Malori zaidi ya 100 Himo yenye shehena ya mahindi yaamuriwa kuuza mahindi yao nchini badala ya kuyasafirisha Kenya

Malori zaidi ya 100 Himo yenye shehena ya mahindi yaamuriwa kuuza mahindi yao nchini badala ya kuyasafirisha Kenya

Hii issue lazima italeta mgogoro kati ya Kenya na Tanzania, sababu wafanya biashara wa Kenya tayari walikua wamesha nunua mahindi kwaajili ya kupeleka kwao kabla ya kauli ya bi mkubwa.
Nafikiri hapa ilitakiwa busara ya kawaida itumike ili kutatua hili jambo na baada ya hapi basi amri ya mama ndipo iendelee kutekelezwa.
Wakenya nao wana figisu nyingi sana kwenye hii biashara ya mahindi pamoja na kwamba wananunua kutoka kwetu lakini wanataka watanzania wapate hasara, ndio maana unaona wanazuia mara mzigo usiingie mara mahindi yana sumu mara hiki mara kile ni bora kabisa tufanye nao biashara nyingine hii ya nafaka tuachane nayo
 
Yaani tuache kufanya mambo yetu bila utaratibu na busara...Sasa Maagizo kutolewa bila kutoa muda wezeshi kuclear, kwa ambao tayari walikuwa na mizigo wa mahindi kuelekea mpakani.. hio sio fair jamani... yaani angalau wangetoa deadline ya siku kadhaa kabla ya kuwafungia mpaka.....
Upo sahihi kabisa mkuu.
Kimsingi Rais pia ni binadam, na yawezekana pia alighafilika kupata taarifa iliyo pelekea yeye kutoa tamko la katazo pale hadarani (ambayo ni sheria).
Sasa Bashe alipaswa aongee na mama ili kuwapa nafasi ambao tayari wamenunua mahindi waweze kuendelea, then hii ndio inaitwa hekima.
Naamini hekima ni pamoja na waziri kumsaidia Rais pengine kwa kumshauri, na sio kumpinga.
 
Amri hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu kwa maelekezo ya Waziri wa Kilimo Bw. Bashe.

Bila shaka amri hii inatokana na zuio la Rais Samia kuzuia kuuza chakula nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa chakula nchini na duniani kwa jumla.

Hoja hapa kwa nini serikali haikuwataarifu wafanyabiashara mapema ili kuwaepusha na hasara watakayopata kwa sababu ya gharama za usafiri? Kwa nini malori yaliyofika hapo Himo kabla ya zuio la Rais yasiruhusiwe kuendelea na safari?

Moja ya athari ya zuio hili ni kuwa bei ya mahindi itaporomoka sana kwa wakulima kutoka zaidi ya Shs. 800/= kwa kilo kwa sasa hadi kuwa chini ya Shs. 500/= kwa kilo!
Acha yazuiwe, kwanini mahindi yauzwe nje ya nchi wakati kuna uhaba wa chakula hapa nchini tayari.

Kama wanapata hasara inabidi Serikali iyanunue kwa hiyo bei wanayotaka wao ili tu yabaki TANZANIA
 
Wakenya nao wana figisu nyingi sana kwenye hii biashara ya mahindi pamoja na kwamba wananunua kutoka kwetu lakini wanataka watanzania wapate hasara, ndio maana unaona wanazuia mara mzigo usiingie mara mahindi yana sumu mara hiki mara kile ni bora kabisa tufanye nao biashara nyingine hii ya nafaka tuachane nayo

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
Nikweli kabisa mkuu, lakini bisahara haijawahi kua na fomular.
Biashara ni mbinu na ujanja, mkuu biashara inataka akili pasipo nguvu.
Anyway.......
Naona hapa kweli una hoja, lakini ebu tulitazame hili la tamko ama zuwio la ghafla kwanza limekaaje kwa wafanya biashara hao.
 
Nafikiri bashe alitakiwa atumie busara kwa kuruhusu wafanya biashara ambao tayari wamesha fikisha mahindi yao Himo waendelee na safari, kisha baada ya hapo ndipo wangeanza kuzuia wale wanao anza kunua mahindi kwaajili ya kupeleka Kenya baada ya tamko la mama. Na huku ndipo kumsaidia Rais
Ni kawaida Tawala nyingi hazifuati "principle za Management"matokeo Kila memba WA Ddmn na Menejementi ni sawa na Kambale ambao hawajavuliwa.@mmoja anawahi kutoa maelekezo akiamini,akiamini yatamnufaisha eye ,kama yeye na siyo taasisi.Hawafuati coordination"na Wala"chain of command s,Kwani hakukuwa na wakutoa maelekezo YASIYOBAD🙃LIKA
 
Amri hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu kwa maelekezo ya Waziri wa Kilimo Bw. Bashe.

