Malkia wa Sheba (Queen of Sheba) ni nani?

Malkia wa Sheba (Queen of Sheba) ni nani?

Jedediah ndiye mfalme Suleimani, linamaanisha MPENDWA WA MUNGU. Hili ndiyo jina halisi la mfalme Suleimani na alipewa na nabii Nathani mara baada tu ya kuzaliwa. Kwa maelezo zaidi soma 2 Samuel 12:25.
Haya turudi kwenye mada yetu, baada ya Malkia Mekeda kwenda kwa Mfalme Jedediah alimjaribu lakini akakuta Suleimani ana utajiri mkubwa wa kuisha na akili kumkichwa. Sasa wanahistoria wa Kiyahudi wanasema kwamba Mekeda akaambiwa na Suleimani alale kwenye kasri yake lakini akamuambia mfalme Suleimani kama ukitaka nilale Sharti usiniguse. Suleimani akamwambia sawa lakini na wewe usiguse kitu chochote cha ndani ndani ya nyumba yangu bila ruhusa yangu.

Suleimani alikuwa na mpango wake kichwani, akawaagiza watumwa wake waweke pilipili na viungo vingi kwenye chakula.
Makeda alivyokula usiku kiu kali ikamshika, basi akataka maji Suleimani akamjibu akasema tulikubaliana hutagusa chochote bila ridhaa yangu. Basi Makeda akazidiwa ujanja ndiyo maana akasema Suleimani ni Mfalme mwenye akili sana kuliko alivyowahi kusikia.

Aliondoka Yerusalem na mimba, akajifungua mtoto wake wa kiume akamuita jina MENELEKI 1 maana yake "SON OF THE WISE". Menelik alivyokuwa mkubwa alienda kuapishwa Yerusalem. Na mwanahistoria wa Kirumi Flavius Josephus anakuambia alikuwa Mfalme wa Ethiopia na Egypt, hapo alipewa jina la babu yake DAUDI. Sasa alivyorudi Ethiopia Mfalme Suleimani alituma kundi la Wasomi wa Kiyahudi zaidi ya 1000 na moja wapo walikuwa kuhani AZALIA na ZADOKI ambao kwenye biblia wapo. Hawa walitumwa kwa dhumuni la kumsaidia atawale ufalme wake vizuri.

Wayahudi wa Ethiopia wale wuesi wanaitwa Falahasha na siyo wote ni uzao wa Mfalme Suleimani. Wengine ni wayahudi kutoka kabila la dani ambalo walipotea baada ya kuvamiwa na Ashuru na Wakaldayo kutoka Babeli. Wayahudi weusi wako wengi sana na hichi watu wengi wanakipinga lakini ndiyo ukweli wenyewe. Lakini Wayahudi walianza kuoana na weusi tangu wako Misri na ushahidi mkubwa ni Abrahamu baba wa Wayahudi alizaa na kijakazi wake Hajira ambaye ndiyo mama wa Waarabu. Hajira alikuwa ni mtu wa Misri na Misri ilikuwa inatawaliwa na watu weusi kabla ya Waarabu. Sehemu ya Pili Nabii Musa alimuoa Zipora mtu wa Ethiopia. Ethiopia ilikuwa inatawaliwa na watu weusi hivyo kuwepo na Wayahudi weusi ni kitu cha kawaida sana.

Hivi miaka hiyo kusafiri toka Ethiopia mpaka Israel walikuwa wanatumia usafiri gani? Meli?
 
Jedediah, suleiman, Solomon nashindwa kuelewa nami nahitaji msaada
[emoji12]

Mfalme Suleimani ni kwa lugha yetu ya Kiswahili.
King Solomon ni kwa lugha ya Kiingereza.
Mfalme Suleimani alipewa majina mawili, la kwanza lilikuwa ndiyo Suleimani likimaanisha "Mtulivu"
Jina la pili ni Jedediah au Yededia likimaanisha "Mpendwa wa Mungu" hili alipewa na nabii wa kiebrania aitwae Nathani.
 
Hivi huyu Solomon alikua Nabii au tapeli? Maana haiwezekani zinaa iwe zambi ila yeye ndie hodari wa kuzini sasa alikua anawafundisha nini wafuasi wake afu mnatuambia alikua na hekima,hekima gani za kutafuna wageni alafu yeye mwenyewe ni mume wa mtu? Mi hawa manabii wa kwenye Biblia nawaona kama vibaka tu na kuiamini Bible inabidi akili yako iwe na walakini kidogo.
 
Asante mleta uzi na wachangiaji,nimejifunza kitu kuhusu mfalme suleiman,malkia sheba na Haile selassie.kwa hio wakuu wayahudi ni rastafarian?
 
