Mali za CCM zilizotokana na makato kwa raia wote wakati wa chama kimoja ni haki ya nani?

Mali za CCM zilizotokana na makato kwa raia wote wakati wa chama kimoja ni haki ya nani?

Uwanja was Mapinduzi mkoani Mbeya ulijengwa na wananchi, meaka 1984 alipofariki EDWARD MORINGE SOKOINE, uwanja ukabadilishwa jina.

Nikishangaa mwaka 1991 CCM wakatangaza kuwa ni uwanja wao.

Kuna siku raia wapenda hakiwatatambua kuwa adui yao mkubwa NI CCM, huo utakuwa ni mwanzo TU, CCM Chanzo Cha Matatizo
Uwanja wa Majimaji Songea pia wananchi kwa sasa wazee wanakumbuka shuruba walizopata. Ilikuwa hatari sana
 
Mwaka 1977 mimi nilichangia shilingi 100 kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu Dodoma na hiyo ilkuwa kwa kila mfanyakazi Tanzania nzima, bara na visiwani. Kipindi hicho mshahara wangu ulikuwa sh. 760/- take home 660 au 690 (sikumbuki vizuri) kwa hivyo 100 ilikuwa na thamani kubwa sana na ilikuwa noti kabisa.

Hata sijui zile fedha zilizokusanywa ziliishia wapi. Watu waliuliza uliza lakini enzi zile za chama kimoja ilikuwa huwezi kufika mbali.
I see!
Ndo nazaliwa June na sasa nina mvi!
Itakuwa ulikuwa unajitunza kimwili na kiroho au ukaolewa na mme asiyekustress hadi leo tuko wote humu na bado cells zinazaliana!
Binafs nakumbuka makato kwenye mauzo ya kahawa kila mkulima kuelekezwa mali za ccm ya leo.
 

Attachments

Viwanja vyote vilipaswa kurudishwa kwa wananchi kwa kukabidhiwa Halmashauri ya maeneo husika kwa sababu ni michango ya wananchi ndio iliyojenga viwanja hivyo.
Tungekuwa mbali sana,viwanja vingekuwa sasa vina hudumiwa na Serikali kupitia Halmashauri,tungekuwa tunazungumzia namna ya kuweka viti,taa na kuweka nyasi bandia.
Mahudhurio katika michezo ingeongezeka.
CCM IMEPORA MALI ZA WANANCHI NA KUJIMILIKISHA
 
Back
Top Bottom