Amri hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu kwa maelekezo ya Waziri wa Kilimo Bw. Bashe.
Bila shaka amri hii inatokana na zuio la Rais Samia kuzuia kuuza chakula nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa chakula nchini na duniani kwa jumla.
Hoja hapa kwa nini serikali haikuwataarifu wafanyabiashara mapema ili kuwaepusha na hasara watakayopata kwa sababu ya gharama za usafiri? Kwa nini malori yaliyofika hapo Himo kabla ya zuio la Rais yasiruhusiwe kuendelea na safari?
Moja ya athari ya zuio hili ni kuwa bei ya mahindi itaporomoka sana kwa wakulima kutoka zaidi ya Shs. 800/= kwa kilo kwa sasa hadi kuwa chini ya Shs. 500/= kwa kilo!