Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Tangu mwezi Mei mwaka huu, China imetekeleza sera ya ushuru sifuri kwa nchi 53 za Afrika ambazo zina uhusiano wa kibalozi nayo, na kuondoa kabisa kizuizi cha ushuru kwa bidhaa za Afrika zinazoingia katika soko la China.
Matokeo ya sera hii yalionekana mara moja. Katika miezi ya Mei na Juni, thamani ya bidhaa zilizoagizwa China kutoka Afrika ilifikia yuan bilioni 193.8, ambalo ni ongezeko la asilimia 23.5 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki. Mauzo ya bidhaa za kilimo za Afrika kwa China yaliongezeka kwa kasi, kwa mfano mauzo ya parachichi yaliongezeka kwa asilimia 130.
Hata hivyo, kuondolewa kwa ushuru pekee hakutoshi. Zamani wafanyabiashara wa Afrika walipouza na kununua bidhaa nchini China, walitumia dola za kimarekani, na faida inayopatikana kutokana na sera ya kutotozwa ushuru ya China ilipotea kwa kiasi kikubwa. Ili kukabiliana na changamoto hii, benki za Afrika zimeanza kuharakisha kujiunga na Mfumo wa Malipo ya RMB ya Kuvuka Mipaka (CIPS). CIPS inafanya kazi kama “barabara kuu ya kasi” kwa ajili ya uhamishaji wa fedha wa kuvuka mipaka. Kwa kujiunga na mfumo huo, benki zinaweza kufanya malipo na upokeaji wa fedha kwa RMB kwa ufanisi mkubwa, bila ya gharama ya kubadilisha fedha.
Hivi karibuni, matumizi ya moja kwa moja ya RMB katika biashara na China yamepokelewa na nchi nyingi za Afrika. Benki ya Ecobank ya Togo hivi karibuni ilisaini makubaliano ya kujiunga na CIPS. Mwishoni mwa mwezi Septemba, Benki ya Kigali ambayo ni benki kubwa zaidi ya kibiashara nchini Rwanda ilitangaza kuwa mshiriki wa moja kwa moja wa CIPS. Benki kubwa zaidi ya ndani nchini Ghana, GCB Bank, pamoja na benki ya pili kwa ukubwa nchini Angola, BFA, nazo pia zinapanga kujiunga na CIPS. Benki ya Stanbic, ambayo ni tawi la Benki ya Standard ya Afrika Kusini tayari imejiunga na mfumo wa CIPS katika shughuli zake nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Ghana, na Namibia. Hii inaruhusu malipo ya kimataifa kukamilika ndani ya dakika chache, mchakato ambao hapo awali ulichukua siku kadhaa.
Kwa wafanyabiashara wa Afrika, faida za kufanya malipo moja kwa moja kwa kutumia RMB katika biashara na China ni dhahiri. Kwanza, inaondoa hatua ya ziada ya kubadilisha fedha, kuokoa gharama na kupunguza hatari zinazotokana na kuyumba kwa viwango vya kubadilisha fedha. Pili, kwa kupunguza utegemezi wa benki za kati, uhamisho wa fedha ni haraka na wa moja kwa moja zaidi. Tatu, matumizi ya RMB wakati wa kufanya biashara na wasambazaji wa China yanahakikisha uwazi zaidi katika uhasibu na kukuza mahusiano ya kibiashara yaliyo imara zaidi.
Hatimaye, wakati sera ya China ya kuondoa ushuru kwa bidhaa za Afrika inafungua mlango, malipo kwa RMB moja kwa moja yanajenga barabara ya kasi, na kufanya biashara kati ya China na Afrika kuwa rahisi zaidi. Mlango ukiwa wazi na njia ikiwa pana, bidhaa za Afrika zinaweza kufika kwa urahisi zaidi katika soko la China. Ili ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika uimarike zaidi, huduma za kifedha lazima ziendelee sambamba. Benki za Afrika kuharakisha kujiunga na CIPS ndiyo ni moja ya hatua madhubuti.