Hadith ya Malkia wa sheba imesimuliwa kwenye vitabu Vya dini mbalimbali kama vile Wayahudi, Wakristo na hata Waislamu. Biblia imemsimulia kuwa alikuwa ni Malkia wa kutoka Mashariki Ufalme wa Aksum (axum) huko Ethiopia. Na pia kuna wanahistoria wanaosema kuwa pengine ilikuwa ni kutoka ufalme wa Saba huko Yemen au toka katika hizo Falme mbili zote kwa maana ya kuwa pengine alitawala sehemu zote mbili. Kwa nini wanasema hivyo? Ni kwa sababu alipeleka Zawadi na moja wapo ikiwa ni viungo au kwa lugha ya kigeni spices. Na ina ya spices hizo inasemekana inapatikana tu kwenye maeneo hayo mawili. Na katika hili kila nchi imekuwa ikidai ni wa kwao. Na ukichukulia kuwa nchi hizi zimetenganishwa na kilomita 25 tu za maji inawezekana zote zikawa sahihi.

Katika hadithi hii ya malkia wa sheba. Anaonekana ni malkia ambaye aliamua kutafuta hekima /elimu au ukweli kuhusiana na alichokuwa akisikia kuhusu mfalme Solomon wa Israel. Mfalme huyu alisifika kila sehemu kuwa alikuwa ni mwenye hekima sana(bahati mbaya hatujapata tena dunia hii viongozi wa namna hii) hivyo alifunga safari akitumia ngamia mpaka yerusalem kuonana na Mfalme Solomon au Selemani. Lengo lilikuwa ni kupima hekima za mfalme na pia kusikia maneno yake ya hekima,mafumbo na misemo mbalimbali. Akamletea viungo(spices) manemane,dhahabu na vito vya thaman kubwa sana. kama zawadi

Mfalme seleman alikuwa amesikia habari za Malkia Sheba na Ufalme wake mkuu. Na alisikia kuwa alikuwa na umbo la kushangaza. Kuwa mguu wake wa kushoto ulikuwa umechanika kule chini kama wa mbuzi na pia ulikuwa na vinyweleo vingi sana. Akiwa na shauku ya kutaka kujua kama hizo hadith zilikuwa za kweli au fiksi tu za walimwengu miaka hiyo.(usidhani umbea umeanza sasa au kupakaziana toka miaka ya nyuma mambo haya yalikuwepo) Mfalme seleman naye kwa kujawa na shauku na umbea wa kutaka kujua kama jambo hilo ni la kweli au vipi akaagiza siku hiyo mle ndani kusafishwe na chini pang’ae kama kioo.(nadhani nao walikuwa na tiles zao za miaka ile) inasemekana alipokanyaga pale chini malkia wa sheba mfalme selemani aliona mguu wa malkia ulio chini kama wa mbuzi ukigeuka na kuwa wa kawaida mbele ya macho yake.akashangaa sana.

Malkia wa sheba akawa akimuuliza mfalme maswali mengi mengi sana na mafumbo ili kumpima hekima yake. Akamjibu kiasi cha kumridhisha kabisa na malkia akafurahia sana na baadaye akamfundisha kuhusiana na Mungu wake yeye Mfalme Seleman (Yahweh) na Malkia wa Sheba akawa muumini wake. Na hivi ndivyo Waethiopia wanaamini Jinsi ambavyo Ukristo uliingia nchini mwao yaani kupitia Malkia wa Sheba.

Malkia alikubali kuwa Mgeni wa Mfalme Seleman.na hapo alikuwa hajaolewa. Akamwonya mfalme seleman asimguse.(najua unaelewa maana ya asimguse). Na mfalme seleman akamwambia kama ni hivyo naye asichukue kitu chochote toka kwake. (toka zaman wanaume walikuwa hawatoi tu zawadi hivi hivi) na hapa mfalme alikuwa amemtega kiujanja kumbuka alikuwa na hekima sana. basi malkia akapewa chakula chnye spices nyingi sana(mfano ukila pilau matokeo yake unakunywa sana maji) Ulipofika usiku Malkia akasikia Kiu. Akachukua Glass ya Maji akanywa. Mfalme akamfuata na kumwambia amevunja makubaliano kuwa hakupaswa kuchukua kitu chochote toka kwake kwa kuwa yeye alisema asiguswe. Hivyo kwa kuahidi kuwa singechukua kitu chochote na mwishowe kunywa maji ya mle ndani amevunja ahadi na mfalme naye atavunja ya kwake ya kutokumgusa.

