Mama aliyedaiwa kufanya ukatili na video yake kusambaa mitandaoni akimpiga mtoto akamatwa

Sio mwanae ni mtoto wake wa kambo mama yake alitofautiana na babaye kitambo
 
Huyu Mama kwa bahati mbaya camera imemnasa lakini haya ni mambo yanatokea kila siku kila mitaa na mabaya zaidi ya haya. Siungi mkono kumpiga mtoto kama unapiga mtu mkubwa ziko njia za kumuadhibu mtoto. Mimi sipigi mtoto lakini naogopwa nikimpiga jicho tu atakuja mwenyewe kuomba msamaha anajuwa hapa nimekosa. Sasa sio watoto wote sawa.

Huyu Mama utampa adhabu gani? labda yeye ndio mzazi bora kwa huyo mtoto na ukimfunga huyo mtoto ndio wa kwanza atamlilia Mama yake kwa uchungu, sio kila jambo kuchukulia kisiasa tu na kukaa na mzazi kumpa somo ajue njia sahihi za kumpa adhabu mtoto sio kumpeleka polisi ili iweje? afungwe? alipe fine, mazingira ya nyumbani tu unaona watu mradi kumekucha. Hawa kina Mama wana stress nyingi, hapo labda analea mtoto mdogo, huyu anamsumbua baba haeleweki kama yupo au single mama. Maisha haya yanachangamoto sana, sitaki watoto wapigwe kama watu wazima lakini pia kina Mama wengi wanapitia stress nyingi sana zinazoletwa na sisi wanaume. Hasira za mume zinaishia kwa mtoto.
 
hivi huyu mchukua video alikuwa wapi muda huo. If I may ask!
 
Wananchi walipaza sauti Heko kwao...viongozi waliochukua hatua...ndio kazi yao...mwezi huu wanakula mshahara kutoka kwaa wananchi walipa kodi kihalali.
Hongera sana waziri Gwajima na jeshi la polisi
 
Yeye anafundsha practical halafu yeye akikosea wamfundshe kwa theory??
Utawafunga wangapi. Shida ni hatuna elimu ya kifamilia, ukoo, jando jinsi ya kukuza watoto.

Kumbuka kwa miaka zaidi ya 3000 tulikuwa na system ndio maana upo unaandika hapa. Hizo systems zimeenda wapi? Angeweza kuita mjomba, Babu, jirani enzi zile. Sasa hivi yuko peke yake. Inanidi afanye ananyojua.
 
Huyu dada anatakiwa awe chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii, anapokamatwa na kuwekwa mahabusu anayeathirika
zaidi ni mtoto, hata baada ya kupigwa mtoto hakuonfoka hapo nyumbani kwani hakuwa na mahali pa kwenda.
 
Kwa hiyo unaona ni sawa mtu mzima kumpiga mtoto mateke kwani hakuna njia nyingine ya kumpa punishment.
 
Mie niko nashangaa eti...
 
Reactions: I M
Afande Muliro anaposema kitendo hicho hakikubaliki..... hakikubaliki na nani ????

Tunataka maafande wanasheria!
 
Hcho ndo kipigo chote ama Kuna chengine hakijaoneshwa mana hcho naona Cha kawaida , hajampiga kichwani Wala kumtoa damu
Ila watoto wa siku hizi tunawadekeza sana! Hicho hakiwezi kuitwa kipigo au kumshambulia mtoto. Ni cha kawaida sana kwa mtoto mtovu wa nidhamu. Kama huwa anampiga kila siku hiyo ni habari nyingine lakini kama ni pale anapokosea, ni kawaida sana!
 
Kuna ngumi hapo kweli? Huu sasa ni uchochezi. Mbona naona kama alikuwa anatumia kiganja kumpiga matakoni? Kitu ambacho ni kawaida sana na mama huyo amekuwa mwangalifu hajampiga makofi kichwani! Jamani watu tumepigwa ati! Hicho cha kawaida mno ukilinganisha na enzi zile!
 
Reactions: I M
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…