Malecela avunja ukimya!

Malecela avunja ukimya!

- Hivi kuna tatizo gani mimi nikisema ni lazima Dr. Slaa awe rais kwenye uchaguzi ujao? Sasa kama DK. Malecela anamtaka Rais Kikwete aendelee tatizo likpo wapi kwani hatakiwi kuwa na choice zake binafsi na kuzisema wazi kama sisi raia wengine?

- Naomba elimu hapo?

FMES!

Malecela anawasakama wana CCM wanaotaka kugombea urais kinyume na katiba na miongozo ya CCM.Hakuna sehemu yoyote inayosema rais incumbent asipingwe, anatumia ukiritimba tu ku force hoja zake binafsi

Anatumia ubabe na heshima yake kuanza kupiga kampeni kable ya kipindi cha kampeni, anaweka maslahi yake binafsi na mfumo wa kulindana mbele kuliko maslahi ya taifa.
 
FM ES,

Tz tungepata mtu mwenye uchungu na mzalendo kama Slaa nchi ingesonga mbele kwa haraka zaidi!

Je CHADEMA watampitisha badala ya Mbowe?

Ila bado upinzani Tz!

Ila akisimama kama mgombea binafsi atapata kura nyingi..sema kuishinda CCM may be sii rahisi!!!
 
- DK, ametoa mawazo yake na ni haki ya kila mwananchi wa Tanzania wewe na mimi inluded kufanya hivyo, kama CCM sio chama changu I could care less what member mmoja has to say, kwa sababu in the end ni CCM collectivelly ndio wanaoamua nani agombee nani asigombeee regarding thie katiba.

- Ni haki kwa DK. Malecela kutoa hoja zake binafsi, kama wewe na mimi tulivyo na hiyo haki, unless amevunja katiba yetu kwa kutoa maoni yake binafsi, mkuu hapa ni mahali pa great thinkers please!
 
FM ES,

Tz tungepata mtu mwenye uchungu na mzalendo kama Slaa nchi ingesonga mbele kwa haraka zaidi!

Je CHADEMA watampitisha badala ya Mbowe?

Ila bado upinzani Tz!

Ila akisimama kama mgombea binafsi atapata kura nyingi..sema kuishinda CCM may be sii rahisi!!!

- Ndio maana mimi ni mwanachama hai wa CCM, lakini niampigia ngoma DR. Slaa kwenye urais ujao, regardless of what DK. Malecela thinks ambayo ni haki yake anyways.
 
Huyu mzee siyo tu kwamba kachoka bali amepitwa na wakati; tumpuuze. Ebu soma nukuu hizi:
1. "Alisema wakati huu wa hali mbaya ya kiuchumi, viongozi wanapaswa kuweka mikakati ya kumsaidia Rais Kikwete ambaye amekuwa akiizunguka dunia kutafuta misaada ya Tanzania, badala ya kuendekeza malumbano."

Anajifanya kipofu kwa kutojua malumbano anayoyakataa yanahusu nini. Malumbano ya Dowans yanahusu uchumi wa Taifa, hivyo kama matatizo ya Dowans na mengine mengi yanayofanana na hayo yasingekuwapo basi Rais asingehangaika kuzunguka dunia kutafuta misaada. Hivi Mzee huyu anaona kazi ya rais kuzunguka akitembeza bakuli kama ombaomba ni ya kujisifia? Haoni ni aibu ukilinganisha na utajiri wa nchi hii.
Tunajua kwa nini anasema hivyo. Wakati CCM inachota fedha kupitia Kagoda yeye si alikuwa na wadhifa mkubwa CCM? Bila shaka alichota.

2 ."Vile vile, Malecela alisema kamwe CCM haitaruhusu matajiri kuongoza chama hicho na kwamba wanaojaribu kufanya hivyo wanajidanganya."

Huu nao ni upofu wa ajabu. Angalia RA, Karamagi, EL, Patel, Chenge (vjisenti), na wengine wengi. Na hawa wanatumia nguvu yao ya pesa kupata uongozi ndani ya CCM. Hivi anavyosema matajiri hawatakiteka chama, mbona wameshakiteka?

Wakuinusuru nchi ni sisi wananchi kwa kuitupa hiyo CCM.
 
