Malengo yako ya mwaka huu yametimia?

Malengo yako ya mwaka huu yametimia?

Ngoja nifurahishe nafsi yako ...ghorofa tayari mkuu[emoji23][emoji23]

Nimehamia
Sasa unahamia vipi kimya kimya kabla hatujanywa kisusio na kutengeneza kichuri kidogo mkuu wangu? Hivi ndio vitu vya kualikana ujuwe!
 
Ni rahisi tu mkuu ni marufuku kuongea ukweli kwa wanawake,au naongopa ndugu zangu ?[emoji28]
Bila uongo mwingi na hela huwezi kuwawin hawa viumbe wakike...nmekupata vyema mwakani muda kama huu nitaleta mrejesho..kikubwa uhai.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tarehe 31 Dec 2021. Nilijiwekea malengo ya kutimiza 2022. Wakati huo Sina hata mia , YAANI nimefulia Sana.
Ikumbukwe kuwa Sina Ajira.

KWA IMANI KABISA NILIMUOMBA MUNGU ANIWEZESHE KUTIMIZA YA FUATAYO.

1. Kupaua frem zangu Tatu za biashara.

Hlo lilikuwa lengo langu kuu lkn sikujua nitapata wapi pesa. Lakini pia nikamuomba Mungu kwamba Kama ukipenda niwezeshe niweke geti hata frem moja.....nikamwambia Tena Mungu ukipenda zaidi nifanye hata finishing ya kuanzia.

MUNGU NI MWEMA SANA. Nimepaua zote , nimeweka mageti zote, nimefanya finishing zote na chazaidi nimefungua na kabiashara kadogo kwenye hizo frem.

SIKO ZOTE MUNGU NI MWEMA SANA
 
Katika mwaka uliokuwa mbaya kwangu i can say 2022 is the most. Sijatimiza lengo hata moja na ndio kwanza nimerudi hatua kadhaa nyuma. Najipanga kwa ajili ya mwaka ujao najua Mungu atafungua njia tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Heri Yako umerudi nyumba kwa mwaka mmoja. Mm 2022 nimeinuka kidogo baada ya kurudi nyuma kwa miaka 7 mfululizo. YAANI tangu 2014 - Dec 2021
 
Kuna demu nilitaka kumbamiza du.du mwaka huu nimemkosa mwisho nikadondokea Kwa shogger nikalifumua
 
Well ni December, tunaumalizia mwaka! Kila mmoja kwa namna yake kuna malengo alijiwekea, yametimia? Kama ndiyo kwa asilimia ngapi? Na kama bado kwa nini? Wapi ulifeli?

Binafsi niseme malengo hayakutimia kwa 95%, kuna biashara ipo somewhere, vijana wanaharibu mwanzo mwisho. Kwa huu mwaka nimeshawabadilisha kama mara 3, nakosa usimamizi mzuri kutokana na majukumu yangu mengine.

kuna bajaji nilinunua (mkononi) bei poa 3.8m, ilikuwa kwenye mazingira mazuri nikampa kijana. Ni headache, kila siku visingizio mara service, kwa wiki hela naweza kupewa mara 4 au tatu, nikamnyang'anya nikampa ndugu yangu akomae.

Huyu ndiyo kirusi kabisa, hela haleti mara service, mara sijui kanunua nini na hivi sina uzoefu na spare na service, kwa ujumla ananipiga haswa! Nimepanga kuiuza na nishamwambia dalali, najua ndugu hawatanielewa lakini hakuna namna.

Kuna ka-plot kako sehemu, nilipanga kujenga lakini nimeishia kuweka tofali tu.

Kuna mtu nilimuazima kiasi kadhaa aiendeleze biashara yake, mambo siyo mambo, niseme ana majanga kuliko mimi, tena hata kumdai nashindwa, naona akinikatia plot kama sehemu ya makubaliano endapo atakwama kunilipa.

Kuna majanga yalitokea kazini, dah, namshukuru Mungu mambo yakaenda powa, ingenigharimu sana.

Kwa kifupi huu mwaka haujawa mzuri kwangu kimalengo, kiuchumi naona niko pale pale nilipokuwa, malengo niliyojiwekea vitu vingi sijatimiza.

Vipi malengo yako yametimia? Kichumi na nyanja nyinginezo? Naamini kuteleza siyo kuanguka, bado tunayo nafasi ya kupambana na kusahihisha tulipokosea.
Mimi malengo yangu asilimia 90% yametimia nilijiwekea huu mwaka niwakujua kwanini nipo hivi mpaka Sasa nimejua kabisa kuwa duniani Mungu ndie anayejua .


Walahiii
 
Back
Top Bottom