Malkia wa Sheba (Queen of Sheba) ni nani?

Malkia wa Sheba (Queen of Sheba) ni nani?

Huyu ametajwa katika Quraan Tukufu , na jina lake linajulikana kama Balqiis.. Ni MAlkia wa Sabaa' hukoo nchini Yemen ambayo inajulikana kama Sheeba.. na kuna kipindi niliona Video inamuonesha mwanamke mmoja wa kizungu akitafuta histora ya huyu Malkia mjini Yemen kumsaida mumewe ambae aliianza hii kazi kwa bahati Mbaya akapooza mwili.

Kwa hiyo huyu mwanamke akawa anajaribu kumalizia kazi aloianza mumewe ..

KWa kifupi Quraan imeeleza hivi ...

Nabii Suleiman Alaihi Ssalaam alikuwa akikaa akizungukwa na Ndege kumuwekea kivuli, siku hiyo kuna Ndege akiitwa Hud Hud alikuwa hayupo sehemu ya kivuli kiasi jua likapitilza mpaka kwenye paja la Nabii Suleiman akasema hii sehemu anatakiwa aifunike Hud Hud .. yuko wapi? Endelea kusoma sasa

20. Na akawakagua ndege, na akasema: Imekuwaje, mbona simwoni Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walio ghibu? Maelezo
21. Kwa yakini nitamuadhibu kwa adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja ya kutosha.
22. Basi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea khabari za yakini.
23. Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa.
Maelezo
24. Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shet'ani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka, Maelezo
25. Na hawamsujudii Mwenyezi Mungu ambaye huyatoa yaliyo fichikana katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza. Maelezo
26. Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi tukufu.. Maelezo
27. Akasema (Sulaiman): Tutatazama umesema kweli au wewe ni miongoni mwa waongo. Maelezo
28. Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha waache na utazame watarejesha nini. Maelezo
29. (Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu. Maelezo
30. Imetoka kwa Sulaiman nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Maelezo
31. Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri. Maelezo 32. Akasema: Enyi wahishimiwa! Nipeni shauri katika jambo langu hili, kwani mimi sikati shauri yoyote mpaka mhudhurie. Maelezo
33. Wakasema: Sisi ni wenye nguvu na wakali kwa vita; na amri iko kwako, basi tazama ni nini unaamrisha. Maelezo
34. Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo. Maelezo
35. Lakini mimi nitawapelekea zawadi, nami nitangoja watakayo rudi nayo wajumbe. Maelezo
36. Basi alipo fika (mjumbe) kwa Sulaiman, alisema (Sulaiman): Hivyo ndio nyinyi mnanisaidia kwa mali? Aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko aliyo kupeni nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia hii zawadi yenu. Maelezo 37. Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge. Maelezo
38. Akasema: Enyi wahishimiwa! Ni nani kati yenu atakaye niletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu amri. Maelezo
39. Akasema: Afriti, katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu. Maelezo
40. Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu. Maelezo
41. Akasema: Mgeuzieni kiti chake cha enzi hiki, tuone ataongoka, au atakuwa miongoni mwa wasio ongoka. Maelezo
42. Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu. Maelezo
43. Na yale aliyo kuwa akiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yalimzuilia. Hakika yeye (Malkia) alikuwa katika kaumu ya makafiri. Maelezo
44. Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Maelezo

Ni Kisa kirefu sana ...
Ukweli unajionyesha kila mahali ya kwamba BIBLIA IMECHAKACHULIWA ila wanapinga kwa maslahi ya dunia.ALLAH atawaadhibu kwakukadhibisha kwao
 
MALCOM LUMUMBA huwa siamini sana hiyo stori ya Nuhu kuwa amezaa hayo mataifa. Inapingana kabisa na tafiti zinazosema mwanzo wa mtu ni Afrika.

Lakini hata nje ya hizo tafiti, huyo mtoto mweusi wa Nuhu alimchungulia baba yake akalaaniwa. So wale wanaopenda habari ya kutukuza weupe wanapenda kuangushia hizo tuhuma kwa weusi. UONGO MKUBWA HUO!!
 