FM ES,

Tz tungepata mtu mwenye uchungu na mzalendo kama Slaa nchi ingesonga mbele kwa haraka zaidi!

Je CHADEMA watampitisha badala ya Mbowe?

Ila bado upinzani Tz!

Ila akisimama kama mgombea binafsi atapata kura nyingi..sema kuishinda CCM may be sii rahisi!!!

kuishinda CCM ni rahisi sana; ni sisi kuamua tu. Usikate tamaa.
Angalia yaliyotokea Madagascar - rais mwenyewe anaachia ngazi. Je walivyokuwa wameanza Pemba, tukipokea wa Bara tukajumuisha na haya ya ufisadi, unadhani Ikulu patakalia? Ogopa nguvu ya Umma
 
- Mkuu sijaona popte pale unapojibu swali, Obama ameichagua timu ya North Carolina kushinda ubingwa wa NCAA what is wrong with that?

- Mkuu haya mambo wakati mwingine mnaya-over do, DK. Malecela anayo haki kama wananchi wengine wote kusema anayofikiri na ndio demokrasia yenyewe tunayoitaka, otherwise ni ku-reveal our inferior na fear.

- Kwenye demokrasia huwezi kumwambia mwananchi yoyote akae kimya kwa sababu hutaki mawazo yake, that is low mkuu! Badala ya siasa na great thinkers mnashusha hadhi wakuu!

FMes,

Na mie nasema hichohicho ila naona kila mtu anatafasiri kivyake. Mzee ni mtu powerful ndani ya CCM. Na kama Mtanzania alivyosema, ndiye mtu pekee kwa sasa mbaye kabaki kuijenga CCM kwa muda mrefu kuliko wote humo ndani. Hii inamfanya yeye kuwa BABA wa chama kwa sasa. Sasa Mzazi huyo, ingelikuwa heri awe NEUTRAL ili hiyo DEMOKRASIA ichukue mkondo wake ndani ya chama na hata kwa nchi kwa ujumla.

Kusema, mtu asigombee na hizo hela heri azitumie kuiendeleza familia yake unaona inaongeza demokrasia ndani ya chama/nchini? Hiyo nayo si unaweza kuiita KUWANYAMAZISHA wanachama wa CCM?
Kusema kaa kimya, sina maana asisime awe bubu. Hapa usitake kuleta maana ambayo mie sikuwa nayo. Ni kuelewashana na si kushindana.

Juu ya Obama kuchagua timu itakayoshinda, ni sawa na Pelle achague timu itakayoshinda. Ila hayo maneno akisema Boss wa NCAA, mhhh italeta sana utata. Hivyo siku zote inategemea nani anasema. Kama Malecela akisema chochote juu chaguzi za CHADEMA, mie ntamuunga mkono. Ni mawazo yake na hayo mawazo yake hayataleta efect yoyote ndani ya Chadema.

Umesahau Maneno ya Nyerere juu ya Lowassa/Malecela/Mwinyi? Kilichofuata ni action tu. Mungu bariki Malecela si powerful kama Nyerere, maana angelikuwa ni yeye basi hiyo ni asilimia 99 kuwa Kikwete kashashinda ndani ya CCM na atabaki yeye peke yake kwenye elimination.

Mwisho si kuwa tuna Over-do. Mzee anastahili heshima zake na anapewa. Na ni hizo hizo heshima ndiyo pia tunazitumia kumuhukumu mara anapoanza kutenga baadhi ya WANAE. Sijui kama umenielewa
 
Last edited:
- Kwenye demokrasia huwezi kumwambia mwananchi yoyote akae kimya kwa sababu hutaki mawazo yake, that is low mkuu! Badala ya siasa na great thinkers mnashusha hadhi wakuu!

Kwa principle hiyo hiyo Malecela hawezi kuwaambia wana CCM wanaotaka kushindana na Kikwete "wanapoteza muda na watapoteza pesa zao" which amounts to the same thing as "kaeni kimya"

Kama unasema mimi siwezi kumzuia malecela kusema kwamba hataki watu wam challenge Kikwete, kwa principle hiyo hiyo unatakiwa uweze kuona kuwa Malecela hana haki ya kuwaambia watu wengine wasi m challenge Kikwete.

Kwanza hamna campaign regulation laws zinazozuia kuanza kampeni kabla ya kutangaza rasmi?
 
