Malori yakwama bandarini Dar, madereva walalamikia ukiritimba na rushwa kurudi kama zamani

Malori yakwama bandarini Dar, madereva walalamikia ukiritimba na rushwa kurudi kama zamani

makusanyo yameshuka toka trillion 2 hadi billion 300 kwa mwezi, TRA wanadai kwa sasa matajiri ndo wanapanga kiasi cha kutoa na si kile wanachostahili kutoa, tunakoelekea mungu pekee ndo anajua
Unafanya biashara mkuu?
 
Naona coment zako nyingi zina jina la Magu[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] huku mada ni msongamano wa magari bandarini
Kaanze comment yangu ya kwanza labda utaelewa.
 
Huwezi kuwa na taasisi imara wakati una rasilimali watu yenye mapungufu makubwa kama yetu. Mnalilia taasisi imara kwa watanzania wapi mkuu, hawa wezi, wavivu, wasio wazalendo? Taasisi imara zinaletwa na raia waliokuzwa katika malezi bora.
Daa kweli mkuu malezi bora yanazaa jamii bora taifa bora
 
Kiukweli yapo mambo mengi Magufuli aliyaweka sawa sana. Bandarini palikaa sawa,japo sio kwa asilimia zote ila mambo mengi yaliwekwa sawa. Hivi sasa rush
wa imeanza kwa kasi hata kwa watu wa chini hawa waendesha mitambo ya kupakia. Soon tutashuhudia ule wizi wa kwenye makontena,kwenye magari yanayoingia unarudi kwa kasi.
"SIRI YA MTUNGI AIJUAYE NI KATA" ITS WAS JUST LIKE A SECRET MOVIE,MIFUKO YOTE YA JAMII ILIFILISIWA ILI KUNUNUA NDEGE NA KUJENGA UYAONAYO.....
#SASA HIVI NI LAZIMA MIFUKO HII IJAZWE FEDHA ILI WASTAAFU WASISUMBUKE TENA...underground publics works must be given priority.....
#Thatcher go on....!
 
Malori yakwama bandarini Dar yakisubiri kupakia na kupakua mizigo || Madereva wafunguka.​

Mkurugenzi wa Bandari na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Rasi Mamama Samia Hasssan Suluhu uwawajibishe kwa uzembe wanaofanya hao viongozi wawili.

Mwananchi online linaripoti kukwama kwa malori bandarini.

Je wapo wanaopima kina cha maji?

========

Mwananchi Digital imeripoti kuwa katika bandari ya Dar es Salaam kuna maroli (magari makubwa ya mizigo) yamekwama kwa siku kadhaa hivyo kusababisha madereva wa maroli kulala na kuamka hapo hadi kufikia siku nne, madereva hao wamedai kulala na kula kwenye magari yao na kuomba kujisadia katika vyoo vya ofisi za jirani kwa kuwa hapo bandarini hakuna vyoo.

Madereva hao wamedai chanzo cha uchelewashaji huo wa mizigo unatokana na ucheleweshwaji wa kupakua na kupakia mizigo na na ucheleweshwaji wa vibali vinavyoruhusu mizigo kusafirishwa.

Hata hivyo juhudi za kumpata mkurugenzi wa mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eriki Hamisi ziligonga mwamba baada ya kujibiwa kuwa yuko kikaoni na baadae simu yake ilipiwa bila kupokelewa. Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamriho aliahidi kumuunganisha mwandishi na watu wanaohusika jambo ambalo pia halikufanyika.

Dereva aeleza, "mimi toka nipo hapa siku ya nne ushushaji wa kopa bandarini ni mbovu ukimuuliza ajenti anakwambia gari zimejaa, mwenye mzigo anasema nimekodisha godauni natumia foko za bandari ukimwambia nilete foko zangu anasema hakuna sheria ya kuleta foko zako. Kwa hiyo bandarini ukiritimba umerudi kama zamani na rushwa imerudi. Tunaomba serikali iingilie kati swala hili madereva tunateseka bandarini kumeoza tunaomba msaada".

Very likely SSH anaweza akaingia kwenye rekodi kuwa RAIS MBAYA KULIKO WOTE hasa anapotegemea ushauri wa awamu wa 4. Dalili zilianzia pale anabadirisha mawaziri na watendaji "wewe nakuacha ukarekebishe". Hopeless kabisa no wonder thats why Kikwete is running the kantri.
 
Hatari sana. Kina kinapimwa.
Jenista ksema Majaliwa kishatia timu bandarini tayari, lazima kinuke. Kuna Watanzania bado wako usingizini pale bandarini, naona hajaamka na kuendana na mazingira mapya ya MAMA
 
LIVE: WAZIRI MKUU ASHTUKIZA BANDARINI Kujua CHANZO CHA MSONGAMANIO wa MALORI, TASAC WATAFUTWA!​

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, leo Mei 12, amefanya ziara ya kushtukiza bandari jijini Dar, kujionea kadhia iliyojitokeza na kusababisha malori kukwama.. Waziri Mkuu ameambatana na Mkuu wa mkoa wa Dar, Aboubakary Kunenge na mkuu wa wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe.

Iko hivi hii foleni sio ya leo Wala Jana, Ila kipindi kilichopita watu walikua wanaogopa kuhoji kwa kuwa Sasa Kuna Uhuru wa kuhoji ndio mana tunayasikia haya kukaa bandarini siku nne ni kawaida na sababu wanakuambia system haifanyi kazi. Wafanyakazi wanafanya Kama wanavojisikia ma operator mpaka uwape chochote mlinzi getini nae hela folio nao pesa ni upupu mtupu
Acha uongo we husikii dreva analalama??
 