Hebu tuanze jambo la kwanza.
Fuvu lilikutwa Olduvai Gorge siyo la HOMO SAPIEN bali ni HOMO HABILIS ambaye alikuwa ni aina ya nyani.
Mimi siamini kama binadamu wa kwanza alikuwa ni nyani. Binadamu alikuwa ni banadamu tangu mwanzo.
Ukukubaliana na utafiti wa daktari Leakey ni dhahili kwamba unaamini binadamu ametokana na nyani.

Pili, umesoma wapi kwamba weusia wametokana na laana?
Nuhu alimlaani Canaan mtoto wa HAM na siyo HAM mwenyewe.
Kwa kukusaidia ukisoma kitabu cha MWANZO 9:25 "Nuhu akasema na alaaniwe Canaan;atakuwa mtumwa kabisa wa ndugu zake"
Canaan iko Mashariki ya kati na siyo Afrika, na walifutiliwa mbali na Waebrania wakiongozwa na Joshua sasa hiyo laana ya mtu mweusi imetoka wapi?

Tatu, baba wa watu weusi siyo Canaan aliyelaaniwa. Ham alikuwa na watoto wengine kama Cush, Mizraim na Phut.
Cush ndiyo baba wa Waethiopia, Mizraim ndiye baba wa Wamisri na Phut ndiye baba wa Walibya. Hata Ptolemy baba yake na Cleopatra aliandika kwamba Libya na ya uzao wa Phut. Wanahistoria wanakubaliana na hili kwanini wewe useme ni wongo halafu hutoi sababu za msingi?

Nne, kwa mtazamo wako kwamba biandamu alitokana na nyani utakuwa unakubaliana na theory of evolution. Hivyo mpaka sasa mzungu ndiye atakuwa binadamu Advanced kuliko watu weusi. Na kinachosikitisha ni unaamini kwamba wewe ulikuwa ni nyani.

Hebu dadavua kwanza haya halafu uje tuendelee kuelimishana. Karibu sana Mkuu.

big gift
 
Safi kabisa kwa maneno mazuri. Ni miaka nenda tumeona nyani kibao lakini hakuna hata mmoja aliepatikana kukaribia na binadamu. so theory ya dr leakey ni ya uongo.
Ila binadamu ni binadamu tuu na tunabadilika kulingana na mazingira.
 
Walielewana kwenye maongezi? I mean King Solomon aliifahamu lugha ya huyo malkia? What about the language barrier?
Ethiopia hadi Israel ni mbali mnooo
Queen alitumia usafiri gani? Alijuaje ramani ya kwenda Israel ?

Ethiopia kipindi hiki ilikuwa ni confederacy ambayo imefika hadi mashariki ya kati.
Ilikuwa imeungana hadi na misri. Ndiyo maana mwanahistoria Flavius Josephus anamwita Makeda kama Malkia wa Ethiopia na Misri, au malkia wa kusini.
Kwa kifupi huu ufalme ulikuwa mkubwa.

Hapo kwenye Lugha hebu jiulize;
1. Ufalme wa China ulikuwa na ubalozi nchini katika falme za Tanganyika hata kabla ya kuja wazungu: Je, walielewana vipi?
2. Columbus alivyofika Marekani alielewana vipi na wahindi wekundu?
3. Wahehe walifanya biashara na wangoni na Wanyamwezi: Je, walitumia lugha gani?
4. Mansa Kankan Musa alivofanya biashara ya watumwa na dhahabu na falme za dunia: Je, alikuwa ni bibi huyu au walikuwa wanaandika chini?
 
Hadith ya Malkia wa sheba imesimuliwa kwenye vitabu Vya dini mbalimbali kama vile Wayahudi, Wakristo na hata Waislamu. Biblia imemsimulia kuwa alikuwa ni Malkia wa kutoka Mashariki Ufalme wa Aksum (axum) huko Ethiopia. Na pia kuna wanahistoria wanaosema kuwa pengine ilikuwa ni kutoka ufalme wa Saba huko Yemen au toka katika hizo Falme mbili zote kwa maana ya kuwa pengine alitawala sehemu zote mbili. Kwa nini wanasema hivyo? Ni kwa sababu alipeleka Zawadi na moja wapo ikiwa ni viungo au kwa lugha ya kigeni spices. Na ina ya spices hizo inasemekana inapatikana tu kwenye maeneo hayo mawili. Na katika hili kila nchi imekuwa ikidai ni wa kwao. Na ukichukulia kuwa nchi hizi zimetenganishwa na kilomita 25 tu za maji inawezekana zote zikawa sahihi.

