KERO Malipo ya Sh 20,000 kwa ajili ya cheti cha kuzaliwa RITA yanahusisha nini na nini? Kwanini natoa malipo ya ziada kama ya lamination?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ili kupata cheti cha kuzaliwa kupitia mfumo wa eRITA, unatakiwa kulipa Sh20,000, kisha kwenda RITA kuchukua cheti.

Wiki hii nilifika RITA Chalinze DC kuchukua cheti cha mtoto. Baada ya kuchapisha cheti, mhudumu alikifanyia lamination na kuniambia nilipie Sh1,000 kwa ajili ya huduma hiyo. Nilipoomba control number, aliniambia malipo hayo yafanywe kwa fedha taslimu. Nililipa, lakini sikupatiwa risiti.

Sh1,000 haikuwa tatizo kwangu, bali ninachojiuliza ni kwa nini malipo hayo hayakuwa na risiti rasmi. Pia nilipouliza Sh20,000 inayolipwa kupitia mfumo wa eRITA inahusisha huduma gani, sikupata jibu.

Naomba RITA itoe ufafanuzi: Je, malipo haya ya ziada kwa ajili ya lamination ni sehemu ya utaratibu rasmi? Ikiwa ni hivyo, kwa nini malipo yanafanyika kwa cash bila control number na risiti?

Pia, je, hili ni agizo rasmi la RITA au ni utaratibu unaofanywa na baadhi ya watendaji? Naomba mamlaka husika itoe ufafanuzi kwa wananchi.
Una miaka mingapi? Maana watu wanaweza kukulaumu kumbe mlamba lips wa miaka 24
 
Sasa kweli mkuu buku ndo kitu cha kuletea uzi ati hukupewa risiti. Mda mwingne tujiongeze kwa mambo madogo madogo yasituabishe. Sasa risita la buku lingekusaidia nini. Cheti kukifuata huko hope ulitumia nauli tena zaid ya buku mbili na hujalalamika lakn buku ka lamination unalalamika kweli ndugu yangu? Kwanza alikusaidia cheti kisiharibike tena kwa buku tu rafk yangu afu ati hukupewa risiti kweli kabisa hata wewe unajisikia hapo kweli?
Jamaa hoja ni kosa la jinai kutumia ofisi ya umma au miundombinu au mali za umma kwa manufaa binafsi
 
Mimi Nina miaka 50 nimeomba juzi siku nne nikawa nimepata kwa malipo ya Tshs. 7,000 ambazo nilizilipia kupitia control number mfumo uliogenerate wenyewe..Sio mtu mzima tuu, hata vyeti vya Kifo unasajili kiulaainni tatizo wabongo hawataki kabisa kujifunza kutumia MIFUMO kama eArdhi, eRita nk
Sidhani mkuu kama ni sahihi kusema kwamba cheti kipya unachoomba kwa mara ya kwamza gharama iwe 7,000.

Mtu mzima kuanzia miaka 18 nakuendelea gharama ya cheti cha kuzaliwa ni 20,000.

7,000 ni wale wenye vyeti vya zamani wanataka kubadili 'Old to New'.
 
Kwani lamination ni lazima?
Hiyo lamination si ni buku hata stationary nje ya hapo, nadhani hapo kosa lap ni kutokukuuliza kama unahitaji hiyo huduma.

Vipi kama ungekua huna hiyo buku na hawajakuliza, si inakua tafrani hapo.
 
Mimi Nina miaka 50 nimeomba juzi siku nne nikawa nimepata kwa malipo ya Tshs. 7,000 ambazo nilizilipia kupitia control number mfumo uliogenerate wenyewe..Sio mtu mzima tuu, hata vyeti vya Kifo unasajili kiulaainni tatizo wabongo hawataki kabisa kujifunza kutumia MIFUMO kama eArdhi, eRita nk
Asante sana kwa ufafanuzi wako.
 
Ili kupata cheti cha kuzaliwa kupitia mfumo wa eRITA, unatakiwa kulipa Sh20,000, kisha kwenda RITA kuchukua cheti.

Wiki hii nilifika RITA Chalinze DC kuchukua cheti cha mtoto. Baada ya kuchapisha cheti, mhudumu alikifanyia lamination na kuniambia nilipie Sh1,000 kwa ajili ya huduma hiyo. Nilipoomba control number, aliniambia malipo hayo yafanywe kwa fedha taslimu. Nililipa, lakini sikupatiwa risiti.

Sh1,000 haikuwa tatizo kwangu, bali ninachojiuliza ni kwa nini malipo hayo hayakuwa na risiti rasmi. Pia nilipouliza Sh20,000 inayolipwa kupitia mfumo wa eRITA inahusisha huduma gani, sikupata jibu.

Naomba RITA itoe ufafanuzi: Je, malipo haya ya ziada kwa ajili ya lamination ni sehemu ya utaratibu rasmi? Ikiwa ni hivyo, kwa nini malipo yanafanyika kwa cash bila control number na risiti?

Pia, je, hili ni agizo rasmi la RITA au ni utaratibu unaofanywa na baadhi ya watendaji? Naomba mamlaka husika itoe ufafanuzi kwa wananchi.
Kama ni buku kwa lamination toa tu thamini watoto wako wacha upumbavu
 
Sidhani mkuu kama ni sahihi kusema kwamba cheti kipya unachoomba kwa mara ya kwamza gharama iwe 7,000.

Mtu mzima kuanzia miaka 18 nakuendelea gharama ya cheti cha kuzaliwa ni 20,000.

7,000 ni wale wenye vyeti vya zamani wanataka kubadili 'Old to New'.
kwa hiyo vya zamani wanavichukua rita , baada ya kupata kipya?
 
Kiongozi, nimeuliza kama huo nao ni sehemu ya utaratibu wa Malipo ya Serikali? Wala haukuwa na haja ya kuandika maelezo meengi, labda kama na wewe ni mnufaika wa mambo kama haya.

INTEGRITY! INTEGRITY! INTEGRITY BUDDY.

Kwani lamination stationary bei gani tuanzie hapo kwanza
 
kwa hiyo vya zamani wanavichukua rita , baada ya kupata kipya?
Unabki nacho maana hakina kazi tena ndiyo maana ukaomba old to new.

Maana mwingine anaomba old to new baada ya kuona kimechakaa sana hivyo hana haja ya kukirudisha cha zamani maana kinakuwa useless na hakina madhara kwasababu taarifa ni za mtu yule yule.
 
  • Thanks
Reactions: Lax

SAwa mkuu
 
Back
Top Bottom