Hakuna mwanamke nimekutana nae ambaye anatoa mali yake au pesa zake kwa moyo mkunjufu kabisa bila kuiwaza na kuikumbuka kila saa na kuanza kutengeneza mazingira ya kuidai.Aidha binafsi uwe na kitu na mwanamke awe na kitu ndio muungane hakuna kupeana lift, na mali ya kila mmoja itambulike hapo ndipo upendo wa kweli utajidhihirisha.
Kila siku huwa nasema wanawake HAWANA UPENDO WA KWELI KABISA zaidi ya kinyemela fedha zako, ngoja zikuishie ndipo utajua mpendwa alikuwa ni fedha na si wewe, pumbavu sana.
Mimi mke wangu hata asipogusa chochote kama housegirl yupo na kufanya kazi yake vizuri, nitampongeza mke wangu kwa kusimamia vizuri huyo housegirl.Hahaha mkuu hivi siyo ninyi ambao mkiajiri housegirls baadaye mnaanza kulalamika kuwa oo sijui mke kajisahau sana housegirl ndio anafanya kila kitu na mwisho mnaanza kutembea na hao housegirls
Sent from my S6 using JamiiForums mobile app
Sawaaa....lakini kama hamjafunga ndoa nani atakuwa msimamizi wa malinza watoto ukiwa haupo??Mkuu kukataa ndoa sio kukataa kuishi na mwanamke , kinacho pigwa apa ni kufunga pingu za maisha .
Issue sio kuhudumia. Issue ni unahudumia mtu wa aina gani. Mabinti wa sasa mpo so focused kwenye kuhudumiwa ila mkiulizwa mnajua majukumu yenu katika mahusiano tukianza na lile la kutii na kuheshimu unakuta ni zero hakuna mnachofahamu.Sasa ulitaka mwanamke ndo akuhudumie wewe? Na majukumu ya kubeba mimba utabeba wewe sio? Ovyo kabisa ndomana mnaolewa na wanaume wenzenu sababu ya kupenda mseleleko pole kwa mama yako ya baba yako.
Me naona Mshana Jr unakwepa hoja ya msingi hapa kwenye huu mjadala. Si kwamba watu wanapinga ndoa ila hapa ukitazama upande wetu sisi wanaume kuna vitu tunazungumzia hapa na wanawake wanavideflect kama sio kuvikwepa kujibu ile direct.ASIWAJU kwa mtazamo wa haraka hakuna tatizo kabisa mtu asipooa au kuolewa.. Lakini huu ni mtazamo wa ujanani unapokuwa damu inachemka na una nguvu ya kufanya karibu kila kitu mwenyewe na huna changamoto yoyote ya maisha
Swali la pili ndoa si suala la lazima au hiari bali ni uamuzi binafsi
Umuhimu wa ndoa huonekana nyakati za shida kubwa, upweke changamoto za kimaisha, magonjwa na uzee.. Kuna mahali unafika unahitaji wa kukuhudumia na kukusaidia maana hujiwezi tena! Huyo hawezi kuwa mzazi ndugu, mtoto ama rafiki
Kuna nyakati unamhitaji mtu wa kukaa naye na kumweleza hisia zako, maumivu yako furaha yako maono yako nk
Katikati ya hali zote hizi na nyinginezo mtu huyo si mwingine bali ni mke au mume
Basi ndio mkubali kwamba mke akiwa mfanyakazi au mfanyabiashara hataweza kutimiza majukumu ya nyumbani ikiwemo na kukulea wewe pamoja na watoto ipasavyo hivyo muache kulala
Kwa upande wangu nimekubaliana nalo kabisa kwasababu akili yangu nimeiweka kwamba yotehayo anafanya kwa maendeleo yetu hata kama ni kidogo anachochangia kwakungu inaonesha ni jinsi gani anajitoa siyo kwa maneno tu bali kwa vitendo kwangu mimi, watoto na ndoa yake.Basi ndio mkubali kwamba mke akiwa mfanyakazi au mfanyabiashara hataweza kutimiza majukumu ya nyumbani ikiwemo na kukulea wewe pamoja na watoto ipasavyo hivyo muache kulalamika
📌Ndoa ni kwa ajili ya wanaume kamili. Ndoa si kwa ajili ya wavulana!
