Malengo hasa ya kuzaa watoto wengi ni nini?

Malengo hasa ya kuzaa watoto wengi ni nini?

Ni bora kuwa na watoto wengi maana kati ya hao watoto 6 ulionao hawawezi wakakutupa wote.

Lazima kuna watoto 2 au 3 kati ya hao lazima watasimama na wewe hadi mwisho.

Watakuangalia na kukujali kama mazazi.
 
Kwa maisha ya sasa sioni kama kuna tija ya kuzaa watoto wengi ni bora watoto wachache ambao utaweza kuwapatia mahitaji yao ya msingi, chakula, malazi, mavazi, furaha na elimu bora.

Mbaya zaidi unakuta mtu ana watoto wengi ambapo yeye anateseka na watoto pia wanateseka kwa kukosa mahitaji yao msingi.

Unakuta mstaafu ana watoto watu wazima na familia zao ila bado yeye anaendelea kuzaa tu.

Ushauri zaa kiasi upate muda na fedha za wewe kujinafasi na mkeo.
😁
 
Zaa kadili ya uwezo wako nikimaanisha kama unauwezo wa kuwatunza watoto 20(kuwapa mahitaji yao ipasavyo) zaa tu hamna namna..

Kwa sasa mwenye karata nyingi ndiye mwenye nafasi ya kushinda

Ukiwa na watoto wengi hutokosa wa kukustill kwa namna yoyote ile.
Na piga uwa garagaza wa kutoboa wapo..
Kuzaa watoto ili wakusitiri nao ni uzembe. Andaa mifumo ndio ije ikusitiri.
 
Ndugu elewa kwamba jamii zetu nyingi zimetokea Mashambani kwa wakulima na wafungaji hivyo ili uwe na mali hauna budi ujikite kwenye kilimo sana na ufungaji kipindi msimu wa kilimo ukifika hivyo unaitaji nguvu kazi ya kulima na kuchunga mifugo

Hapo ndio dhana ya kuzaa watoto wengi ilikuja ili wazazi wapate vijana wa kuchunga ng'ombe na kufanya kazi za mashambani kwa gharama ndogo sana

Tujiulize wewe upo mjini unazaa watoto wengi wanakupa faida ipi mjini hakuna mashamba hakuna mapori yakuchungia

Kijijini mtoto wa miaka kumi na mbili ana tija kwenye familia ila mjini ni mzigo kwenye familia maana atachunga mifugo, au kufanya kazi za mashambani kama parizi nk
Sahihi kwa kiasi kikubwa
 
Kwa maisha ya sasa sioni kama kuna tija ya kuzaa watoto wengi ni bora watoto wachache ambao utaweza kuwapatia mahitaji yao ya msingi, chakula, malazi, mavazi, furaha na elimu bora.

Mbaya zaidi unakuta mtu ana watoto wengi ambapo yeye anateseka na watoto pia wanateseka kwa kukosa mahitaji yao msingi.

Unakuta mstaafu ana watoto watu wazima na familia zao ila bado yeye anaendelea kuzaa tu.

Ushauri zaa kiasi upate muda na fedha za wewe kujinafasi na mkeo.
Ivo yaan😘
 
Wanazaa watoto wengi wanaanza kupiga vizinga vya ada za watoto

Na ndio Hawa Hawa hata bima za watoto ni mgogoro
 
Dahhhh....
Nime sikitika sana kuchelewa kushiriki kwenye huu uzi.
Ebu ngoja niwe msomaji tu sasa.
 
Wanazaa watoto wengi wanaanza kupiga vizinga vya ada za watoto

Na ndio Hawa Hawa hata bima za watoto ni mgogoro
Kipimo cha watoto wengi ni kuanzia wangapi mkuu??
Lakini pia minaona bora mtu asizae ikiwa kama hawezi kuhudumia wanawe.
 
Dini Dini Dini....

'mtoto ni baraka' 'kila mtoto anakuja na sahani yake' 'zaeni mkaijaze dunia' ni sawa tu, ila watu hawazingatii uchumi kama unatosheleza

angalia nchi zilizoendelea ambazo hazina sana dini, watu wanazaa kwa mpangilio, tena kuna wengine wako serious kabisa kuliko wazae wanaamua kufuga kambwa kamoja
Maisha yamebadilika hakuna mtoto utakae mzaa bila kumuandaa kwa kumsomesha na kumpa mahitaji ya muhimu na kuja kumpa Chanel ya baada ya kusoma hayo yoye yanaitaji pesa Haina umuhimu unazaa watoto wengi unakuja kuwatesha kwa kushindwa kuwahudumia

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Bwashee, kila mtu si anaishi anavyojua au? Mie nina watoto 3 tu, ingawa sielewi kwa nini mtu anakuwa na watoto wengi, siwezi wahukumu maana ni maisha yao.
Wengi wanaozaaa watoto wengi wana maisha ya kuunga unga. Sijawahi one matajiri au watu wa kipato cha kati wanazaa watoto wengi.
Kuzaa watoto wengi sio ganatiii kuwa watakusaidia baadae. Zaa watoto unaoweza kuwatunza na kuwapatia mahitaji yote muhimu. Kuna watu maisha yao yote wanalea watoto sababu ya kuwa na watoto wangi. Anashindwa hata kujiwekea akiba. Unakuta una watoto saba hadi 10 lakini ukilazwa hospital hawawezi changia hata laki 2 za matibabu.
 
Ninafanya kazi ofc kubwa sana hapa nchini, na wote wenye akili mingi ndani yake wanao leta matokeo makubwa ni walio soma Kayumba, na wenye mbwembwe na wanaiba kila siku na kufukuzwa ni hao unao watengeneza na wewe nyumbani kwako ambao huku ofisini hawana uwezo wowote wa kazi zaidi ya kunyoosha ki English kwenye hamna, kaa kwenye ujinga, watoto wakuozee ndani na nje
Viongozi wetu karibia wote wamesoma kayumba, lakini wengi ni wezi na wabadhilifu wa mali za umma.
 
Ni bora kuwa na watoto wengi maana kati ya hao watoto 6 ulionao hawawezi wakakutupa wote.

Lazima kuna watoto 2 au 3 kati ya hao lazima watasimama na wewe hadi mwisho.

Watakuangalia na kukujali kama mazazi.
Sio wote wana hiyo bahati. Wengine wana watoto hata 7 lakini wametelekezwa na wtoto wao.
 
Sio wote wana hiyo bahati. Wengine wana watoto hata 7 lakini wametelekezwa na wtoto wao.
Asilimia ya bahati ya maisha ni ndogo Sana maisha yamebadilika Sana hao watoto utakao zaa 6 mpaka 7 unawaandaje na maisha yao? Kama ni elimu inaitaji pesa na hata ukimsomesha akimaliza bado swala la kupata kazi ni shida na ukitaka apate kazi ya maana lazima utumie pesa ya kumpa hio kazi hio bahati inatoka WAP? Kila siku watu wanamaliza chuo wanaingia mitaani wengine wanajifunza utapeli kupitia elimu yao na wengine wanaingia kwenye ulevi kutokana na stress za kusoma na hamna kazi hakuna bahati inayokuja kwa maisha ya Sasa bila ya kuiandaa

Nilikuwa namjibu huyo anayesema ukizaa utapata wa kukutunza uzeeni
 
Back
Top Bottom