Angel Nylon
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 9,164
- 18,402
NakaziaNi ujinga tu kupiga watoto. Ninao wanne wa kwanza 18 wa mwisho 11 sijawahi wapiga hata siku moja na wote wana tabia njema. Tena mitoto inayo pigwa pigwa ndio inakua minunda na katili.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NakaziaNi ujinga tu kupiga watoto. Ninao wanne wa kwanza 18 wa mwisho 11 sijawahi wapiga hata siku moja na wote wana tabia njema. Tena mitoto inayo pigwa pigwa ndio inakua minunda na katili.
Hapana, sina rekodi yakupigwa kama mwizi mkuu.Wewe mbona kipigo kilikusaidia? Watoto wasiosikia mara moja moja unamtandika. Mbona wengi wananyooka tu.
Mwenyewe nashangaa. Labda kuna part twoHcho ndo kipigo chote ama Kuna chengine hakijaoneshwa mana hcho naona Cha kawaida , hajampiga kichwani Wala kumtoa damu
Hicho ndo kipigo au Kuna part two?Utawaweza baba na mama junior? Ndio hao wanaona huyo mtoto kapigwa sana yaani angeweza kufa.
Mama junior uko poa?Hicho ndo kipigo au Kuna part two?
Yaani Niko poa.na.kajunior kangu sogea uone weeMama junior uko poa?
Huyu mchukua video kwanini asitete huyo mtoto?Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Sabrina Shabani, mwenye umri wa miaka 28, mkazi wa Mbezi Mwisho, baada ya video kusambaa mitandaoni ikimuonesha akimshambulia mtoto mdogo. Tukio hilo limeibua masikitiko na hasira kwa umma, na uchunguzi wa awali ulifanywa kwa kushirikiana na Idara ya Ustawi wa Jamii.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara tu uchunguzi utakapokamilika. Jeshi la Polisi limewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya ukatili, likionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahalifu.
Taarifa ya Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linapenda kutoa taarifa kuhusiana na tukio la picha mjongeo (video) zilizoonekana kwenye mitandao ya kijamii zikionesha mwanamke mmoja akimshambulia mtoto mdogo kwenye eneo la makazi. Vitendo hivyo havikubaliki na kwa hali hiyo upelelezi wa awali ulifanyika kwa kushirikiana na idara ya ustawi wa jamii na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Sabrina Shabani miaka 28 mkazi wa Mbezi mwisho Ubungo Dar es Salaam.
Pia, Soma:
+ Waziri Gwajima kukomesha ukatili baada ya video ya Mama akimshambulia mtoto kusambaa
+ House girl aliyemkata shingo mtoto wa mwajiri wake akamatwa na polisi
+ Kemeo la ukatili dhidi ya mtoto Malik Hashim Kitumbi
+ TLS Yalaani Vikali Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia wa Binti kutoka Yombo Dovya, Dar es Salaam
Wazazi wa siku hizi tumekuwa nyoronyoro sana! Biblia yenyewe inatuagiza tuwatandike sasa huyo kuguswa tu yamekuwa makelele! Mh. Gwajima mwachie huyo mama akaendelea na shughuli zake!Mtoto hufundishwa akiwa mdogo, utii, nidhamu na uwajibikaji hayaji tu hivi hivi. Awe mama yake au sio mama yake mzazi binafsi sijaona ukatili hapo. Tena kampiga vibao vinne tu kama sijakosea.
Kwa malezi ya online, no wonder watoto wanatukana wazazi wao mitandaoni huko, watoto hawali mpaka uwawekee cortoon zao pendwa, watoto wawatuma hadi dada wa kazi 😂😂
Nadhani hii ndio point ila huyu mama yeye anajipigia tuu randomly nadhani mtoto anatakiwa kuelekezwa. Sijawaelewa watu wanaosema kapigwa kidogoHapana, sina rekodi yakupogwa kama mwizi mkuu.
Sisi tulichapwa sio kupigw kama jambazi.
Tulikuwa tukikosea saana, mzazi anakuita anakuonya na anakwambia ukakate fimbo nikuchape ili ukitaka kukosea tena ukumbuke hiki kiboko.
Unachapwa kwa staha na utaratibu
Ni ujinga.Nadhani hii ndio point ila huyu mama yeye anajipigia tuu randomly nadhani mtoto anatakiwa kuelekezwa. Sijawaelewa watu wanaosema kapigwa kidogo