Malengo yako ya mwaka huu yametimia?

Malengo yako ya mwaka huu yametimia?

Nina mategemeo ya kupata mazuri mwaka ujao Mungu akinipa uhai na afya.

Mwaka huu ulienda ndivyo sivyo kwakuwa mwaka jana mwishoni kuna mradi niliingia kichwa kichwa ukavuruga malengo ya mwaka huu wote.

Mwaka huu nimeishi kwa Neema ya Mungu tu.
Shukuru Mungu kwa zawadi ya uhai,,, mapambano yanaendelea
 
Well ni December, tunaumalizia mwaka! Kila mmoja kwa namna yake kuna malengo alijiwekea, yametimia? Kama ndiyo kwa asilimia ngapi? Na kama bado kwa nini? Wapi ulifeli?

Binafsi niseme malengo hayakutimia kwa 95%, kuna biashara ipo somewhere, vijana wanaharibu mwanzo mwisho. Kwa huu mwaka nimeshawabadilisha kama mara 3, nakosa usimamizi mzuri kutokana na majukumu yangu mengine.

kuna bajaji nilinunua (mkononi) bei poa 3.8m, ilikuwa kwenye mazingira mazuri nikampa kijana. Ni headache, kila siku visingizio mara service, kwa wiki hela naweza kupewa mara 4 au tatu, nikamnyang'anya nikampa ndugu yangu akomae.

Huyu ndiyo kirusi kabisa, hela haleti mara service, mara sijui kanunua nini na hivi sina uzoefu na spare na service, kwa ujumla ananipiga haswa! Nimepanga kuiuza na nishamwambia dalali, najua ndugu hawatanielewa lakini hakuna namna.

Kuna ka-plot kako sehemu, nilipanga kujenga lakini nimeishia kuweka tofali tu.

Kuna mtu nilimuazima kiasi kadhaa aiendeleze biashara yake, mambo siyo mambo, niseme ana majanga kuliko mimi, tena hata kumdai nashindwa, naona akinikatia plot kama sehemu ya makubaliano endapo atakwama kunilipa.

Kuna majanga yalitokea kazini, dah, namshukuru Mungu mambo yakaenda powa, ingenigharimu sana.

Kwa kifupi huu mwaka haujawa mzuri kwangu kimalengo, kiuchumi naona niko pale pale nilipokuwa, malengo niliyojiwekea vitu vingi sijatimiza.

Vipi malengo yako yametimia? Kichumi na nyanja nyinginezo? Naamini kuteleza siyo kuanguka, bado tunayo nafasi ya kupambana na kusahihisha tulipokosea.
Yatimie yasitime wote tutakufa tu
 
Malengo yangu hayajatimiaa....nataka kshinda milioni 3,smart tv "55",smartphone na redio ya bluetooth....bado sijafanikiwa naendelea kucheza.. mchongo pesa.
 
Back
Top Bottom