Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
MALENGO MAKUU YA VITA NI KUISHI NA KUSHINDA; SIO KUJITOA MHANGA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Unapoingia kwenye vita yoyote jambo la kwanza unapaswa kuangalia uwezekano wa kuishi upo. Kuyalinda maisha yako. Hilo ndilo jambo la kwanza.
2. Jambo la pili, kama uwezekano ni mdogo je kuna exist door, mpango wa kuepa, kutoroka ukabaki salama. Hilo ni jambo la pili
3. Jambo la tatu, umeshajua hiyo vita kuishi au ku-escape uwezekano upo. Je ushindi upo? Je unamuweza adui yako kumuangamiza?
4. Kama jibu ni ndio, je ni zipi njia atakazotumia adui yako ku- escape na kutoroka ukikaribia kumshinda.
5. Zingatia adui aliyetoroka hujamshinda. Kwa sababu kutoroka ni sehemu ya mbinu ya ushindi. Ndio maana hata wewe lazima ujue ukizidiwa utafanya nini ili u- escape.
6. Kwenye vita ukishafikiria kujitoa mhanga ujue hiyo vita umepigwa.
7. Kujitoa mhanga ni ushindi nusu ikiwa utakufa na adui yako. Sio ufe mwenyewe au uue wasiohusika.
Mfano; unauadui na mimi Mtibeli. Tupo kwenye mapigano. Sasa wewe badala ya kuja kujitoa mhanga ufe na mimi, wewe unaenda kujitoa mhanga unakufa na walinzi wangu au rafiki zangu. Nope!
8. Maisha yako yana thamani kubwa kuliko kitu chochote. Lazima uyalinde.
9. Unapokuwa kwenye vita vya kisiasa jitahidi sana ufanye hesabu zako vizuri sana. Option ya kujitoa mhanga isiwepo kwenye Ramani na war plan yako.
10. Vita vya kisiasa ni kama kinyonga. Vinabadilika badilika. Leo rafiki yako kesho adui yako. Leo adui yako kesho rafiki yako.
Inategemea kwa muda huo maslahi yenu yakoje
Kumbuka maslahi ya watu au mtu hubadilika badilika kulingana na hali, umri, wakati, uelewa na mazingira.
11. Kwenye vita vya kisiasa hakunaga mtu wa kumlaumu isipokuwa wewe mwenyewe.
12. Usiingie kwenye vita kama huna War plan ya kueleweka itakayoonyesha ushindi wako na jinsi ya kutoroka ikitokea vita vimeenda kinyume
13. Vita haindeshwi na mihemko. Vita inaendeshwa na Malengo, mipango, mikakati, na rasilimali
14. Kupigania Haki hakuondoi kutokuwa na malengo (ambayo ni kupata haki), mipango, mikakati na rasilimali.
Sio kwamba kwa vile jambo ni haki yako basi ndio upigane kichwa kichwa. Hata wanyama wasio na utashi hawafanyi hivyo.
15. Uvumilivu na subira ya muda sahihi(timing) sio Uwoga. Ni moja ya mbinu ya kushinda vita.
16. Kama utajitoa mhanga ni lazima uwe na hakika kuwa vita hiyo mmeshashinda. Na sio ujitoe mhanga vita ikiwa bado mbichi.
17. Unajitoa Mhanga ili kumaliza vita na. Kupata ushindi kwa timu yako. Sio unajitoaa mhanga alafu vita bado inaendelea. Ni hasara kwako na timu yako.
Ni sawa kwenye mpira mchezaji ujitoe mhanga upigwe redcard dakika za kwanza kipindi cha kwanza. Unaigharimu timu yako.
18. Luis Suarez yeye alitumia mbinu ya kujitoa mhanga kudaka mpira kimakusudi kabisa dakika za majeruhi kuzuia goli walilokuwa wanafungwa.
Na timu yake ilishinda na yeye licha ya kupigwa kadi nyekundu na kupewa adhabu lakini kwa timu yake yeye ndiye man of the match.
19. Vita inahitaji godfather na mastermind mbobevu. Usikubali kwenda kichwa kichwa ikiwa nyuma yako hakuna Godfather au Masternind mwenye kueleweka.