Maneno ya Mzee JSC Malecela yanikumbusha hadithi ya vipofu watano wakijaribu kumwelezea Tembo kila mtu kwa nafasi yake na alipomgusa, kuna mmjoa alisema tembo ni kama ukuta, mwingine ni kama Mti....kwasababu wote ni vipofu kulikuwa na majibu 5 ambayo kila kipofu aliyaona ni sahihi ambayo hawakukubaliana kabisa. Huenda mzee Malecela kwa fikra zake anahisi yupo sahihi hata kama amechemka kisiasa.

NB

Reality may be viewed differently depending upon one's perspective, suggesting that what seems an absolute truth may be relative due to the deceptive nature of half-truths.

main_logo.jpg
 
mzee anapalilia kitumbua chake, si mnajua yeye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm kwa maisha yake yote?

Mtazamo wangu ni kuwa analinda kitumbua chake (na ikiwezekana kizazi chake) kama MDAU WA KUDUMU WA TABAKA TAWALA kwa maisha yake yote ambapo CCM kama NGOME YA TABAKA LAKE itaendelea kuwa MADARAKANI.

omarilyas
 
Tatizo si Mzee Malecela Kuexpress mawazo yake the big picture ni kwamba viongozi wetu wako makini sana katika kutetea maslahi yao na ya vizazi vyao binafsi hili ndilo linalotufanya tuwatoe thamani na hii haikuanza leo ama jana hii ipo tokea tulipopata uhuru.UBINAFSI.Wanajamii nambieni hivyo sababu ya msingi ya huyu mzee wetu kuitsha huu mkutano wote tunakubaliana ni kwa manufaa yake analinda kitumbua chake na anamkampenia Kikwete.Is Kikwete more qualified candidate among CCM ? the answer is NO by far.Tumemjaribu ameshindwa,tuna makesi ya ufisadi hayana hata muelekeo.Ameonyesha uoga wa hali ya juu katika uongozi wake.Then huyu mzee anakuja kutubabaisha na sisi tunampa attention.STOP>STOP>STOP. THINK TWICE.

SAHIBA.
 
FMes,

Na mie nasema hichohicho ila naona kila mtu anatafasiri kivyake. Mzee ni mtu powerful ndani ya CCM. Na kama Mtanzania alivyosema, ndiye mtu pekee kwa sasa mbaye kabaki kuijenga CCM kwa muda mrefu kuliko wote humo ndani. Hii inamfanya yeye kuwa BABA wa chama kwa sasa. Sasa Mzazi huyo, ingelikuwa heri awe NEUTRAL ili hiyo DEMOKRASIA ichukue mkondo wake ndani ya chama na hata kwa nchi kwa ujumla.

- Kiongozi wa CCM kama DK. Malecela, anawezaje kuwa neutral? Lini kiongozi wa Democrat aliwahi kuwa neutral kule US?

- analinda kutumbua kipi wakati ni waziri mkuu mstaafu na makamu wa kwanza wa rais, anayepewa mafao na katiba ya jamhuri?

Unajua wakuu mnaharibu kitu kimoja tu ni kwamba mnashindwa kuwasiaida wananchi wa kawaida na hizi hoja, badala ya kcuhambua what the man said kuhusiana na taifa lao, mimi nimemuelea kwamba yeye ni member wa CCM ameongea kwa faida ya chama chake, na kuonyesha wazi kwamba angetaka Rais wa sasa achaguliwe tena na mimi ninasema ningependa DK. Slaaa apewe next uchaguzi, na wewe sema ungependa nani awe rais next,

- Lakini ya kwamba ana nguvu nyingi sana na the rst of the story mna-over do to for nothing, elimisheni wananchi wakuu kwa sababu believe me jana amekisaidia sana chama chake CCM. kwa sababu ndio imepita hiyo!

Do you know who is overdoing ? ni CCM wanataka kuwa overshadow wapinzani na wao wasivyo na strategy wamekaa kimya hawajui la kufanya instead of taking advantage na huu msuguano wa CCM wameduwaa kama hawaexist katika taifa lenye demokrasia.Wanasubiri wakati wa kampeni uanze wenzao wanawafunika wanaanza kampeni mapema hapo watakaposhtuka itakuwa too late.Wapinzani Wamelala Tanzania. THINK TWICE.

