Mama aliyedaiwa kufanya ukatili na video yake kusambaa mitandaoni akimpiga mtoto akamatwa

Mama aliyedaiwa kufanya ukatili na video yake kusambaa mitandaoni akimpiga mtoto akamatwa

Wewe mbona kipigo kilikusaidia? Watoto wasiosikia mara moja moja unamtandika. Mbona wengi wananyooka tu.
Hapana, sina rekodi yakupigwa kama mwizi mkuu.
Sisi tulichapwa sio kupigwa kama jambazi.
Tulikuwa tukikosea saana, mzazi anakuita anakuonya na anakwambia ukakate fimbo nikuchape ili ukitaka kukosea tena ukumbuke hiki kiboko.

Unachapwa kwa staha na utaratibu
 
Ndio Matukio ambayo kitengo Cha polisi Cha intelligenjensia huwa kinajipatia maujiko.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Sabrina Shabani, mwenye umri wa miaka 28, mkazi wa Mbezi Mwisho, baada ya video kusambaa mitandaoni ikimuonesha akimshambulia mtoto mdogo. Tukio hilo limeibua masikitiko na hasira kwa umma, na uchunguzi wa awali ulifanywa kwa kushirikiana na Idara ya Ustawi wa Jamii.

Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara tu uchunguzi utakapokamilika. Jeshi la Polisi limewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya ukatili, likionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahalifu.
Taarifa ya Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linapenda kutoa taarifa kuhusiana na tukio la picha mjongeo (video) zilizoonekana kwenye mitandao ya kijamii zikionesha mwanamke mmoja akimshambulia mtoto mdogo kwenye eneo la makazi. Vitendo hivyo havikubaliki na kwa hali hiyo upelelezi wa awali ulifanyika kwa kushirikiana na idara ya ustawi wa jamii na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Sabrina Shabani miaka 28 mkazi wa Mbezi mwisho Ubungo Dar es Salaam.
Pia, Soma:
+
Waziri Gwajima kukomesha ukatili baada ya video ya Mama akimshambulia mtoto kusambaa
+ House girl aliyemkata shingo mtoto wa mwajiri wake akamatwa na polisi
+ Kemeo la ukatili dhidi ya mtoto Malik Hashim Kitumbi
+ TLS Yalaani Vikali Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia wa Binti kutoka Yombo Dovya, Dar es Salaam
Huyu mchukua video kwanini asitete huyo mtoto?
 
Mtoto hufundishwa akiwa mdogo, utii, nidhamu na uwajibikaji hayaji tu hivi hivi. Awe mama yake au sio mama yake mzazi binafsi sijaona ukatili hapo. Tena kampiga vibao vinne tu kama sijakosea.

Kwa malezi ya online, no wonder watoto wanatukana wazazi wao mitandaoni huko, watoto hawali mpaka uwawekee cortoon zao pendwa, watoto wawatuma hadi dada wa kazi 😂😂
Wazazi wa siku hizi tumekuwa nyoronyoro sana! Biblia yenyewe inatuagiza tuwatandike sasa huyo kuguswa tu yamekuwa makelele! Mh. Gwajima mwachie huyo mama akaendelea na shughuli zake!
Screenshot_20241023-191450_Biblia.jpg
 
  • Nzuri
Reactions: I M
Hapana, sina rekodi yakupogwa kama mwizi mkuu.
Sisi tulichapwa sio kupigw kama jambazi.
Tulikuwa tukikosea saana, mzazi anakuita anakuonya na anakwambia ukakate fimbo nikuchape ili ukitaka kukosea tena ukumbuke hiki kiboko.

Unachapwa kwa staha na utaratibu
Nadhani hii ndio point ila huyu mama yeye anajipigia tuu randomly nadhani mtoto anatakiwa kuelekezwa. Sijawaelewa watu wanaosema kapigwa kidogo
 
Nadhani hii ndio point ila huyu mama yeye anajipigia tuu randomly nadhani mtoto anatakiwa kuelekezwa. Sijawaelewa watu wanaosema kapigwa kidogo
Ni ujinga.
Ndio maana watanzania wengi ni makondoo kwa vile wamelelewa kama wanyama.
Mimi ni mlezi bora sana, naelekeza, naonya kwa upole na ukali inapobidi...fimbo ni hatua ya mwisho tena fimbo ya staha na utu.

Huyu mwanamke angekuwa mke wangu yaani ilikuwa ndio kwaheri.

Unapiga mtoto kama kibaka?
 
Back
Top Bottom