Basi hapo wakalala wote yaani wakafanya mapenzi na kumbuka mfalme alikuwa amemsubiria kwa hamu sana. Akamnanii….. na siku aliporudi nyumban kwake Malkia wa sheba alikuja kugundua ana ujauzito akamzaa Menelik na kumkuza yeye mwenyewe. Siku moja menelik akaamua kutembelea Israel kwenda kuonana na baba yake. Aliporudi alikuja na sanduku la agano lililokuwa limebeba amri kumi za Mungu alizotoa kwa Wayahudi. Hadith za kale zinasema kuwa sanduku liliendelea kuwa Ethiopia toka kipindi hicho na Waethiopia wana mwona Menelik kama ni Ufalme uliotukuka uliojipanua mpaka karne ya 20. Hii ndiyo hadithi ya Malkia wa sheba.
Hii simulizi yako inapatikana ktk kitabu gani cha hadithi,
Ambacho binadamu anakuwa na mguu Wa mbuzi harafu unabadilika unakuwa Wa binadamu kwa sekunde tu.
 
Hebu tuanze jambo la kwanza.
Fuvu lilikutwa Olduvai Gorge siyo la HOMO SAPIEN bali ni HOMO HABILIS ambaye alikuwa ni aina ya nyani.
Mimi siamini kama binadamu wa kwanza alikuwa ni nyani. Binadamu alikuwa ni banadamu tangu mwanzo.
Ukukubaliana na utafiti wa daktari Leakey ni dhahili kwamba unaamini binadamu ametokana na nyani.

Pili, umesoma wapi kwamba weusia wametokana na laana?
Nuhu alimlaani Canaan mtoto wa HAM na siyo HAM mwenyewe.
Kwa kukusaidia ukisoma kitabu cha MWANZO 9:25 "Nuhu akasema na alaaniwe Canaan;atakuwa mtumwa kabisa wa ndugu zake"
Canaan iko Mashariki ya kati na siyo Afrika, na walifutiliwa mbali na Waebrania wakiongozwa na Joshua sasa hiyo laana ya mtu mweusi imetoka wapi?

Tatu, baba wa watu weusi siyo Canaan aliyelaaniwa. Ham alikuwa na watoto wengine kama Cush, Mizraim na Phut.
Cush ndiyo baba wa Waethiopia, Mizraim ndiye baba wa Wamisri na Phut ndiye baba wa Walibya. Hata Ptolemy baba yake na Cleopatra aliandika kwamba Libya na ya uzao wa Phut. Wanahistoria wanakubaliana na hili kwanini wewe useme ni wongo halafu hutoi sababu za msingi?

Nne, kwa mtazamo wako kwamba biandamu alitokana na nyani utakuwa unakubaliana na theory of evolution. Hivyo mpaka sasa mzungu ndiye atakuwa binadamu Advanced kuliko watu weusi. Na kinachosikitisha ni unaamini kwamba wewe ulikuwa ni nyani.

Hebu dadavua kwanza haya halafu uje tuendelee kuelimishana. Karibu sana Mkuu.

big gift
Hakuna sehemu nimesema binadamu katokana na nyani.

Hilo fuvu la Dr. Leakey halikua la nyani. Acha kupotosha bana. Haikusaidii kitu.

Kuhusu huyo Nuhu kuwa chanzo cha hizo kabila bado hakuna utafiti unaoweka wazi hayo. Huyo Plotemy yeye aliandika historia na sio utafiti wa kisayansi.

Kama una chochote kinachothibitisha Nuhu kuwa chanzo cha waLibya. WaMisri na waEthiopia let's share. Sio masimulizi.
 
Safi kabisa kwa maneno mazuri. Ni miaka nenda tumeona nyani kibao lakini hakuna hata mmoja aliepatikana kukaribia na binadamu. so theory ya dr leakey ni ya uongo.
Ila binadamu ni binadamu tuu na tunabadilika kulingana na mazingira.
Theory ya evolution sio ya Dr. Leakey. Kama unajua tofauti nijuze.
 
Hii simulizi yako inapatikana ktk kitabu gani cha hadithi,
Ambacho binadamu anakuwa na mguu Wa mbuzi harafu unabadilika unakuwa Wa binadamu kwa sekunde tu.
Stori zingine ndo kama sungura alivyomwambia fisi miaka ile tunakua. Hiyo ya mguu wa mbuzi imeharibu stori yote.
 
Utumie lugha za kiungwana unapomzumngumzia suleiman ni nabii anayeheshimiwa na dini zote. Usitumie lugha za kumdhalilisha wala maneno ya kihuni kama kusex n.k
 
Hivi huyu Solomon alikua Nabii au tapeli? Maana haiwezekani zinaa iwe zambi ila yeye ndie hodari wa kuzini sasa alikua anawafundisha nini wafuasi wake afu mnatuambia alikua na hekima,hekima gani za kutafuna wageni alafu yeye mwenyewe ni mume wa mtu? Mi hawa manabii wa kwenye Biblia nawaona kama vibaka tu na kuiamini Bible inabidi akili yako iwe na walakini kidogo.
Hahahahaha, suala la amri kumi aliliinvent mzee mmoja hivi na kujidai amepewa na Mungu. Solomon alikuwa karibu sana na Mungu wake, na kujamiiana ilikuwa ni kiburudisho huru enzi hizo!
 