- CCM hawana msuguano ila wana-practise demokrasia ambayo haikwepo ndani ya chama chetu kwa muda mrefu sana, DK. Malecela ni CCM tena damu, jana amekisaidia sana chama chetu kuliko mnavyofikiri, kwa sababu kama mjumbe wa CC ameweka wazi changamoto ya mgombea anyemtaka maana huu ni wakati wa uwazi, ingekwua zamani angejificha ficha na kufanya kampeni za chini chini.

- Sasa ajitokeze mjumbe mwignine aweke wazi anamtaka nani kuwa rais next, matatizo ya upinzani sisi CCm hayatuhusu, na the fact kwamba sasa hata upinzani nao wako involved na demokrasia ya malumbano ya CCM kwangu ni kichekesho kikubwa sana, eti CCM wanaweza kugombana ili kuwasadia upinzani?

Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Wewe kama CCM lazima ufurahi kwa sababu Chama chako kinafaidika hapa na wapinzani wanagubikwa bila kujijua na watakaposhtuka again it will be too late.With all this circus,we know Hakuna upinzani Tanzania they are so weak.Upinzani unatakiwa kustep up.

SAHIBA.
 
FMES,
Mkuu hata kama asingesema ukweli ni kwamba JK ndiye mgombea wa CCM mwaka 2010.. Haya mawazo ya watu wengine nje ya ukweli huo ni kujipa moyo tu. Hao waliouliza kama Malecela atagombea mwaka 2010 hawafahamu taratibu, lakini mimi nataka kufahamu Mh. malecela kasema hayo kwa sababu anamuunga mkono JK au kasema kulingana na taratibu za chama hata kama sio chaguo lake..
 
- Wapinzani wanaponzwa na sisi baadhi yetu na michango isiyokuwa makini, matusi mengi na kejeli, bila ya kujua the agenda ya jana na Malecela, the agenda ilikuwa kuwafahamisha wanaotaka kuleta vurugu ndani ya CCM kwamba wanajulikana tayari na njama zao, sasa waache mara moja, tusaidiane kuweka nguvu moja CCM tumsaidie rais wa sasa awe rais tena, that is all what was needed na believe me ujumbe umefika unakolengwa.

- Uchaguzi ujao utakuwa smooth bila matatizo as opposed na asingeongea jana, ndio maana ya kuwa na wazee wa chama, au wa kijiji, ya upinzani sisi hayatuhusu shauri yao.

Agenda ilikuwa Stalinism, kwamba kama una kitu cha kuongea kilete bungeni behind closed doors(ambako Spika Six atakuziba mdomo akiona unavuka mpaka) au Chamani (ambako Kingunge and company watakurarua ukivuka mpaka).Huko kote behind closed doors, halafu wananchi wakipata story inakuwa tayari spinned mpaka haieleweki.

Agenda ilikuwa kuwatisha watu wasipeleke mambo kwenye press conferences ambako mambo yataanikwa wazi.

Agenda ilikuwa JF wasipate mp3 audio hapa live na kuwararua wazembe wazembe.

Agenda ilikuwa kuendeleza ukiritimba, kutokomeza "Ukweli na Uwazi", kufungisha breki gari la Perestroika na Glasnost.

Huwezi kuwa mpenda maendeleo unayeelewa umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na free flow of information halafu wakati huo huo ukafurahia vitisho vya Malecela.
 
- Agenda ya jana ilikuwa amani ya chama chetu CCM na rais wa sasa kuendelea na imepita hiyo!

Respect!

FMES
 
FMES,
Mkuu hata kama asingesema ukweli ni kwamba JK ndiye mgombea wa CCM mwaka 2010.. Haya mawazo ya watu wengine nje ya ukweli huo ni kujipa moyo tu. Hao waliouliza kama Malecela atagombea mwaka 2010 hawafahamu taratibu, lakini mimi nataka kufahamu Mh. malecela kasema hayo kwa sababu anamuunga mkono JK au kasema kulingana na taratibu za chama hata kama sio chaguo lake..

- Mkuu Bob, kweli mimi nitajua alikuwa anafikiri nini mkuu? Alichosema ndicho alichosema, anamuunga mkono JK na ni chaguo lake uchaguzi mwakani what is wrong with that?

FMES!
 
Back
Top Bottom