Bila shaka amri hii inatokana na zuio la Rais Samia kuzuia kuuza chakula nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa chakula nchini na duniani kwa jumla.

Hoja hapa kwa nini serikali haikuwataarifu wafanyabiashara mapema ili kuwaepusha na hasara watakayopata kwa sababu ya gharama za usafiri? Kwa nini malori yaliyofika hapo Himo kabla ya zuio la Rais yasiruhusiwe kuendelea na safari?

Moja ya athari ya zuio hili ni kuwa bei ya mahindi itaporomoka sana kwa wakulima kutoka zaidi ya Shs. 800/= kwa kilo kwa sasa hadi kuwa chini ya Shs. 500/= kwa kilo!
Si walisema wakulima wasipangiwe... Akili zimeanza kuwarudia sasa.
 
Wakati tunashauri kwamba kwa kilimo hiki cha watz cha hand to mouth hakuna namna tunaweza kutosheleza mahitaji ya ndani bado tupate na ziada ya kuuza nje, Msomali akatujibu kwa kiburi sana kwamba kama haturidhiki na hali ya bei nchini kuwa kubwa na sisi tukalime. Leo yako wapi, msomali analazimika kula matapishi yake. Nisichokielewa ni je wanazuia mauzo nje kwa kuwa kila mkulima ameuza mazao nje na sasa kila mkulima kawa bilionea?
 
Hii issue lazima italeta mgogoro kati ya Kenya na Tanzania, sababu wafanya biashara wa Kenya tayari walikua wamesha nunua mahindi kwaajili ya kupeleka kwao kabla ya kauli ya bi mkubwa.
Nafikiri hapa ilitakiwa busara ya kawaida itumike ili kutatua hili jambo na baada ya hapi basi amri ya mama ndipo iendelee kutekelezwa.
Hatahivyo MH. Rais alitumia busara kubwa sana kuzuia chakula kuuzaa nje ya nchi na kuwataarifu wakulima wasiuze mzao, Kwa maana Mvua haikunyesha vizuri msimu huu na uzakishaji umekuwa mdogo sana. Yaani Hali ya chakula Kwa ujumla sio nzuri hapa nchini
 
Acha yazuiwe, kwanini mahindi yauzwe nje ya nchi wakati kuna uhaba wa chakula hapa nchini tayari.

Kama wanapata hasara inabidi Serikali iyanunue kwa hiyo bei wanayotaka wao ili tu yabaki TANZANIA
Serikali haina uwezo wa kununua mahindi yote ya wakulima. Mwaka huu itanunua tani 500,000 tu na hivyo kubakiza mzigo mwingi sana ambao utauzwa kwa bei ya chee ambayo haitamnufaisha mkulima..
 
Naamini lengo la serikali yetu ni zuri lakini why huwa execution ni kama dharula hivi, stakeholders wanakuwa caught by suprise bila kujali pesa na muda wa hawa wafanyabiashara.
 
Hasara kubwa Sana hii Kwa wafanyabiashara.
Hii biashara naijua jinsi ilivyokuwa ngumu kwenye kukusanya mzigo alafu anatokea MTU wa ofisini anasema hakuna kuuza nje ya nchi... Tanzania ni nchi ngumu Sana Kwa mfanyabiashara
Hii ilinitokea 2018 lile jiwe lilizuia mahindi kuuzwa nje halafu katika msimu mzuri wa soko likaruhusu mahindi kutoka Zambia yaingie nchini.

Zee la hovyo
 
Hasara kubwa Sana hii Kwa wafanyabiashara.
Hii biashara naijua jinsi ilivyokuwa ngumu kwenye kukusanya mzigo alafu anatokea MTU wa ofisini anasema hakuna kuuza nje ya nchi... Tanzania ni nchi ngumu Sana Kwa mfanyabiashara
Hayo mambo yanatokea duniani kote,national interest huwa ni kipaumbele namba 1 kuliko faida za watu wachache.
Ulisha wahi fikiria kuhusu wafanyabiashara wa Russia baada ya vikwazo vya uchumi vya west????
 
Mahindi hayapaswi kuzidi elfu 50 kwa gunia, mimi nalima na gharamaza za uzalishaji kwa gunia moja ni elfu 30 mpaka 35 ikizidi sana 40 sasa unakuja kuuza gunia laki hiyo si ni kumkufuru Mungu muumba mbingu na nchi?
 
Back
Top Bottom