Malisa akamatwa na Polisi, Namanga na kupelekwa kusikojulikana

Malisa akamatwa na Polisi, Namanga na kupelekwa kusikojulikana

Nani aliyebadilisha Roho za hawa watanzania mbona hatukuzoea haya mambo.Tuliishi kistaarabu,mtu mwenye kosa alifika kwenye vyombo kiungwana,hatukupeana mimakosa mikubwa kubwa kukomoana,hatukuuana kwa ajili ya maneno,mtu akifa tuliombololeza wote.Kifupi tumeishi kiungwana kwa miaka mingi lakini kuanzia 2017 mambo yamebadilika, watu wamebadilika .Tuombe Mungu atusaidie turudishe roho za upendo na uungwana kwenye nchi yetu na pepo la kuuana na kunyanyasana liondoke na tuishi kwa upendo.
Zamani mambo ya kutukana viongozi wa serikali hayakuwepo
 
Malisa GJ Leo alikuwa safarini kutoka Marekani ambapo amekuwa kwa zaidi ya miezi tisa (9), tangu alipoenda kuiwakilisha nchi yetu kama mtanzania pekee aliyechaguliwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani kwenda kupata mafunzo ya uongozi. Fursa ambayo hujitokeza kwa watanzania wachache sana kama ilivyowahi kutokea kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

View attachment 3660922

Alipofika Nairobi- Kenya asubuhi ya leo, alishindwa kuendelea na safari kutokana na kuwepo kwa mgomo wa wafanyakazi unaondelea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Hivyo aliamua kusafiri kwa usafiri binafsi mpaka Namanga ambao ni mpaka kati ya nchi yetu na Kenya ili kuingia nchini kupitia Arusha.

Aliwasili Namanga majira ya saa tisa(9) mchana na kwenda kwa maafisa uhamiaji ili kugongewa hati ya kusafiria (Passport) na hatimaye kuingia nchini kama utaratibu unavyotaka.

Soma Pia: Malisa: Wakili Madeleka amekamatwa na watu waliojitambulisha ni polisi

Baada ya kufika kwa maafisa uhamiaji hao, walichukua hati yake ya kusafiria na kumwambia kuwa haisomeki kwenye mfumo (system) hivyo wao hawana namna ya kufanya mpaka mkuu wao (in- charge) aje ndio anaweza kuona kwenye mfumo.

Kutokana na kadhia hiyo, na kwa kuwa aliambiwa Mkuu huyo hayupo kwa muda Malisa GJ aliendelea kukaa katika ofisi hizo za uhamiaji akisubiri Mkuu huyo kuja na kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi.

Cha kushangaza ilipofika saa moja jioni, alichukuliwa na gari ambalo si la Polisi jeupe Double Cabin na kupelekwa kituo cha Polisi Longido. Hata hivyo gari hilo halikukaa sana likaondoka kuelekea uelekeo wa Arusha.

Mpaka natoa taarifa hii hakuna taarifa kamili za aliko Malisa GJ na nini ni sababu ya kukamatwa kwake. Aidha simu zake zote zimezimwa tangu alipokuwa anatolewa Namanga.

Nitoe rai kwa Polisi na Uhamiaji kumwachia huru mara moja au kuhakikisha wanatoa taarifa kwa umma za aliko Malisa GJ na sababu ya kukamatwa kwake. Kama haitoshi kuhakikisha anapewa haki zake za kisheria ikiwemo kuonana na mawakili wake na haki ya Mawasiliano.

Dickson Matata (Wakili)
31/8/2026
Arusha-Tanzania.

