kitalembwa
JF-Expert Member
- Jul 12, 2014
- 3,607
- 9,430
- Thread starter
-
- #21
Kuishi kwa malengo Ni Namna Bora ya kujipangilia, pia inasaidia kile unachokipata (income) kuelekezwa kule ambako umekusudia !Mimi huwa siishii kwa malengo naishi kulingana na maisha yalivyo. Kwangu malengo ni illusion
Next year tujipange mkuu,,,, kikubwa uzimaNamshukuru Mungu kwa kunilinda hadi leo, malengo yangu kwa Mwaka huu hayajatimia kama ambavyo nilipanga.
Mkuu mbona umejikatia tamaa ? Kwamba huwez kufanikisha Tena ? Mapambano mkuu ongezaKuna jambo nilipanga mwaka huu...hadi saa ivi halijatimia na hakuna dalili ya kutimia..kisaikolojia tayari nimejiandaa kulikosa maisha yangu yote...maana nimelipigania muda mno..ni hayo tu
Mengine..uzima thanks to the almighty..mapambano yanaendelea
C, nataka niifanyie service kidogo walau nipate hela ya maana!Mkuu hiyo bajaji ni namba D,C or B unaiiuza kwa ngapi?
[emoji1][emoji1]amini kwambaBado tuna siku 30 nisiseme yametimia maana naweza nikaokota embe dodo kwenye lami Mara pa nimekuwa Waziri wa Fedha-malengo yote yakatimia.
Mzee wa mitulingaIla hadi Leo hii tofauti na kupumua sina lengo nililokamilisha.
Kwa kweli tusiishi kwa ndoto alisema Prof.Jay
Inshallah na ikaweNiliomba Mungu Mimi na familia yangu tuwe na afya njema Hadi naandika tumefanikiwa sijui Sasa hizo siku kadhaa zilizobaki. In Shaa Allah naamini tutavuka salama.
Mengine majaaliwa.
Karibu mtaani mkuu ! Pachungu Sana usipojipanga,,,, Kaz zenyewe Ni connection Kama hujulikani Ni noma !Cha maana kilicho timia mwaka huu ni kumaliza Elimu yangu ya chuo. Saiv ndo tunaandaa ramani kwa ajili ya 2023, 2024, 2025.
Hakika mungu aendelee kua pamoja nami
Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
Dalili sio nzuri, Dashboard warning lights zimebadilika na kuwa red ninahisi kabisa kama si mwaka huu basi 2023 lazima kitu kivute.Sanda ? Ya nini mkuu !
Mapambano yaendeleeeKatika mwaka uliokuwa mbaya kwangu i can say 2022 is the most. Sijatimiza lengo hata moja na ndio kwanza nimerudi hatua kadhaa nyuma. Najipanga kwa ajili ya mwaka ujao najua Mungu atafungua njia tuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Amen ms Liverpool,,,,! tuendelee kuamini na kupambana huku tukimtanguliza Mungu mbeleBado hayajatimia
Ila kuna yale ambayo Mungu amenipa ,namshukuru.
Anaendelea kutenda.
Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Mungu ni mwaminifu.Amen ms Liverpool,,,,! tuendelee kuamini na kupambana huku tukimtanguliza Mungu mbele
[emoji120][emoji120] maisha ni lazima yaendelee,[emoji123][emoji123]Mkuu mbona umejikatia tamaa ? Kwamba huwez kufanikisha Tena ? Mapambano mkuu ongeza
Mkuu kila mtu huwa Ana utaratibu wake na mwisho wa mwaka wake. Mfano wengine labda April ndio December kwao. Sio wote wanaofuata utaratibu waliokuta. Mfano vyuo vikuu sahivi ndio Kama January pia serikali bajeti inasomwa ama inapangwa July ndio mwisho wa mwaka kwao.Well ni December, tunaumalizia mwaka! Kila mmoja kwa namna yake kuna malengo alijiwekea, yametimia? Kama ndiyo kwa asilimia ngapi? Na kama bado kwa nini? Wapi ulifeli?
Binafsi niseme malengo hayakutimia kwa 95%, kuna biashara ipo somewhere, vijana wanaharibu mwanzo mwisho. Kwa huu mwaka nimeshawabadilisha kama mara 3, nakosa usimamizi mzuri kutokana na majukumu yangu mengine.
kuna bajaji nilinunua (mkononi) bei poa 3.8m, ilikuwa kwenye mazingira mazuri nikampa kijana. Ni headache, kila siku visingizio mara service, kwa wiki hela naweza kupewa mara 4 au tatu, nikamnyang'anya nikampa ndugu yangu akomae.
Huyu ndiyo kirusi kabisa, hela haleti mara service, mara sijui kanunua nini na hivi sina uzoefu na spare na service, kwa ujumla ananipiga haswa! Nimepanga kuiuza na nishamwambia dalali, najua ndugu hawatanielewa lakini hakuna namna.
Kuna ka-plot kako sehemu, nilipanga kujenga lakini nimeishia kuweka tofali tu.
Kuna mtu nilimuazima kiasi kadhaa aiendeleze biashara yake, mambo siyo mambo, niseme ana majanga kuliko mimi, tena hata kumdai nashindwa, naona akinikatia plot kama sehemu ya makubaliano endapo atakwama kunilipa.
Kuna majanga yalitokea kazini, dah, namshukuru Mungu mambo yakaenda powa, ingenigharimu sana.
Kwa kifupi huu mwaka haujawa mzuri kwangu kimalengo, kiuchumi naona niko pale pale nilipokuwa, malengo niliyojiwekea vitu vingi sijatimiza.
Vipi malengo yako yametimia? Kichumi na nyanja nyinginezo? Naamini kuteleza siyo kuanguka, bado tunayo nafasi ya kupambana na kusahihisha tulipokosea.
π π π Chanjo gani uliyoigomea? Au ya Covid-19?Mwaka uhu kikubwa nilichofanya ni kugoma kuchanjwa....