Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa

Mkuu kama kwako wanawake wana nafasi kubwa sana katika maisha yako haimaanishi kila mwanaume ana wachukulia wanawake hivyo.

Soma sifa mbalimbali za makundi mbalimbali ya watu.
Hapana hawana nafasi kubwa kwangu bali wana nafasi yao kwangu hasa nikizingatia maandiko ya imani yangu ya kidini
 
Mkuu Mimi naona Maisha ya Mtu kukaa single bila Attachment na Mwanamke ni mazuri Sana

Kula vizuri
Lala vizuri
Sali Sana
Kataa ndoa
Tafuta pesa kwa ajili yako na wazazi na wasiojiweza huu mradi wa Ndoa unawafaidisha wanawake tu.
Mmoja wapo wa wazazi wako angefanya kama ulivyosema usingeandika haya
 
Kwanini niende umbali wote huu kisa tuu ndoa wakati naweza tuu nikapata mtoto na nikamlea vizuri bila hata hayo maisha ya ndoa.
Ingekuwa rahisi hivi, pata mtoto lea mwenyewe. Ila jua wapo wanaoteswa na hao watoto hasa wanapotaka kujua mzazi wake mwingine yupo wapi....utaficha wee ila utaumizwa na mtoto huyohuyo na jamii itaumizwa na mtoto huyohuyo tutasema hana maadili kwasababu alilelewa na mzazi mmoja.
 
Ndoa zinahitaji ushauri wa kisaikolojia zaidi kuliko wakati wote.
 
Asipokuwa na tamaa kwako huwezi kumtawala
 
Usipooa utaolewa.
Changamoto ni kwamba huwa hamna hoja za kutetea kuoa zaidi ya "negativity words" mmekosa hoja za kutetea ndoa imeishia kutukana.

Sasa sijajua kati ya watoa matusi na wapokea matusi nani ana upungufu wa akili.

Anyway, toeni tusi lolotee hata liwe jipya kiasi gani ila HATUOI.

#YNWA
 
Wapi nimekutukana rafiki?
 
Masingle madha wa kujitakia (sio hawa waliofiwa na waume zao) ni moja ya sababu kubwa na vijana wa hovyo kwenye taifa la tanzania na dunia kwa ujumla wake ambao ndio hawa kutwa kucha wanaimba mashairi na ngonjera za kukataa na kuponda mahusiano matakatifu ya ndoa.

If I were a president kijana yoyote anayeingia kwenye mahusiano pasipo kuonesha muelekeo wa kuoa au kuolewa cha moto angekiona.
 
Haya ni maneno alitakiwa ayaandike mdada aisee mwanaume unatakiwa uoe, uwe kichwa na uongoze familia
vinginevyo una fail ile mbaya

Kufeli unazungumzia kivipi..
Maana hapa Duniani tunaona wengi waliokimbia ndoa na wakafanikiwa...
Wakina diamond, dangote, na ma actor kibao hull duniani Hawana ndoa na Wana mafanikio makubwaa.

Unapozungumzia kufeli UNAMAANISHA NINI?

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…