View attachment 3660903
We kima ni nani uiagize jeshi la polisi? Alifikiri nini alivyokuwa anahamasisha vurugu, uasi, kumtukana Rais wa nchi mitandaoni. Watakamatwa moja baada ya mwingine Tanzania ni mama yetu wote huwezi kutumia mitandao kutaka kuiangamiza kisa uko nje ya nchi. Ajibu mashitaka yake hii nchi siyo ya kihuni wala ya kuichezea
 
Aiseee!!! Kwenye hadidu za rejea za SAMIA kwa MAFWELE .jina la Malissa,GJ ni lazima limo..
Nilishapata mashaka kitambo...hakupswa kurudi Bongo..kabisa..
CCM ni laana..yaani Mtu kwa USA anakuwa wa maana....Nchini kwake anawindwa auawe.!!!?
Asirudi Bongo aende wapi na muda wake ulishaisha. Uongozi alioenda kuusomea ni ule upuuzi aliokua akiandika mitandaoni? Sasa ngoja wamshughulikie ajue maana ya nchi, ajue maana ya dola. Hawa vijana wa chadema ni wapumbavu, hawana maarifa, hekima, busara, heshima wao wanachojua ni kutukana mtu yeyote. Hakuna nchi itaruhusu huo upuuzi hata hiyo Marekani ndiyo kabisa, we ni adui wa Taifa
 
Zamani mambo ya kutukana viongozi wa serikali hayakuwepo
Yalikuwepo labda kwa vile hakukuwepo Simu janja na mitandao.Umewahi kujiuliza kwa nini kulikuwepo na vitabu kama Pepo ya Mabwege,Kivuli kinaishi,Wasakatonge nk..Sio kwamba watu walikuwa wanakubalia kila kitu hapana.Viongozi pia walijua kuvumilia na kusamehe tofauti na sasa.Naona visasi vinavyoitafuna Zambia vikija kwenye nchi yetu mbeleni huko.Mbona Kikwete aliweza kuishi na watu wake pamoja na kusemwa na kutukanwa.Shida viongozi wa sasa wanaishi mitandaoni wanataka kila linaloongelewa walijue
 
Wanawapoteza watanganyika, na siyo watanzania. Kwao wazanzibari ni sawa, hawaguswi......Ni sisi tu watanganyika
Ccm haiangalii uzanzibar au utanganyika hasa pale utakapo onekana ww ni hatari Kwa masilahi yao ,haya yanayo endelea Tanzania Kwa Sasa Zanzibar yamekuwa yakitokea Kwa miaka mingi hasa dhidi ya wanaharakati walikuwa Wana pinga muungano.
Kuendelea na hizo hoja zenu za Utanganyika na uzanzibar ni kubust propaganda za ccm.
 
We kima ni nani uiagize jeshi la polisi? Alifikiri nini alivyokuwa anahamasisha vurugu, uasi, kumtukana Rais wa nchi mitandaoni. Watakamatwa moja baada ya mwingine Tanzania ni mama yetu wote huwezi kutumia mitandao kutaka kuiangamiza kisa uko nje ya nchi. Ajibu mashitaka yake hii nchi siyo ya kihuni wala ya kuichezea
Zamu yako itafika bwashe subiri tu...unafukiri hata Polepole kuna siku atafikwa na yaliyomfika?
 
Nani aliyebadilisha Roho za hawa watanzania mbona hatukuzoea haya mambo.Tuliishi kistaarabu,mtu mwenye kosa alifika kwenye vyombo kiungwana,hatukupeana mimakosa mikubwa kubwa kukomoana,hatukuuana kwa ajili ya maneno,mtu akifa tuliombololeza wote.Kifupi tumeishi kiungwana kwa miaka mingi lakini kuanzia 2017 mambo yamebadilika, watu wamebadilika .Tuombe Mungu atusaidie turudishe roho za upendo na uungwana kwenye nchi yetu na pepo la kuuana na kunyanyasana liondoke na tuishi kwa upendo.
Magufuri ndo muanzilishi wa siasa za chuki ndani ya nchi hii na Samia anaonekana somo la mwalimu wake Magu lilimuingia kisawasawa.
Kipindi magufuri anaanzisha siasa za kibabe watu tunao ona mbali tulionya kuwa haya mambo aliyo yaanzisha Magu yana athari mkubwa na ya muda mrefu Kwa nchi yetu ,lakini ilivyo kuwa michawa yake ilikuwa ikitushambulia Kwa maneno mchafu eti sisi ni mafisadi,na vyeti feki.
 
Back
Top Bottom