Dah ila aisee tukiacha hii mada, tukijielekeza katika hii picha watu wanakula vitu vya ajabu jamani khaaaaaah. Hayo mabaka sijui imekuwaje.Hawa ndio vinara wa kupinga ndoa.. Vijana wa hovyo.. Hapo anaona kafanya bonge la tukio la kijanja kumbe lofa tuuView attachment 2509032
Hili ni gumu sana kwa sasa..Wazazi hawaishi sana na watoto kama ilivyokuwa huko zamani .Kwahiyo anaweza kuwa na mtoto lakini asimfahamu tabia yake ya kweli akiwa nyumbani na maeneo ya nyumbani ana act tuHata wwe unaelekea kuwa mzazi amini ..Tafuta familia ,tabia usizozipenda usivumilie kabisa kwa mkeo mtarajiwa Bora ukachukue kijijini.
Angalia tabia za mama ako na jinsi alivyokulea basi nawe tafuta mwanamke mwenye tabia izo ikiwezekana muombe mama ako akutafutie mchumba kutoka jamii yake.
Kichaa ,siwezi kukupangia hata ufanye uwizi ni juuu lako..Kuleta kampeni na kushawishi watu ndo hatutaki.
At least tutaolewa sasa...daah
So goodHatuoi tunazalisha kisha tunapita hivi.
STAMINA amesikia lakini....?Good morning Tanganyika!
Nimeshindwa kuvumilia baada ya kuona ongezeko la mada za kupinga kuoa, ndoa na maisha ya ndoa! Jamii Forums ni kama kioo cha Taifa kwasasa. Think tank kubwa ya nchi nathubutu kusema iko humu JF, sasa kitu kinapotrend sana Jamii forums ni lazima upate picha ya kinachoendelea nchini.
Hili ongezeko la mada za kupinga, kukosoa, kukejeli ndoa na maisha ya ndoa si jambo zuri hata kidogo bali ni msiba kwa taifa zima! Kuna sumu mbaya wamelishwa vijana wetu na imewaingia barabara!
~ Kukataa ndoa ni kukataa kujikubali.
~ Ni kukataa kujitambua.
~ Ni kukataa majukumu.
~ Ni kukosa malezi sahihi.
~ Ni kukosa akili.
~ Ni kukosa hekima.
~ Ni kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu (kwa waamini).
~ Ni kukosa upendo upeo na maono!
Tunataka kuunda Taifa gani bila ndoa?
~ Ndoa ndio chanzo cha familia.
~ Ndoa ni dalili njema ya ukomavu wa akili.
~ Ndoa ni msingi wa uwajibikaji kujali, amani, furaha na upendo.
~ Ndoa ni future, bila ndoa future haina maana sana.
~ Makuzi yasiyo sahihi.
~ Wazazi wasiojitambua.
~ Wazazi wasio na muda wala ukaribu na familia zao.
~ Utandawazi.
~ Elimu potofu mitandaoni juu ya dhana nzima ya ndoa na maisha yake ni visababishi vikubwa mno vya matokeo hasi wanayopata vijana kuhusu ndoa na wao bila kujitambua huyafanya hayo kama ndio uhalisia na kuja na mada za kila aina.
Kama maandiko ya misahafu ya kiimani yanawaasa wanaume waishi na wanawake kwa akili, tafsiri yake ni kwamba mkataa ndoa hana akili ndio maana hawezi kuishi maisha ya ndoa.
Ukomavu wa kiakili, maono na hekima hukufanya uitamani ndoa ili kujipima. Uwezo wako wa kumudu maisha ya ndoa. Utayari wako wa kuhudumia ndoa. Ujasiri wako wa kuyakabili magumu ya ndoa nk, nk.
Ndoa ni kwa ajili ya wanaume kamili. Ndoa si kwa ajili ya wavulana!
