DrKeku
Member
- Mar 5, 2024
- 6
- 22
Ili kupata cheti cha kuzaliwa kupitia mfumo wa eRITA, unatakiwa kulipa Sh20,000, kisha kwenda RITA kuchukua cheti.
Wiki hii nilifika RITA Chalinze DC kuchukua cheti cha mtoto. Baada ya kuchapisha cheti, mhudumu alikifanyia lamination na kuniambia nilipie Sh1,000 kwa ajili ya huduma hiyo. Nilipoomba control number, aliniambia malipo hayo yafanywe kwa fedha taslimu. Nililipa, lakini sikupatiwa risiti.
Sh1,000 haikuwa tatizo kwangu, bali ninachojiuliza ni kwa nini malipo hayo hayakuwa na risiti rasmi. Pia nilipouliza Sh20,000 inayolipwa kupitia mfumo wa eRITA inahusisha huduma gani, sikupata jibu.
Naomba RITA itoe ufafanuzi: Je, malipo haya ya ziada kwa ajili ya lamination ni sehemu ya utaratibu rasmi? Ikiwa ni hivyo, kwa nini malipo yanafanyika kwa cash bila control number na risiti?
Pia, je, hili ni agizo rasmi la RITA au ni utaratibu unaofanywa na baadhi ya watendaji? Naomba mamlaka husika itoe ufafanuzi kwa wananchi.