Katika hadithi hii ya malkia wa sheba. Anaonekana ni malkia ambaye aliamua kutafuta hekima /elimu au ukweli kuhusiana na alichokuwa akisikia kuhusu mfalme Solomon wa Israel. Mfalme huyu alisifika kila sehemu kuwa alikuwa ni mwenye hekima sana(bahati mbaya hatujapata tena dunia hii viongozi wa namna hii) hivyo alifunga safari akitumia ngamia mpaka yerusalem kuonana na Mfalme Solomon au Selemani. Lengo lilikuwa ni kupima hekima za mfalme na pia kusikia maneno yake ya hekima,mafumbo na misemo mbalimbali. Akamletea viungo(spices) manemane,dhahabu na vito vya thaman kubwa sana. kama zawadi

Mfalme seleman alikuwa amesikia habari za Malkia Sheba na Ufalme wake mkuu. Na alisikia kuwa alikuwa na umbo la kushangaza. Kuwa mguu wake wa kushoto ulikuwa umechanika kule chini kama wa mbuzi na pia ulikuwa na vinyweleo vingi sana. Akiwa na shauku ya kutaka kujua kama hizo hadith zilikuwa za kweli au fiksi tu za walimwengu miaka hiyo.(usidhani umbea umeanza sasa au kupakaziana toka miaka ya nyuma mambo haya yalikuwepo) Mfalme seleman naye kwa kujawa na shauku na umbea wa kutaka kujua kama jambo hilo ni la kweli au vipi akaagiza siku hiyo mle ndani kusafishwe na chini pang’ae kama kioo.(nadhani nao walikuwa na tiles zao za miaka ile) inasemekana alipokanyaga pale chini malkia wa sheba mfalme selemani aliona mguu wa malkia ulio chini kama wa mbuzi ukigeuka na kuwa wa kawaida mbele ya macho yake.akashangaa sana.

Malkia wa sheba akawa akimuuliza mfalme maswali mengi mengi sana na mafumbo ili kumpima hekima yake. Akamjibu kiasi cha kumridhisha kabisa na malkia akafurahia sana na baadaye akamfundisha kuhusiana na Mungu wake yeye Mfalme Seleman (Yahweh) na Malkia wa Sheba akawa muumini wake. Na hivi ndivyo Waethiopia wanaamini Jinsi ambavyo Ukristo uliingia nchini mwao yaani kupitia Malkia wa Sheba.

Malkia alikubali kuwa Mgeni wa Mfalme Seleman.na hapo alikuwa hajaolewa. Akamwonya mfalme seleman asimguse.(najua unaelewa maana ya asimguse). Na mfalme seleman akamwambia kama ni hivyo naye asichukue kitu chochote toka kwake. (toka zaman wanaume walikuwa hawatoi tu zawadi hivi hivi) na hapa mfalme alikuwa amemtega kiujanja kumbuka alikuwa na hekima sana. basi malkia akapewa chakula chnye spices nyingi sana(mfano ukila pilau matokeo yake unakunywa sana maji) Ulipofika usiku Malkia akasikia Kiu. Akachukua Glass ya Maji akanywa. Mfalme akamfuata na kumwambia amevunja makubaliano kuwa hakupaswa kuchukua kitu chochote toka kwake kwa kuwa yeye alisema asiguswe. Hivyo kwa kuahidi kuwa singechukua kitu chochote na mwishowe kunywa maji ya mle ndani amevunja ahadi na mfalme naye atavunja ya kwake ya kutokumgusa.

