Malengo yako ya mwaka huu yametimia?

Malengo yako ya mwaka huu yametimia?

Kuna jambo nilipanga mwaka huu...hadi saa ivi halijatimia na hakuna dalili ya kutimia..kisaikolojia tayari nimejiandaa kulikosa maisha yangu yote...maana nimelipigania muda mno..ni hayo tu

Mengine..uzima thanks to the almighty..mapambano yanaendelea
Mkuu mbona umejikatia tamaa ? Kwamba huwez kufanikisha Tena ? Mapambano mkuu ongeza
 
Niliomba Mungu Mimi na familia yangu tuwe na afya njema Hadi naandika tumefanikiwa sijui Sasa hizo siku kadhaa zilizobaki. In Shaa Allah naamini tutavuka salama.

Mengine majaaliwa.
Inshallah na ikawe
 
Cha maana kilicho timia mwaka huu ni kumaliza Elimu yangu ya chuo. Saiv ndo tunaandaa ramani kwa ajili ya 2023, 2024, 2025.

Hakika mungu aendelee kua pamoja nami

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
Karibu mtaani mkuu ! Pachungu Sana usipojipanga,,,, Kaz zenyewe Ni connection Kama hujulikani Ni noma !
 
Amen ms Liverpool,,,,! tuendelee kuamini na kupambana huku tukimtanguliza Mungu mbele
Mungu ni mwaminifu.

Kiuchumi nimerudi nyuma sana ila kiroho nimesogea.
Na namshukuru Mungu amenipa furaha na amani,
Amenipa afya njema.

Naamini mwaka ujao atanisogeza mbele kiuchumi na atazidisha furaha zaidi kwangu na Kwa mwenzangu.
 
Well ni December, tunaumalizia mwaka! Kila mmoja kwa namna yake kuna malengo alijiwekea, yametimia? Kama ndiyo kwa asilimia ngapi? Na kama bado kwa nini? Wapi ulifeli?

Binafsi niseme malengo hayakutimia kwa 95%, kuna biashara ipo somewhere, vijana wanaharibu mwanzo mwisho. Kwa huu mwaka nimeshawabadilisha kama mara 3, nakosa usimamizi mzuri kutokana na majukumu yangu mengine.

kuna bajaji nilinunua (mkononi) bei poa 3.8m, ilikuwa kwenye mazingira mazuri nikampa kijana. Ni headache, kila siku visingizio mara service, kwa wiki hela naweza kupewa mara 4 au tatu, nikamnyang'anya nikampa ndugu yangu akomae.

Huyu ndiyo kirusi kabisa, hela haleti mara service, mara sijui kanunua nini na hivi sina uzoefu na spare na service, kwa ujumla ananipiga haswa! Nimepanga kuiuza na nishamwambia dalali, najua ndugu hawatanielewa lakini hakuna namna.

Kuna ka-plot kako sehemu, nilipanga kujenga lakini nimeishia kuweka tofali tu.

Kuna mtu nilimuazima kiasi kadhaa aiendeleze biashara yake, mambo siyo mambo, niseme ana majanga kuliko mimi, tena hata kumdai nashindwa, naona akinikatia plot kama sehemu ya makubaliano endapo atakwama kunilipa.

Kuna majanga yalitokea kazini, dah, namshukuru Mungu mambo yakaenda powa, ingenigharimu sana.

Kwa kifupi huu mwaka haujawa mzuri kwangu kimalengo, kiuchumi naona niko pale pale nilipokuwa, malengo niliyojiwekea vitu vingi sijatimiza.

Vipi malengo yako yametimia? Kichumi na nyanja nyinginezo? Naamini kuteleza siyo kuanguka, bado tunayo nafasi ya kupambana na kusahihisha tulipokosea.
Mkuu kila mtu huwa Ana utaratibu wake na mwisho wa mwaka wake. Mfano wengine labda April ndio December kwao. Sio wote wanaofuata utaratibu waliokuta. Mfano vyuo vikuu sahivi ndio Kama January pia serikali bajeti inasomwa ama inapangwa July ndio mwisho wa mwaka kwao.
So hii ishu iko subjective personally sio objective.
Wapo wengine wanavaa labda vizuri na kula pilau miezi fulani sio lazima let say Christmas.

Yaani wapo wasioendana na mapokeo ya dunia.
Dunia iko pale pale inalizunguka jua haijawahi simama ivyo inategemea umeingilia wapi kwenye huo mzunguko.yupo aliyeajiriwa November or agosti ndio ataseti hapo bm aka benchmark yake ama reference point,Kama Ile surveyors wanavyoseti height ya vitu like milima from mean sea level.

Wapo wanaokumbia jumamosi ndio siku ya Saba wengine jumanne Mana ndipo alipoingilia kuhesabu.


S
Usipende na upepo Bali kuwa na your own direction.


Kama hii najua utanishambulia Mana beliefs zeetu, assumptions, subjectivity, opinions zimedifa. Ni nature ya ubongo unapoonyesha utofauti wa inachokiamini na inachukua muda mpaka ikitoe icho iingize kingine kipya Mana beliefs Ni energy.
 
Mwaka huu nilikuwa na malengo makuu mawili
1. Kujenga msingi wa nyumba ndogo , boma na kupaua kwenye plot yangu.
2. Kujusanya na ku save pesa Hadi kufikia 7M mwisho wa mwaka huu ili mwakani mwishoni nipate ka lusafiri kangu.

Lakini Hadi kufikia desemba hii malengo yangu hayajafanikiwa kama nikivyojipangia
1. Kwenye plot yangu nimejenga msingi tu.
2. Kwenye makusanyo mpaka sasa Nina 5.5M out of 7M targeted na nikiangilia uwezekano wa kupata hiyo 1.5M desemba hii ili kufikia malengo haupo.

Wanasema mipango si matumizi.
 
Back
Top Bottom