Mama aliniambia baba aliyenilea kwa miaka 25 si wangu baada ya kifo chake, lakini daima nitakukumbuka baba uliyenilea kuzidi aliyerusha mbegu

Mama aliniambia baba aliyenilea kwa miaka 25 si wangu baada ya kifo chake, lakini daima nitakukumbuka baba uliyenilea kuzidi aliyerusha mbegu

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Baba niliemjua ni baba yangu mzazi ambae nae alijua mimi ni mtoto wake alinilea kwa mapenzi yote, kunifundisha vingi katika maisha, kunisomesha shule mpaka chuo kikuu, kunivisha, kunilisha, n.k. Kwa miaka 25, hata nilipoanza kujitegemea bado nahesabia kuna majukumu yake kama baba yaliendelea kwenye malezi ikiwemo kunipa ushauri, kunijulia hali, n.k.

Baba wa kibailojia nilikuja kumjua baada ya msiba wa baba, ila kumjua namjua haikuwa sura ngeni maana kuna kipindi hasa utotoni mama alikuwa anaomba nimsindikize sehemu ila tunapitia kwa bwana huyo ni mbali kidogo kama kilometa 3 hivi alikuwa anapenda kuninunulia vyakula na kunipa vitoy lakini hivi vya kurudi navyo mama alikuwa anavipeleka sijui wapi maana nilikuwa sivioni, hata sekondari mara kadhaa ashawahi kunipa pesa ila nikimuuliza we nani anabaki tu kusema nimuite uncle, kiukweli ni kama alikuwa anatumia nguvu kubwa kujenga ukaribu ambao kwangu ulishindikana, si mnajua tena kuna watu hata ukilazimisha urafiki huwa haiwezakani, basi tu nilikuwa namvumilia maana ni mtu mzima.

Baada ya mzee kutoweka nae mama alianza kuumwa sana, alikuwa ni mtu wa mawazo sana, stress kibao, ndipo kuna siku aliniita na mda huo tayari nishaanza maisha ya kujitegemea, ndio bimkubwa akanipa hio siri kwamba yule mbaba ni baba yangu, alinisihi sana nisiwaambie wengine, kwa utu uzima niliokuwa nao wa kuyaona mengi wala haikuwa pigo zito sana maana nilishatambua baba ni yule alienilea na haitakuwa kivingine,

Kinachoniuma ni kwamba huwa naona mama alimfanyia unyama baba alienilea, lakini siwezi jua labda pengine nae mzee alikua anajua na huenda kuna siku angeniambia ila akawahi kuondoka ama aliamua kuifagilia ishu hii chini ya kapeti, ila yote kwa yote nilizaliwa kipindi ambacho tayari wamo kwenye ndoa, mzee alienilea alinitambulisha kwa ndugu zake wengi na nina ukaribu nao kina baba mkubwa, baba mdogo na mashangazi.

Napata mashaka zaidi kama walionitangulia na niliemtangulia kama ni watoto wa baba alienilea ama wa mwengine.
 
Baba nilemjua ni baba yangu mzazi ambae nae alijua mimi ni mtoto wake alinilea kwa mapenzi yote, kunifundisha vingi katika maisha , kunisomesha shule mpaka chuo kikuu, kunivisha, kunilisha, n.k. Kwa miaka 25, hata nilipoanza kujitegemea bado nahesabia kuna majukumu yake kama baba yaliendelea ikiwemo ushauri.

Ni baada ya kifo chake ndipo mama akaniambia ukweli.

Baba wa kibailojia nilikuja kumjua baada ya msiba wa baba, kusema kweli hata hatujazoeana hata kidogo ila namjua tu, kiufupi hata hatuna cha kujadiliana,

Napata mashaka zaidi kama walionitangulia na niliemtangulia kama ni watoto wa baba alienilea ama wa mwengine.

Lakini huwa nawaza sana huwa nahisi mama alimfanyia unyama baba alienilea.
Duh...inatia uchungu.
 
Mheshimu tu lakini huyo aliyerusha mbegu ndio babaako halisi.

Kwa kifupi wewe ni Jiwe la kwenye manati, na manati yenyewe ni babaako aliyekurusha kwenye tumbo la mamaako.
Waheshimu wote tafadhali... Huyo mlezi alikulea kwa sababu ya utamu wa mbususu ya mama
 
Baba nilemjua ni baba yangu mzazi ambae nae alijua mimi ni mtoto wake alinilea kwa mapenzi yote, kunifundisha vingi katika maisha , kunisomesha shule mpaka chuo kikuu, kunivisha, kunilisha, n.k. Kwa miaka 25, hata nilipoanza kujitegemea bado nahesabia kuna majukumu yake kama baba yaliendelea ikiwemo ushauri.

Ni baada ya kifo chake ndipo mama akaniambia ukweli.

Baba wa kibailojia nilikuja kumjua baada ya msiba wa baba, kusema kweli hata hatujazoeana hata kidogo ila namjua tu, kiufupi hata hatuna cha kujadiliana,

Napata mashaka zaidi kama walionitangulia na niliemtangulia kama ni watoto wa baba alienilea ama wa mwengine.

Lakini huwa nawaza sana huwa nahisi mama alimfanyia unyama baba alienilea.
Km unayoyasema ni ya kweli, basi huyo mamako ni shetani. Kuna sababu gani ya kukueleza hayo zaidi ya kukuharibu kisaikolojia? Km Anataka kumrudia huyo anayeitwa babako wa kibailojia si akafanye bila kukueleza huo ushetani?
 
Back
Top Bottom