Basi hapo wakalala wote yaani wakafanya mapenzi na kumbuka mfalme alikuwa amemsubiria kwa hamu sana. Akamnanii….. na siku aliporudi nyumban kwake Malkia wa sheba alikuja kugundua ana ujauzito akamzaa Menelik na kumkuza yeye mwenyewe. Siku moja menelik akaamua kutembelea Israel kwenda kuonana na baba yake. Aliporudi alikuja na sanduku la agano lililokuwa limebeba amri kumi za Mungu alizotoa kwa Wayahudi. Hadith za kale zinasema kuwa sanduku liliendelea kuwa Ethiopia toka kipindi hicho na Waethiopia wana mwona Menelik kama ni Ufalme uliotukuka uliojipanua mpaka karne ya 20. Hii ndiyo hadithi ya Malkia wa sheba.
HIS IMPERIAL MAJESTY EMPEROL HAILE SELASSIE I
 
Jedediah ndiye mfalme Suleimani, linamaanisha MPENDWA WA MUNGU. Hili ndiyo jina halisi la mfalme Suleimani na alipewa na nabii Nathani mara baada tu ya kuzaliwa. Kwa maelezo zaidi soma 2 Samuel 12:25.
Haya turudi kwenye mada yetu, baada ya Malkia Mekeda kwenda kwa Mfalme Jedediah alimjaribu lakini akakuta Suleimani ana utajiri mkubwa wa kuisha na akili kumkichwa. Sasa wanahistoria wa Kiyahudi wanasema kwamba Mekeda akaambiwa na Suleimani alale kwenye kasri yake lakini akamuambia mfalme Suleimani kama ukitaka nilale Sharti usiniguse. Suleimani akamwambia sawa lakini na wewe usiguse kitu chochote cha ndani ndani ya nyumba yangu bila ruhusa yangu.

Suleimani alikuwa na mpango wake kichwani, akawaagiza watumwa wake waweke pilipili na viungo vingi kwenye chakula.
Makeda alivyokula usiku kiu kali ikamshika, basi akataka maji Suleimani akamjibu akasema tulikubaliana hutagusa chochote bila ridhaa yangu. Basi Makeda akazidiwa ujanja ndiyo maana akasema Suleimani ni Mfalme mwenye akili sana kuliko alivyowahi kusikia.

Aliondoka Yerusalem na mimba, akajifungua mtoto wake wa kiume akamuita jina MENELEKI 1 maana yake "SON OF THE WISE". Menelik alivyokuwa mkubwa alienda kuapishwa Yerusalem. Na mwanahistoria wa Kirumi Flavius Josephus anakuambia alikuwa Mfalme wa Ethiopia na Egypt, hapo alipewa jina la babu yake DAUDI. Sasa alivyorudi Ethiopia Mfalme Suleimani alituma kundi la Wasomi wa Kiyahudi zaidi ya 1000 na moja wapo walikuwa kuhani AZALIA na ZADOKI ambao kwenye biblia wapo. Hawa walitumwa kwa dhumuni la kumsaidia atawale ufalme wake vizuri.

Wayahudi wa Ethiopia wale wuesi wanaitwa Falahasha na siyo wote ni uzao wa Mfalme Suleimani. Wengine ni wayahudi kutoka kabila la dani ambalo walipotea baada ya kuvamiwa na Ashuru na Wakaldayo kutoka Babeli. Wayahudi weusi wako wengi sana na hichi watu wengi wanakipinga lakini ndiyo ukweli wenyewe. Lakini Wayahudi walianza kuoana na weusi tangu wako Misri na ushahidi mkubwa ni Abrahamu baba wa Wayahudi alizaa na kijakazi wake Hajira ambaye ndiyo mama wa Waarabu. Hajira alikuwa ni mtu wa Misri na Misri ilikuwa inatawaliwa na watu weusi kabla ya Waarabu. Sehemu ya Pili Nabii Musa alimuoa Zipora mtu wa Ethiopia. Ethiopia ilikuwa inatawaliwa na watu weusi hivyo kuwepo na Wayahudi weusi ni kitu cha kawaida sana.
Thanks mkuu
 
Heshima kwako mkuu, umeniongezea maarifa na pia wale watu 1000 waliotuma na suleimain kumsaidia menelik 1 nao walijichanganya tuu na ngozi nyeusi na kuzaa pia ya misri nilikua sina ilo wazo ili ni kweli kabisa na nategemea hadi sasa kuwe na hiyo damu ya uyahudi kwa kiasi kikubwa.
Kumbe nami ni Myahudi! Babu aliniambia walitokea kaskazini kwenye nchi ya milima[emoji12]
 
Jedediah, suleiman, Solomon nashindwa kuelewa nami nahitaji msaada
[emoji12]
Ikupilika Nkoba, Kamba Luffo

Back
Top Bottom