Malkia wa Sheba (Queen of Sheba) ni nani?

God'sBeliever

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
5,788
Reaction score
3,033
Naskia wakimtaja sana huyu malkia wa sheba kama mwanamke flani amaizingi sana na mtaalamu sana wa mapenzi.

Pia aliwahi kumtembelea mfalme Solomoni baada ya malkia kusikia habari za hekima za mfalme Solomoni.

Inafahamika malkia alizaa mtoto wa kiume aliemuita Menelik na huyu alikuja kuwa mfalme na huu utawala ulianza mwana 1232 hadi ulipofikia kikomo pale mfalme wa mwisho Haile Selassie alipopinduliwa mwaka 1975 na habari za huu ufalme zikafikia kikomo hapo.

Walikuwa wanauita Solomon family/dynasty. Japo kwenye biblia haijawekwa wazi kwamba Solomon alilala na malkia wa sheba(makeda). Embu wenye additional information wajazie please tupate habari iliyonyooka.

Kumbuka pia Solomon alikua anapenda sana wanawake na alilala na zaidi ya wanawake 1000 so uwezekano wa wao ku sex ni mkubwa. Pia tunaona walivyo Wayahudi wengi weusi Ethiopia.

Swali langu ni juzi kuna mwanamke nilimsema vibaya akaanza kunichamba kwa maneno ya kasha kwamba yeye ni malkia wa sheba anajua sana kuteka wanaume.

Sasa najiuliza huyu mwanamke wa usheba vipi? Embu mwenye taarifa atupe kuhusu habari zake za ngono maana yaonekana alikuwa mwanamke mmoja hatari sana.
========

Baadhi ya michango kutoka kwa Wadau


 
Kwa nini using Google ukapata full information? Hakuwa malkia wa mapenzi hata kidogo wala mambo ya ngono hakuwa nayo kabisa. ..she was genius ndiyo maana akaenda kutafuta hekima nyingine kwa Mfalme SELEMANI. ...Google pia MANSA MUSSA wa MALI , wote wana very interesting story. ..na ni waafrika. ..good luck my friend
 
Wadau nimefika home lakini so late na unajua folen zetu hizi Dar,. nlisema ningeelezea habari za Malkia wa Sheba ambapo pia kuna utata kama alikuwa ni kutoka yemeni au hii ethiopia na pia kuna scholars wanaosema alikuwa ni malkia wa Egypt na Ethiopia. lakini sijafaham kwa nini huyo dada alimhusisha na mambo ya utamaduni mkubwa wa waafrika (ngono) huyu umaarufu wake si kwenye mambo hayo. nadhan ni misconception tu. naomba kesho niwaelezee historia yake kwa kuwa nimebakiwa na dk chache tu za kulala kwa sasa. kesho mchana nitakuwa nimewapa kisa chake. naomba mniwie radhi wadau.
wabillah tawfiq.
 
Suleiman alisex naye akampata mtoto wa kwanza alieitwa menelik ambao ndio ufalme ulianzia hapo wa kisolomon ukafikia kikomo pale haile selassie alipipinduliwa mwaka 1975. acha ubishi kwenye biblia haijawekwa wazi ila kunasehemu niliona baada ya menelik kuwa mkubwa alienda kumtembelea baba yake (solomon) na huko alipewa zawadi pia solomon alituma watumish kwa ajili ya kuiangalia hiyo familia, kumbuka alitaka amfanye awe meneli awe mfalme wa israel lakini ilishindikana
 
Sawa. Tunakusubiri
 
Kwa calendar gani unayotumia?Mbona miaka ya uongo na ni Queen of Sheba yupi utawala wake uliongozana na Haille Selassie gani?
 
Alimegwa kirahisi sana na Jedediah na akarudi kwake na kitumbo.
Ehh jedediah ndo nani mkuu? mimi naimani solomon alikula mzigo sababu huyu jamaa pamoja na hekima zake alizama sana kwa wanawake na nadhani hata chanzo cha wayahudi ethipioa ni huu uzao kati ya sololom na malkia wa sheba. ufalme wa ethiopia wanauita solomon dynasty!
 