Mwananchi online linaripoti kukwama kwa malori bandarini.

Je wapo wanaopima kina cha maji?

========

Mwananchi Digital imeripoti kuwa katika bandari ya Dar es Salaam kuna maroli (magari makubwa ya mizigo) yamekwama kwa siku kadhaa hivyo kusababisha madereva wa maroli kulala na kuamka hapo hadi kufikia siku nne, madereva hao wamedai kulala na kula kwenye magari yao na kuomba kujisadia katika vyoo vya ofisi za jirani kwa kuwa hapo bandarini hakuna vyoo.

Madereva hao wamedai chanzo cha uchelewashaji huo wa mizigo unatokana na ucheleweshwaji wa kupakua na kupakia mizigo na na ucheleweshwaji wa vibali vinavyoruhusu mizigo kusafirishwa.

Hata hivyo juhudi za kumpata mkurugenzi wa mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eriki Hamisi ziligonga mwamba baada ya kujibiwa kuwa yuko kikaoni na baadae simu yake ilipiwa bila kupokelewa. Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamriho aliahidi kumuunganisha mwandishi na watu wanaohusika jambo ambalo pia halikufanyika.

Dereva aeleza, "mimi toka nipo hapa siku ya nne ushushaji wa kopa bandarini ni mbovu ukimuuliza ajenti anakwambia gari zimejaa, mwenye mzigo anasema nimekodisha godauni natumia foko za bandari ukimwambia nilete foko zangu anasema hakuna sheria ya kuleta foko zako. Kwa hiyo bandarini ukiritimba umerudi kama zamani na rushwa imerudi. Tunaomba serikali iingilie kati swala hili madereva tunateseka bandarini kumeoza tunaomba msaada".

Nachukia sana Kiongozi dhaifu dhaifu, tunarudi kama enzi za Mr.Dhaifu wa Msoga
 
Utalaumu Watumishi unafikiri meli inapakuliwa kwa mikono? Mwulizeni Magufuli na Kakoko walioiba fedha zote za Bandari wakaiacha haina hata uwezo wa kununua wala kurepea mashine za kupakua na kupakilia mizigo; mnalaumu msiyoyajua...Samia atamwajibisha mfanyakazi asiyekuwa na vifaa vya kazi, na ambaye kwa miaka mitano amedhulumiwa haki zake?
Nawe una shida tu sisi tupo bandalin toka enzi za jk, magu na sasa suluu kipindi ambacho vifaa vimeongezeka kwa wingi bandarin ni kipindi cha Magufuli, upo tu unaongea ongea bila kujua unaongea nini
 
Nawe una shida tu sisi tupo bandalin toka enzi za jk, magu na sasa suluu kipindi ambacho vifaa vimeongezeka kwa wingi bandarin ni kipindi cha Magufuli, upo tu unaongea ongea bila kujua unaongea nini
Jamaa anaboa sana
 
JPM mlikuwa mnasema anatengeneza matatizo hili ayatatue, kamwambie SSH na yeye atatue haya matatizo anayotengeneza ili tuone kichwani yupo vizuri, sio kutuambia tu viongozi wake wanademka.
Tumpima na hizi data kama tulivomoima kikwete na JPM
images%20(2).jpg
JamiiForums355102718.jpg
 
Magufuli hakufanya lolote kuisaidia bandari iwe na Ufanisi...baada ya zile ziara zake za kufokafoka na kugombana na ambulance za Membe uliwahi tena kumwona akifika bandarini na fujo zake zile? Unafikiri kwanini hakufika? Jibu simple...tatizo lake lilikuwa wateule wa Kikwete, alipofanikiwa kuwaondoa akaweka wapiga dili wake wa Tanroads hakuwa na habari tena na bandari, akina Kakoko wakaota mapembe, wakafanya ufisadi wa kutisha kwa kushirikiana na Mamlaka ya Juu...ndo juzi mlikuwa mnashangilia ametumbuliwa kwa wizi mlifikiri aliiba baada ya Magufuli kufa? au mlikuwa mnashangilia kitu gani?
We nawe mnafki mkubwa kupitiliza mimi wakati wote naingia bandalin. Ukweli ni kwamba enzi za Magufuli bandari ilikuwa safi sana kila mfanyakazi wa bandar unamkuta katika kituo cha kazi na unahudumiwa kama vile uko stendi ya basi na ni muda ule hakuna wasafiri yaani mchana, lkn mambo yale ya zamani ya kucheleweshewa huduma, kutokuwa ktk kituo cha kaz yameanza baanda ya Mwendazake kwenda.
 
kuna watu wanataka hii nchi irudi nyuma kabisaa, tena ikae chini. viongozi kuweni makini sana.

baadhi yao ni wananfiki na wa lagjai nia yao iliyo jificha ni kuona anguko la awamu 6.
 
kwakweli inasikitisha sana tena sana.

Huu uzembe sio wa kuvumiliwa hata kidogo, haiwezekani baadhi ya kikundi cha watu wachache wanadiriki kuchezea uchumi wa nchi yetu.

nashindwa kuamini kama kweli tatizo ni mfumo wa malipo unao sababishwa na ukosefu wa umeme.

kuna tatizo la msingi
 
Sijui huyo dreva alikuwa na nia gani ? Watanzania mda mwingne tunakuwa wachawi wenyewe
 
Back
Top Bottom