Hivi huyu Solomon alikua Nabii au tapeli? Maana haiwezekani zinaa iwe zambi ila yeye ndie hodari wa kuzini sasa alikua anawafundisha nini wafuasi wake afu mnatuambia alikua na hekima,hekima gani za kutafuna wageni alafu yeye mwenyewe ni mume wa mtu? Mi hawa manabii wa kwenye Biblia nawaona kama vibaka tu na kuiamini Bible inabidi akili yako iwe na walakini kidogo.
Alisema hayo n batili
 
Utumie lugha za kiungwana unapomzumngumzia suleiman ni nabii anayeheshimiwa na dini zote. Usitumie lugha za kumdhalilisha wala maneno ya kihuni kama kusex n.k
Hivi huyu Solomon alikua Nabii au tapeli? Maana haiwezekani zinaa iwe dhambi ila yeye ndie hodari wa kuzini sasa alikua anawafundisha nini wafuasi wake alafu mnatuambia alikua na hekima,hekima gani za kutafuna wageni alafu yeye mwenyewe ni mume wa mtu?
 
Jedediah ndiye mfalme Suleimani, linamaanisha MPENDWA WA MUNGU. Hili ndiyo jina halisi la mfalme Suleimani na alipewa na nabii Nathani mara baada tu ya kuzaliwa. Kwa maelezo zaidi soma 2 Samuel 12:25.
Haya turudi kwenye mada yetu, baada ya Malkia Mekeda kwenda kwa Mfalme Jedediah alimjaribu lakini akakuta Suleimani ana utajiri mkubwa wa kuisha na akili kumkichwa. Sasa wanahistoria wa Kiyahudi wanasema kwamba Mekeda akaambiwa na Suleimani alale kwenye kasri yake lakini akamuambia mfalme Suleimani kama ukitaka nilale Sharti usiniguse. Suleimani akamwambia sawa lakini na wewe usiguse kitu chochote cha ndani ndani ya nyumba yangu bila ruhusa yangu.

Suleimani alikuwa na mpango wake kichwani, akawaagiza watumwa wake waweke pilipili na viungo vingi kwenye chakula.
Makeda alivyokula usiku kiu kali ikamshika, basi akataka maji Suleimani akamjibu akasema tulikubaliana hutagusa chochote bila ridhaa yangu. Basi Makeda akazidiwa ujanja ndiyo maana akasema Suleimani ni Mfalme mwenye akili sana kuliko alivyowahi kusikia.

Aliondoka Yerusalem na mimba, akajifungua mtoto wake wa kiume akamuita jina MENELEKI 1 maana yake "SON OF THE WISE". Menelik alivyokuwa mkubwa alienda kuapishwa Yerusalem. Na mwanahistoria wa Kirumi Flavius Josephus anakuambia alikuwa Mfalme wa Ethiopia na Egypt, hapo alipewa jina la babu yake DAUDI. Sasa alivyorudi Ethiopia Mfalme Suleimani alituma kundi la Wasomi wa Kiyahudi zaidi ya 1000 na moja wapo walikuwa kuhani AZALIA na ZADOKI ambao kwenye biblia wapo. Hawa walitumwa kwa dhumuni la kumsaidia atawale ufalme wake vizuri.

Wayahudi wa Ethiopia wale wuesi wanaitwa Falahasha na siyo wote ni uzao wa Mfalme Suleimani. Wengine ni wayahudi kutoka kabila la dani ambalo walipotea baada ya kuvamiwa na Ashuru na Wakaldayo kutoka Babeli. Wayahudi weusi wako wengi sana na hichi watu wengi wanakipinga lakini ndiyo ukweli wenyewe. Lakini Wayahudi walianza kuoana na weusi tangu wako Misri na ushahidi mkubwa ni Abrahamu baba wa Wayahudi alizaa na kijakazi wake Hajira ambaye ndiyo mama wa Waarabu. Hajira alikuwa ni mtu wa Misri na Misri ilikuwa inatawaliwa na watu weusi kabla ya Waarabu. Sehemu ya Pili Nabii Musa alimuoa Zipora mtu wa Ethiopia. Ethiopia ilikuwa inatawaliwa na watu weusi hivyo kuwepo na Wayahudi weusi ni kitu cha kawaida sana.
HAO UNAOWAZUNGUMZIA WOTE NI WATU WEUSI. ....wazungu waongo sana
 
Back
Top Bottom