20. Kama umetumwa na Mungu lazima akupe ishara ujihakikishie aliyekutuma ni Mungu. Tena mwenye nguvu.
Lazima umuulize huyo Mungu na akupe ishara.
Mfano Nabii Musa hakutaka kwenda kuwatoa Ndugu zake waisraeli kwa mafarao bila kuhakikishiwa na kuthibitisha anayemtuma. Ndio Mungu anampa ishara za miujiza.
Musa alipewa ishara Mbili za ajabu.
21. Musa ni mjeshi na jasusi kitaaluma. So anajua aina ya vita aliyotumwa inahitaji awe na Godfather na Mastermind wa kueleweka. Hivyo Mungu ambaye hapa ni Yahweh ndiye aliyekuwa nyuma ya Muda.
Mfano mwingine ni kwa Daudi mtoto wa Yese ambaye baadaye alikuja kuwa Mfalme mashuhuri duniani.
22. Daudi hakujituma kuwa mfalme. Wala hakuwa na hiyo mipango katika maisha yake. Alikuwa ni mchungaji wa mifugo ya baba yake, lakini pia alikuwa mwanamuziki wa kuimba na kutunga nyimbo.
23. Nabii Samwel alitumwa na Mungu aende kwa Daudi akampake mafuta awe mfalme.
Baada ya kupakwa mafuta ndipo hekaheka zikaanza zikiratibiwa na Godfather na mastermind ambaye ni Mungu Yahweh.
Hata kumpiga Goliathi ni tukio lililoratibiwa na Mungu ili kumpa Daudi political Promotion. Hata kushinda kwake kwa Goliathi ilikuwa mission impossible lakini Godfather ndiye alikuwa chiefmaker
24. Ni kweli sio lazima utumwe na Mungu ndio ushinde. Kweli kabisa. Ila lazima uwe na mipango, mikakati, na rasilimali. Hapo kwenye Rasilimali lazima awepo Godfather au mastermind wa kueleweka. Kwa sababu unapoingia vita sio muda wote akili yako itakuwa kwenye ufanisi. Kuna wakati utachoka, utakuwa hauko motivated, utahitaji backup n.k.
24. Unataka kusema nini Robert?
25. Usijitume! Kwenye vita usijipeleke kama hujatumwa na wewe unajua sio Godfather au Mastermind.
Yakikukuta hata umwombe Mungu hatakuwa na msaada wowote. Vita vinaendeshwa kwa Oda. Chain of command.
Ukivunja Protokali ni ngumu kupata msaada.
26. Watu wengi wanauliza, kwa nini Mungu haingilii kati pale wenye haki wanapoonewa wakiingia vitani. Jibu ni moja. Mungu ni Mungu wa majeshi.
Kama hakukutuma aiseeh utahitaji Rehema zake tuu na sio haki yake kukuokoa.
Ila kama amekutuma huhitaji Rehema zake bali ni haki yake kukuokoa. Na ukitumwa na Mungu lazima utoboe.
27. Unapambana na haki lakini wewe unakandamiza haki za wengine waliochini yako. Mkeo, watoto, wafanyakazi wako, au wateja wako unawaibia au huwapi huduma zinazowastahili. Hivi unafikiri ukidai haki kwa Mungu yeye atakupa?
28. Najaribu kukuambia kuishi na kushinda ni lengo namba moja la vita yako. Lazima ufanye calculations zako vizuri sana. Ikiwezekana tafuta wataalamu wakusaidie.
26. Je Robert kwa hiyo watu wasipiganie Haki zao? Unatuambia nini Taikonmaster, toka hapa uatufundisha woga!
27. Siwafundishi Woga. Nawafundisha kuwa na Akili. Zingatia sisi watibeli ni Haki, ukweli, Upendo na Akili.
Mimi kukuambia hayo sio kwamba nataka uache kupigania haki bali nakuambia pigana kwa Akili ukijua vita ni kuishi na kushinda sio Kufa au kushindwa.
Kama unaona uwezekano wa kufa au kushindwa Abort hiyo vita. Weka makubaliano na adui yako kwa muda. Ndivyo watibeli tunavyofanya.
Mungu awabariki sana.
Linda maisha yako. Linda maisha ya watu wako. Taifa lako.
Acha nipumzike sasa.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam