uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,657
- 2,406
Binafsi ya kwangu hayakutimia kwa asilimia kadhaa, nilikuwa na mradi wa doda bodoWell ni December, tunaumalizia mwaka! Kila mmoja kwa namna yake kuna malengo alijiwekea, yametimia? Kama ndiyo kwa asilimia ngapi? Na kama bado kwa nini? Wapi ulifeli?
Binafsi niseme malengo hayakutimia kwa 95%, kuna biashara ipo somewhere, vijana wanaharibu mwanzo mwisho. Kwa huu mwaka nimeshawabadilisha kama mara 3, nakosa usimamizi mzuri kutokana na majukumu yangu mengine.
kuna bajaji nilinunua (mkononi) bei poa 3.8m, ilikuwa kwenye mazingira mazuri nikampa kijana. Ni headache, kila siku visingizio mara service, kwa wiki hela naweza kupewa mara 4 au tatu, nikamnyang'anya nikampa ndugu yangu akomae.
Huyu ndiyo kirusi kabisa, hela haleti mara service, mara sijui kanunua nini na hivi sina uzoefu na spare na service, kwa ujumla ananipiga haswa! Nimepanga kuiuza na nishamwambia dalali, najua ndugu hawatanielewa lakini hakuna namna.
Kuna ka-plot kako sehemu, nilipanga kujenga lakini nimeishia kuweka tofali tu.
Kuna mtu nilimuazima kiasi kadhaa aiendeleze biashara yake, mambo siyo mambo, niseme ana majanga kuliko mimi, tena hata kumdai nashindwa, naona akinikatia plot kama sehemu ya makubaliano endapo atakwama kunilipa.
Kuna majanga yalitokea kazini, dah, namshukuru Mungu mambo yakaenda powa, ingenigharimu sana.
Kwa kifupi huu mwaka haujawa mzuri kwangu kimalengo, kiuchumi naona niko pale pale nilipokuwa, malengo niliyojiwekea vitu vingi sijatimiza.
Vipi malengo yako yametimia? Kichumi na nyanja nyinginezo? Naamini kuteleza siyo kuanguka, bado tunayo nafasi ya kupambana na kusahihisha tulipokosea.
ambapo nilikuwa na kijana kusema ukweli alikuwa mwaminifu kwa kuleta rejesho.
Nikajishauri mwenyewe kwamba mwaka huu nibadilishe hiyo biashara ninunue ngómbe wa maziwa badala
ya piki piki sababu ni kwamba nilipopiga mahesabu niliona.mwisho wa mkataba pikipiki inaondoka.
lakini kwa wafugaji,unauza maziwa unarudisha fedha yako na bado unabaki na mifugo na faida nyingine kama vile mbolea shambani.
Basi bwana nikanunua mmoja mtamba nikampandisha na kuendelea kumuudumia.
mimba ikiwa na miezi mitatu,akafa ghafla na hivyo pesa yote ikapotea.
hivyo lengo langu halikutimia,sijui kama nilikosea kuchanga karata.
Nami naamini kama wewe kuteleza siyo kuanguka.