Maliwato si lazima yachukue nafasi kubwa kwenye nyumba

Mimi bathroom yangu nikiwa ndani nikisikia kishindo kwa nje inabidi nikohoe kidogo ili mtu ajue kuna mtu ndani maana mlango mbovu inabidi naushikilia huku namalizia kazi maalumu
 
Favorite part of the house kwangu ni hiyo choo (me huwa naita Rest room or thinking room). Maana nikiingia huko huwa nabeba simu kabisa. Naweza kaa hata lisaa au saa na nusu. Just a place ambapo napata privacy ya kutosha kuwa pekee yangu mbali na dunia na walimwengu.

So Kimsingi kwangu ujenzi wa choo unazingatia vigezo vya rest room.
 
40 sqm au 4-6 sqm. 40 sqm ni sawa na mita 4 x 10 au 5 x 8, hata sitting room basi ni ndogo
Ni kweli...ila wapo wajengao majumba ya kifahari wanafanya hilo wale wenye hobby na kuoga kama sehemu ya relaxation (sio tu sehemu ya kuosha mwili)...
 
Exactly mkuu..sisi wabongo wengi tunaona huko ni sehemu ya kukaa dakika 5 maximum 10..wakati baadhi wana spend huko kama usemavyo 1hr ama zaidi kwa kuwa mazingira ni safi nadhifu na ya kuvutia...kind of mini spa
 
unaweza kuweka choo karibu ná sitting


Choo Karibu na sitting room!!!--- ili watu wakiwa sitting room wasikie mlio wa tumbo la kuendesha??!!, ili harufu ya huko ukifungua mlango wa maliwato iwapige watu wa sitting room??.

Katika Chumba kidogo cha choo ni lazima kuwepo na Ventilators vinginevyo chumba kidogo hakifai kiafya.
 


Dah, nikiangalia hizi picha nikifananisha na hapa ninapochutama kufanya yangu, mh! Maisha yapo tofauti jamani. Eti natazama picha nanyong'onyea utasema mtu kanionea. kumbe maisha tu yamenipiga
 
Una maana urefu mita 8 na upana mita 5 ndio 40 sqm mbona hilo bathroom kubwa sana zaidi ya sitting roo
Hiyo kwa mabwanyenye wenye fedha zao..sisi makabwela 6 hadi 12 sqm zatutosha kiasi kwamba tunadhani hiyo ndio standard..btw kuna sitting ni kubwa kuliko 40sqm so definitely mtu mwenye ukubwa huo wa bathroom sitting yake iko massive vilevile..ujue hatulingani watu dunia yako sio ya mwingine
 
Kama una eneo kwa nini usijinafasi?.

long baths and comfortable sh.**ing is very therapeutic
 
Exactly mkuu..sisi wabongo wengi tunaona huko ni sehemu ya kukaa dakika 5 maximum 10..wakati baadhi wana spend huko kama usemavyo 1hr ama zaidi kwa kuwa mazingira ni safi nadhifu na ya kuvutia...kind of mini spa
Yeees thank youu
 
Pakubwa ndio pazuri, sio kabafu kadogo ukijisugua mgongo mara tiiiii umejigonga kiwiko, unainama kidogo, ukiinuka tiiii umegonga kiuno kwenye bomba..... umemaliza kuoga kwa hasira unatoka zako mara tiiiii kidole kidogo cha mguu kwenye mlango
Mmh kwani ukioga huwa unafanya na mazoezi ya kung fu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…