PostGE2025 Malisa: Wazazi wangu na majirani wamewekwa chini ya ulinzi na Polisi

PostGE2025 Malisa: Wazazi wangu na majirani wamewekwa chini ya ulinzi na Polisi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Acheni kujazana ujinga jinga hapa. Sasa kwanini mtu aje kulialia hapa kama kengele badala ya kwenda kuripoti kituo cha polisi.

Kwanini asiende kupeleka maelezo yake polisi na malalamiko yake juu ya wazazi wake kusumbuliwa? Yeye si amesema wanamtafuta yeye? Sasa si aende kituo cha polisi? Nini anaogopa ? Kwamba hajui vituo vya polisi vilivyo? Si mnataka haki ?
Kwahiyo aende kwa mapolisi hao hao tena wa wapi wewe?
 
Acheni kujazana ujinga jinga hapa. Sasa kwanini mtu aje kulialia hapa kama kengele badala ya kwenda kuripoti kituo cha polisi.

Kwanini asiende kupeleka maelezo yake polisi na malalamiko yake juu ya wazazi wake kusumbuliwa? Yeye si amesema wanamtafuta yeye? Sasa si aende kituo cha polisi? Nini anaogopa ? Kwamba hajui vituo vya polisi vilivyo? Si mnataka haki ?
Siwezi kushangaa kuona comment yako mkuu! Katika watu huku ndani ambao ni zero brainer kaka unaongoza kabsa!
Kwanza kabsa Kaka Malisa na familia yake wameshachukua RB ambayo Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kasema haifatambui!
Kingine sio kila jambo lenye mada serious ulete mambo ya mbogamboga!
Hao no wazazi wake sio wazazi wa wako! Acha hizo!
 
Jana nilitoa Uzi wakupongeza kwa kile kilicho wapata MAASKARI pale mbeya ajabu akaja memba ambaye anajifanyaga mtetezi wa wanyonge akaja kutetea mapolisi akiwa yeye na shoga yake nilishangaa sana tena ananita mjinga kisa kuwananga polisi nilimshitukia kwa unyama walio nao hao watu huwezi pata moyo wa kiwatetea huwezi huyo Beira boy ni spy nawachqna atakae sikia asikie na atakae puuza apuuze
 
Naona hii ndio njia mpya ya Samia na genge lake wanatumia ili kuwapata wazalendo wa Watanganyika.

Kuna dada mmoja wa chadema geita waliteka familia yote, wazee, watoto hadi majirani. Polepole walimteka dada yake, wakajaribu kwa mama yake. Familia ya Malisa inafanyiwa mambo hayohayo.

Halafu Mwigulu akwambia kuna tume ya maridhiano. Tutunze amani yetu. Amani kwao ni ukae kimya hata akitekwa, akiuwawa, kutupwa jela ndugu yako, wakifisadi nchi na kuiba chaguzi.
 
Ndugu zangu, Muda huu (mchana wa leo Disemba 20, 2025) askari wenye silaha wapo nyumbani kwa wazee wangu, kijiji cha Old Moshi Kidia. Leo wameenda na magari mawili, yenye namba za usajili.

Wamemuweka mama yangu mzazi(70) chini ya ulinzi na wamemnyang'anya simu. Majirani walioenda kushuhudia, nao wamewekwa chini ya ulinzi!

Tumewasiliana na Mwenyekiti wa Kijiji ili aende kujua nini kinaendelea lakini naye sasa hapatikani (bila shaka nae kawekwa chini ya ulinzi). Mpaka sasa hatujui nini kinaendelea.

Nalaani vikali tukio hili la kinyama. Ikiwa Polisi wananitafuta mimi, zipo njia nyingi wanaweza kutumia zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria za Nchi kuliko kuwaghasi wazazi wangu ambao ni wazee. Huu ni unyama na haukubaliki

Tukio hili limetokea leo baada ya jana kutoa taarifa ya watu wasiojulikana (ambao hawakujitambulisha wala kuwa na magari yenye namba) kuvamia nyumbani usiku wa manane na kukata umeme.

Marafiki zetu ambao ni mawakili waliopo Moshi wanaelekea kijijini kutoa msaada wa kisheria. Naomba watu wa Old Moshi Kidia muende kwa wingi hapo nyumbani kujua kinachoendelea.

Uovu huu usikaliwe kimya!
Do, nachoka sana
 
Back
Top Bottom