO, Victor wa happy, Red Giant, Da'Vinci , Tobinho, mtembea kwa miguu, born again pagan, God Heals, FisadiKuu, UncleBen, Quinine Mwitu, Complex
 
Habari Mkuu.

Heri ya Mwaka mpya.

Nina maswali mengi sana sana. Nataka nikueulize lakini mm naomba nifungue uzi wa Interview yako ili na wengine wakuulize.

Mkuu wewe uliza hapa hapa, maan mengi nishayajibu!
Hata yakiwa mengi nitajitahidi kukujibu kwa kadiri ya uwezo wangu.
Karibu sana kiongozi....
 
I hope u are somebody in this country, unauwezo wa hali ya juu sana kwenye mambo mengi Siasa, Uchumi, biashara, Utamaduni, ujasusi.

Unalizungumziaje swala la T Lissu kushutiwa dodoma..?
Mimi nina Bachelor tu mkuu.


Nilitokea kupenda sana Falsafa za Malcom X (Brother Shabaz) na huyu ndugu Patrice Emery Lumumba,
Hivyo nikayaunganisha kutengeneza jina Malcom Lumumba.
 
I hope u are somebody in this country, unauwezo wa hali ya juu sana kwenye mambo mengi Siasa, Uchumi, biashara, Utamaduni, ujasusi.

Unalizungumziaje swala la T Lissu kushutiwa dodoma..?

Mkuu,
Yes I am somebody in this country " A Citizen who loves his country with all his heart"
Kuhusiana na Swala la Tundu Lissu ninalaani sana lile Shambulio kwasababu ni Uvunjifu wa Haki za Binadamu, Pia linahatarisha Amani na Usalama wa nchi yetu.. (Siyo jambo jema hata kidogo)

NB: Siwezi kuzungumzia zaidi ya hapa kwasababu jambo hili kwasasa liko chini ya Uchunguzi wa vyombo vya dola.
 
Ombi.

Naomba links za nyuzi zako zoooote Ulizoanzisha majukwaa ya Jf Intell,, zInternational etc nikaongeze maarifa..
Mkuu,
Yes I am somebody in this country " A Citizen who loves his country with all his heart"
Kuhusiana na Swala la Tundu Lissu ninalaani sana lile Shambulio kwasababu ni Uvunjifu wa Haki za Binadamu, Pia linahatarisha Amani na Usalama wa nchi yetu.. (Siyo jambo jema hata kidogo)

NB: Siwezi kuzungumzia zaidi ya hapa kwasababu jambo hili kwasasa liko chini ya Uchunguzi wa vyombo vya dola.
 
Ombi.

Naomba links za nyuzi zako zoooote Ulizoanzisha majukwaa ya Jf Intell,, zInternational etc nikaongeze maarifa..

Mkuu,
Nimeendika nyuzi nyingi sana hadi nimesahau.
Nipe muda nizitafute halafu nitajulisha kupitia (Tag).
 
ahsante mkuu kwa majibu yako mazuri mkuu, najifunza vingi.pole kwa maswali mengi..

pamoja na vikwazo vingi ambavyo north korea imewekewa ila imeendelea kufanya vizuri kwenye ukuaji wake wa uchumi,na kwenye program zake za siraha za nuclear, nini hasa kimefanya kwa muda wa miaka 2 imepiga saana hatua kwenye mipango ya hiyo ya siraha za masafa marefu na nucliear wakati imekuwa sabotage kwa namna nyingi..

Je NK anapata wap tecnolojia ya kutengeneza siraha,mbona yeye silaha zake anatengeneza na anauza kwa bei rahisi??

kwa mtazamo wako je kuna dalili marekani ikakubali NK kuwa na nuclear weapon??, ikitokea imekubali vipi kuhusu SK au Japan watakubali kuachia ipite hivi hivi??
 
Back
Top Bottom