Mjadala utaendelea.
Tafsiri ya neno ndoa ni kuvumilia malezi mabovu ya mwenzako
Kama we ni msukuma isiwe sababu ya kunishawishi ugali n mtamu ..Pambana na ushamba wako ..Kila mtu ashinde mechi zake hauna jipya la kunifundishaHutaki wewe kaa kutulia,kwani watu wasipo oa wewe kinakuwasha nini?kila mtu na maisha yake.
Naropoka haya kajambe.
Nyie ndo mnatengeneza watoto wa mitaani watoto wanaokosa malezi ya baba na mama. Unadhani malezi ya mtoto ni kumwaga tu mbegu na kwenda labor.
Watoto wa kiume wanazaliwa na kukosa malezi ya baba unajua madhara yake au una bwabwaja tu.
Kuoa ama kuolewa sio lazima, lakini kufanya kampeni ili kubadilisha mind ya kila mtu haikubaliki.
Unachoona hakikufai mwenzio kinamfaa.
Kaa hapo usioe, ukazae huko na uwaambie watoto wako wasije kuoa ama kuolewa.
Tatizo Zinaa imekua rahisi sanaa na inazidi kurahisishwa kadri siku zinavoenda ndo mna mtu anaona ya nini kuoa kma kile ambacho angekipata ndani ya ndoa anakipata sasaGood morning Tanganyika!
Nimeshindwa kuvumilia baada ya kuona ongezeko la mada za kupinga kuoa, ndoa na maisha ya ndoa! Jamii Forums ni kama kioo cha Taifa kwasasa. Think tank kubwa ya nchi nathubutu kusema iko humu JF, sasa kitu kinapotrend sana Jamii forums ni lazima upate picha ya kinachoendelea nchini.
Hili ongezeko la mada za kupinga, kukosoa, kukejeli ndoa na maisha ya ndoa si jambo zuri hata kidogo bali ni msiba kwa taifa zima! Kuna sumu mbaya wamelishwa vijana wetu na imewaingia barabara!
~ Kukataa ndoa ni kukataa kujikubali.
~ Ni kukataa kujitambua.
~ Ni kukataa majukumu.
~ Ni kukosa malezi sahihi.
~ Ni kukosa akili.
~ Ni kukosa hekima.
~ Ni kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu (kwa waamini).
~ Ni kukosa upendo upeo na maono!
Tunataka kuunda Taifa gani bila ndoa?
~ Ndoa ndio chanzo cha familia.
~ Ndoa ni dalili njema ya ukomavu wa akili.
~ Ndoa ni msingi wa uwajibikaji kujali, amani, furaha na upendo.
~ Ndoa ni future, bila ndoa future haina maana sana.
~ Makuzi yasiyo sahihi.
~ Wazazi wasiojitambua.
~ Wazazi wasio na muda wala ukaribu na familia zao.
~ Utandawazi.
~ Elimu potofu mitandaoni juu ya dhana nzima ya ndoa na maisha yake ni visababishi vikubwa mno vya matokeo hasi wanayopata vijana kuhusu ndoa na wao bila kujitambua huyafanya hayo kama ndio uhalisia na kuja na mada za kila aina.
Kama maandiko ya misahafu ya kiimani yanawaasa wanaume waishi na wanawake kwa akili, tafsiri yake ni kwamba mkataa ndoa hana akili ndio maana hawezi kuishi maisha ya ndoa.
Ukomavu wa kiakili, maono na hekima hukufanya uitamani ndoa ili kujipima. Uwezo wako wa kumudu maisha ya ndoa. Utayari wako wa kuhudumia ndoa. Ujasiri wako wa kuyakabili magumu ya ndoa nk, nk.
Ndoa ni kwa ajili ya wanaume kamili. Ndoa si kwa ajili ya wavulana!
Mjadala utaendelea.
Mbona wewe ulizaliwa??? Bila ndoa ya mama yako na baba yako, ungezaliwa????
Huo ni uoga wa maisha