Kwa calendar gani unayotumia?Mbona miaka ya uongo na ni Queen of Sheba yupi utawala wake uliongozana na Haille Selassie gani?
1000 ivi na kitu ndio huyu mtoto wa malkia wa sheba alianza ufalme then later ukaitwa solomon dynast (menelik ndio mtoto wa kiume wa huyu malkia) ukomo wa huu ufalme wa solomon uliisha pale haile selesie alipopinduliwa mwaka 1975.
 
Kwahiyo huyo malkia alikuwa anamsaliti mume wake ambaye ni mfalme hadi kutoka na mfalme sulemani?
 

Jedediah ndiye mfalme Suleimani, linamaanisha MPENDWA WA MUNGU. Hili ndiyo jina halisi la mfalme Suleimani na alipewa na nabii Nathani mara baada tu ya kuzaliwa. Kwa maelezo zaidi soma 2 Samuel 12:25.
Haya turudi kwenye mada yetu, baada ya Malkia Mekeda kwenda kwa Mfalme Jedediah alimjaribu lakini akakuta Suleimani ana utajiri mkubwa wa kuisha na akili kumkichwa. Sasa wanahistoria wa Kiyahudi wanasema kwamba Mekeda akaambiwa na Suleimani alale kwenye kasri yake lakini akamuambia mfalme Suleimani kama ukitaka nilale Sharti usiniguse. Suleimani akamwambia sawa lakini na wewe usiguse kitu chochote cha ndani ndani ya nyumba yangu bila ruhusa yangu.

Suleimani alikuwa na mpango wake kichwani, akawaagiza watumwa wake waweke pilipili na viungo vingi kwenye chakula.
Makeda alivyokula usiku kiu kali ikamshika, basi akataka maji Suleimani akamjibu akasema tulikubaliana hutagusa chochote bila ridhaa yangu. Basi Makeda akazidiwa ujanja ndiyo maana akasema Suleimani ni Mfalme mwenye akili sana kuliko alivyowahi kusikia.

Aliondoka Yerusalem na mimba, akajifungua mtoto wake wa kiume akamuita jina MENELEKI 1 maana yake "SON OF THE WISE". Menelik alivyokuwa mkubwa alienda kuapishwa Yerusalem. Na mwanahistoria wa Kirumi Flavius Josephus anakuambia alikuwa Mfalme wa Ethiopia na Egypt, hapo alipewa jina la babu yake DAUDI. Sasa alivyorudi Ethiopia Mfalme Suleimani alituma kundi la Wasomi wa Kiyahudi zaidi ya 1000 na moja wapo walikuwa kuhani AZALIA na ZADOKI ambao kwenye biblia wapo. Hawa walitumwa kwa dhumuni la kumsaidia atawale ufalme wake vizuri.

Wayahudi wa Ethiopia wale wuesi wanaitwa Falahasha na siyo wote ni uzao wa Mfalme Suleimani. Wengine ni wayahudi kutoka kabila la dani ambalo walipotea baada ya kuvamiwa na Ashuru na Wakaldayo kutoka Babeli. Wayahudi weusi wako wengi sana na hichi watu wengi wanakipinga lakini ndiyo ukweli wenyewe. Lakini Wayahudi walianza kuoana na weusi tangu wako Misri na ushahidi mkubwa ni Abrahamu baba wa Wayahudi alizaa na kijakazi wake Hajira ambaye ndiyo mama wa Waarabu. Hajira alikuwa ni mtu wa Misri na Misri ilikuwa inatawaliwa na watu weusi kabla ya Waarabu. Sehemu ya Pili Nabii Musa alimuoa Zipora mtu wa Ethiopia. Ethiopia ilikuwa inatawaliwa na watu weusi hivyo kuwepo na Wayahudi weusi ni kitu cha kawaida sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…