Mkuu umeongea mengi ila bado sijaona kama umekuja kwenye hoja niliyoizungumzia in the first place, kwahiyo kwako ni kipi kinawezekana je wewe unaona inawezekana mwanamke aliyeajiriwa anayetoka nyumbani saa kumi na mbili asubuhi, na kurudi saa kumi na mbili jioni amechoka kama mumewe kufanya majukumu ya nyumbani ipasavyo
Hivi unajua kwamba kwa hao wazungu kazi za ndani pamoja na kulea watoto ni za wote mwanaume na mwanamke, kwamba yeyote atayewahi kurudi nyumbani kabla ya mwenzie basi atafanya au wakiona mambo ni mengi wanaweka msaidizi wa kazi, unajua kwamba kwa wazungu ni kawaida mwanaume kuamka asubuhi na kumuandalia mkewe breakfast huku mkewe kalala ilihali kwa waafrika itaonekana mume kakaliwa
Na unajua kwamba kwa waarabu mambo ni tofauti wao mwanamke anakaa tu ndani na mwanaume ndio anatafuta pesa na kuhudumia mke pamoja na watoto, sasa kwanini waafrika hamtaki kuchagua moja hapo kati ya kusaidiana wote majukumu yenu au kila mmoja afanye majukumu yake kikamilifu, yani ninyi mnataka mume afanye majukumu yake tu ila mke afanye majukumu yake na ya mume
Hilo la kusema kwamba mke akipata pesa ni za kwake bado halina mashiko sababu point ni kwamba bado anatafuta pesa, maana ilitakiwa akae ndani na jukumu la kumhudumia lilikuwa la mume ila kwa sababu ya ubinafsi wa wanaume wengi wa miaka hii na kukimbia majukumu, basi wanaona kama kuhudumia wake zao ni kama kuwafanyia favour
Na sababu kwanini wanawake wengi pesa zao wanatumia wenyewe ni hiyo niliyoisema kwamba wanaona bado majukumu ya nyumbani wanaachiwa wao, ndio maana nao hawaoni faida ya kusaidia majukumu yenu sababu ninyi hamtaki kusaidia ya kwao, lazima tuchague kimoja kusaidiana majukumu ya kila mmoja au kila mtu afanye majukumu yake ila siyo mwanamke afanye majukumu yote ya mwanaume na mwanamke
Sent from my S6 using
JamiiForums mobile app