Malori zaidi ya 100 Himo yenye shehena ya mahindi yaamuriwa kuuza mahindi yao nchini badala ya kuyasafirisha Kenya

Malori zaidi ya 100 Himo yenye shehena ya mahindi yaamuriwa kuuza mahindi yao nchini badala ya kuyasafirisha Kenya

Hasara kubwa Sana hii Kwa wafanyabiashara.
Hii biashara naijua jinsi ilivyokuwa ngumu kwenye kukusanya mzigo alafu anatokea MTU wa ofisini anasema hakuna kuuza nje ya nchi... Tanzania ni nchi ngumu Sana Kwa mfanyabiashara
Logistics za kukusanya Mahindi Vijijini ni mtihani mkubwa. Kuna wakati unatumia hata Boda kufikisha mzigo kwenye Lorry.
 
Bashe ni Msanii tu. Lumbesa ya Viazi imemshinda Wakulima wa zao hilo wananyonywa na Wafanyabiashara kama kawa.
 
Safi,naunga mkono zuio la kutoa chakula nje,ilihali ndani kuna uhitaji mkubwa.
Ifahamike kuwa,wanao export mazao nje ni wafanyabiashara 90%&wala si wakulima.
Bei ya mazao wanayonunua kwa wakulima ni pungufu,na inamnufaisha mkulima.
Serikali inazuia kutoa mazao nje ili kudhibiti upungufu wa chakula nchini.
 
Amri hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Nurdin Babu kwa maelekezo ya Waziri wa Kilimo Bw. Bashe.

Bila shaka amri hii inatokana na zuio la Rais Samia kuzuia kuuza chakula nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa chakula nchini na duniani kwa jumla.

Hoja hapa kwa nini serikali haikuwataarifu wafanyabiashara mapema ili kuwaepusha na hasara watakayopata kwa sababu ya gharama za usafiri? Kwa nini malori yaliyofika hapo Himo kabla ya zuio la Rais yasiruhusiwe kuendelea na safari?

Moja ya athari ya zuio hili ni kuwa bei ya mahindi itaporomoka sana kwa wakulima kutoka zaidi ya Shs. 800/= kwa kilo kwa sasa hadi kuwa chini ya Shs. 500/= kwa kilo!
Wakati wanapewa mbolea kwa sh 70,000/hili hawakulijua?
 
Hasara kubwa Sana hii Kwa wafanyabiashara.
Hii biashara naijua jinsi ilivyokuwa ngumu kwenye kukusanya mzigo alafu anatokea MTU wa ofisini anasema hakuna kuuza nje ya nchi... Tanzania ni nchi ngumu Sana Kwa mfanyabiashara
Tz wasemaji wengi kila mtu hanasema lake
 
Back
Top Bottom