Mama aliyedaiwa kufanya ukatili na video yake kusambaa mitandaoni akimpiga mtoto akamatwa

Unafiki tu wa watu, labda kuwe na video nyingine au mkasa mwingine haujawekwa wazi.
Mtoto unampiga ngumi na mateke halafu unaona sawa tu! Tuchukulie ni mwanao yupo kwa mkeo mdogo ama kwa ndg yako yeyote uingie gafla ukute ananyukwa mangumi. Wewe unaangalia ngumi zinapanda na kushuka ushapiga hesabu ya force ya hizo ngumi?? Huna mtoto wewe hata kama unae basi humpendi na kumthamini kivile
 
Niliona original post sikufungua kwasababu sipendi kuangalia ukatili. Ila leo nimesema ngoja nione. Hii video ndio yote au kuna kipigo kimefichwa? Hebu tuache utani. Huyo dogo ni bingwa wa kupiga yowe tu hakuna kipigo hapo. Au sio mama yake? Kama ni mtoto wa mwingine labda ila mwanae hio adhabu ya kawaida sana.
 
Duuuh labda kama kuna video nyingine. Ila hicho kipigo mbona cha kawaida saana hata police kutolea tamko.
 
Reactions: I M
Hcho ndo kipigo chote ama Kuna chengine hakijaoneshwa mana hcho naona Cha kawaida , hajampiga kichwani Wala kumtoa damu
Sawa, wewe umewahi kupigwa kichwani ? Kama hakumpiga kichwani na kumtoa damu hiyo inahalalisha kipigo sehemu zingine za mwili ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