Mama amshauri mwanaye kuacha kazi kisa ndoa

Hayo ni maoni yako mkuu. Mfano uliotoa hausadifu hiki ninachokisema hapa. Kuacha kazi kisa mume ni uwendawazimu. Cha ajabu huyo mume unayekaa naye bega kwa bega akiamua kuchepuka, lazima atachepuka tu. Kukaa pamoja sio ulinzi sahihi kwa mume kwani mume hulindwa na Mungu, sio mke.
 
DUh mwanaume kuwa mbeya hivi haipendezi aisee , ila una hoja usikilizwe
 
kila mtu ana vipaumbele vyake. Na kwa afya ya familia na ndoa ni vyema wanandoa waishi pamoja
Please compare the cost of losing the job and the benefit of staying together with wife/husband. These are two incomparable entities. Dont compare thresh (marriage) with treasure (employment).
 
Mkuu usitetee jambo la ovyo kama hili. Hebu muonee huruma mwenzako. Sasa hivi anajuta kusikiliza maoni ya mama yake. Anatamani walau apate mtu amuajiri kama dada wa kazi, lakini wapi!
Jamaa anatakiwa atafute mtaji wafanye biashara
 
Mkuu ni wewe ndio umeambiwa uache kazi? Yeye mwenye mume kaona sawa, mama yake mzazi aliyemzaa na kumsomesha CPA kaona sawa wewe ambaye huusiki hata robo eti unakereka. Wewe ndio mwenye matatizo

Baada ya kuacha kazi wamekuja kukuomba hela ya kula?

Tuliza munkari we jamaa. Waache watu na maisha yao na mambo yao. Eti kaacha kazi kafata mbunye, ndio mawazo yako yameenda huko? Kama wewe unachukulia light mambo ya ndoa kuna wenzio wanachukulia serious. Nyie wenyewe kila siku mnasema hakunaga distance relationship sasa mtu akimfata mwenzie pia ni nongwa.

We jomba hebu jali mambo yako itakuzidishia afya
 
Wewe umejuaje yote haya ndugu yangu? Ila Mkuu kuna watu ajira na fedha sio vipaumbele vyao wala tusiwashangae na kuwalaumu.
Huyu ni ndugu yangu wa karibu. Niliposikia kuwa ameacha kazi kwa ushauri wa mamaye na nikitazama maisha anayoishi sasa namsikitikia sana
 
Umaskini na uoga wa maisha ndio unaweza kumfany mtu akashangaa ila n kawaida tu.

On my side nkishakuwa kikaz mkoa mwingine na mpenz yupo kwingne hapo huwa simpi attention yangu kama hapo awali sababu hata kucheatiwa n dk 0 tu huwenda Mama mtu kaliona hilo na hana njaa ya pesa.
 



We haujakomaa bado kuweza kudadavua mambo kwa kina.

Unawaza mambo negative kuwa ukiacha Kazi serikalini utakufa au maisha kuwa magumu .

Je haujiulizi kabla ya kupata Kazi serikalini alikuwa anaishi vipi.
 
Kama familia yote inajiweza kwanini asiache kazi na kumfuata mumewe?.

Umasikini ndio chanzo wanawake kuwa watafutaji.
Hii ndio fwact yenyewe....mwanamke ni pambo inabidi atulie nyumbani kidume uchakarike.
Haya mambo ya kuoa mke yupo mwanza mume dodoma ni kudanganyana tuu hapo everybody will cheat its a matter of time tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…