Malengo yako ya mwaka huu yametimia?

Malengo yako ya mwaka huu yametimia?

Well ni December, tunaumalizia mwaka! Kila mmoja kwa namna yake kuna malengo alijiwekea, yametimia? Kama ndiyo kwa asilimia ngapi? Na kama bado kwa nini? Wapi ulifeli?

Binafsi niseme malengo hayakutimia kwa 95%, kuna biashara ipo somewhere, vijana wanaharibu mwanzo mwisho. Kwa huu mwaka nimeshawabadilisha kama mara 3, nakosa usimamizi mzuri kutokana na majukumu yangu mengine.

kuna bajaji nilinunua (mkononi) bei poa 3.8m, ilikuwa kwenye mazingira mazuri nikampa kijana. Ni headache, kila siku visingizio mara service, kwa wiki hela naweza kupewa mara 4 au tatu, nikamnyang'anya nikampa ndugu yangu akomae.

Huyu ndiyo kirusi kabisa, hela haleti mara service, mara sijui kanunua nini na hivi sina uzoefu na spare na service, kwa ujumla ananipiga haswa! Nimepanga kuiuza na nishamwambia dalali, najua ndugu hawatanielewa lakini hakuna namna.

Kuna ka-plot kako sehemu, nilipanga kujenga lakini nimeishia kuweka tofali tu.

Kuna mtu nilimuazima kiasi kadhaa aiendeleze biashara yake, mambo siyo mambo, niseme ana majanga kuliko mimi, tena hata kumdai nashindwa, naona akinikatia plot kama sehemu ya makubaliano endapo atakwama kunilipa.

Kuna majanga yalitokea kazini, dah, namshukuru Mungu mambo yakaenda powa, ingenigharimu sana.

Kwa kifupi huu mwaka haujawa mzuri kwangu kimalengo, kiuchumi naona niko pale pale nilipokuwa, malengo niliyojiwekea vitu vingi sijatimiza.

Vipi malengo yako yametimia? Kichumi na nyanja nyinginezo? Naamini kuteleza siyo kuanguka, bado tunayo nafasi ya kupambana na kusahihisha tulipokosea.
Mim nusu nusu.lakin sina sababu yakulalamika namshukuru mungu hata kwa hii nusu malengo
 
Namshuku Mungu Muumba kwa huu mwaka kanijalia afya njema mimi pamoja na familia yangu yote.kuhusu malengo hayajatimia kutokana na changamoto mbali mbali,naamini kwa kwa uzima alionipa Mungu mwakani nitatoboa.AMINA
 
Bado mwez hujaisha huu,nilipanga lazima nibebe mimba mwaka huu[emoji38]...huenda nikabahatika kunasa mwez huu...isipotimia bas itangoja mwakan..japo mwakan nilitaka nipakate
Bwana wa majeshi, akutangulie lengo /tamanio lako litimie
 
Namshuku Mungu Muumba kwa huu mwaka kanijalia afya njema mimi pamoja na familia yangu yote.kuhusu malengo hayajatimia kutokana na changamoto mbali mbali,naamini kwa kwa uzima alionipa Mungu mwakani nitatoboa.AMINA
Amina,,,,,
 
Back
Top Bottom