Malisa: Wakili Madeleka amekamatwa na watu waliojitambulisha ni polisi

Malisa: Wakili Madeleka amekamatwa na watu waliojitambulisha ni polisi

Wakili Peter Madeleka amekamatwa muda huu na watu waliojitambulisha kuwa ni Polisi akiwa katika Mahakama ya uhujumu uchumi (maarufu kama Mahakama ya Mafisadi) iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Watu hao hawajaeleza sababu ya kumkamata.
Mahakama ya wahujumu uchumi IPO mikocheni? Na wewe ni miiongoni mwa waliomkamata?
 
Kwa madai ya Malisa aliyochapisha katika mtandao wa Istagram amesema Wakili Peter Madeleka amekamatwa muda huu na watu waliojitambulisha kuwa ni Polisi akiwa katika Mahakama ya uhujumu uchumi (maarufu kama Mahakama ya Mafisadi) Mikocheni, jijini Dar.

Watu hao hawajaeleza sababu ya kumkamata na hawajasema anapelekwa kituo gani? Kwa mijibu wa taarifa iliyotolewa na Wakili Gideon Mathew watu hao wamekamata pia gari yake, fedha na nyaraka kadhaa alizokua nazo.!

Soma Pia: Wakili Madeleka: Mahakama ichukue hatua dhidi ya Polisi kwa vitendo vya ukiukaji Sheria

View attachment 3650381

14 August 2026
Mahakama ya Uhujumu Uchumi
Mikocheni
Dar es Salaam, Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=4fRcvbYdTu8


Mahakama ya Uhujumu Uchumi (maarufu kama Mahakama ya Mafisadi) Mikocheni, jijini Dar es Salaam Tanzania
 
Wanakamata,wanatesa, wanapoteza na kuua watu wenye akili kubwa na kuacha wapumbavu kama Mwaipopo na Nabii Tito wanatamba mitandaoni. cc Mshana Jr
 

Attachments

  • VID-20260812-WA0001.mp4
    10 MB
Wanamsumbua tu bila sababu za msingi… mahakama haijasema au kutoa amri kwamba akamatwe… huo ni uonevu na usumbufu tu… wanataka akamsalimie Lissu huko ukonga kwa lazima…
 
Nchi inaelekea pabaya watu walipotea na wanaendelea kupotea chini ya serikali ya ccm
 
Back
Top Bottom