Masaki
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,463
- 754
Jedediah ndiye mfalme Suleimani, linamaanisha MPENDWA WA MUNGU. Hili ndiyo jina halisi la mfalme Suleimani na alipewa na nabii Nathani mara baada tu ya kuzaliwa. Kwa maelezo zaidi soma 2 Samuel 12:25.
Haya turudi kwenye mada yetu, baada ya Malkia Mekeda kwenda kwa Mfalme Jedediah alimjaribu lakini akakuta Suleimani ana utajiri mkubwa wa kuisha na akili kumkichwa. Sasa wanahistoria wa Kiyahudi wanasema kwamba Mekeda akaambiwa na Suleimani alale kwenye kasri yake lakini akamuambia mfalme Suleimani kama ukitaka nilale Sharti usiniguse. Suleimani akamwambia sawa lakini na wewe usiguse kitu chochote cha ndani ndani ya nyumba yangu bila ruhusa yangu.
Suleimani alikuwa na mpango wake kichwani, akawaagiza watumwa wake waweke pilipili na viungo vingi kwenye chakula.
Makeda alivyokula usiku kiu kali ikamshika, basi akataka maji Suleimani akamjibu akasema tulikubaliana hutagusa chochote bila ridhaa yangu. Basi Makeda akazidiwa ujanja ndiyo maana akasema Suleimani ni Mfalme mwenye akili sana kuliko alivyowahi kusikia.
Aliondoka Yerusalem na mimba, akajifungua mtoto wake wa kiume akamuita jina MENELEKI 1 maana yake "SON OF THE WISE". Menelik alivyokuwa mkubwa alienda kuapishwa Yerusalem. Na mwanahistoria wa Kirumi Flavius Josephus anakuambia alikuwa Mfalme wa Ethiopia na Egypt, hapo alipewa jina la babu yake DAUDI. Sasa alivyorudi Ethiopia Mfalme Suleimani alituma kundi la Wasomi wa Kiyahudi zaidi ya 1000 na moja wapo walikuwa kuhani AZALIA na ZADOKI ambao kwenye biblia wapo. Hawa walitumwa kwa dhumuni la kumsaidia atawale ufalme wake vizuri.
Wayahudi wa Ethiopia wale wuesi wanaitwa Falahasha na siyo wote ni uzao wa Mfalme Suleimani. Wengine ni wayahudi kutoka kabila la dani ambalo walipotea baada ya kuvamiwa na Ashuru na Wakaldayo kutoka Babeli. Wayahudi weusi wako wengi sana na hichi watu wengi wanakipinga lakini ndiyo ukweli wenyewe. Lakini Wayahudi walianza kuoana na weusi tangu wako Misri na ushahidi mkubwa ni Abrahamu baba wa Wayahudi alizaa na kijakazi wake Hajira ambaye ndiyo mama wa Waarabu. Hajira alikuwa ni mtu wa Misri na Misri ilikuwa inatawaliwa na watu weusi kabla ya Waarabu. Sehemu ya Pili Nabii Musa alimuoa Zipora mtu wa Ethiopia. Ethiopia ilikuwa inatawaliwa na watu weusi hivyo kuwepo na Wayahudi weusi ni kitu cha kawaida sana.
Hivi miaka hiyo kusafiri toka Ethiopia mpaka Israel walikuwa wanatumia usafiri gani? Meli?