Mama ana rafiki yake ambaye ni mganga wa jadi sasa ndiye anayetoa maaumuzi ya kila kitu

Mama ana rafiki yake ambaye ni mganga wa jadi sasa ndiye anayetoa maaumuzi ya kila kitu

Kwa sasa kiongoz ni mimi bandage mzee kufariki,

Kuhusu kipato nina namshukuru Mungu familia inapata mahitaji ya msingi

Wadogo zangu wawili wakike waolewa mmoja yuko chuo kikuu arusha anamaliza mwezi ujao na mmoja yuko anajihusisha na kazi za ukopesha kwenye microfinance hizi za mtaani

Mama alikuwa na kazi ya kuuza kuni ila mpaka mtaji uliisha,so anapotumiwa hela anagawanya
Okay .


Nadhani ikiwa wewe ndo kiongozi wa Familia .

Jaribu kuongea nae kirafiki na Umwambie kuhusu hilo swala .
Akigoma na kuendelea kumpatia hela Mganga.

Basi unabidi kuwa mnampatia Matumizi na kumlipia bills Zane zote pasipokumpatia hela.

Na ikiwa mtapatia hela basi iwe katika Cashless .

Mfano umeme ukiisha unanunua then unamtumia.

Bills ya Maji unalipia .

Matibabu unamkatia Bima ya Afya .

Kila kitu unakiweka katika huo Mfumo then akitaka hela unamuuliza unataka Kununua nini then unamuambia nenda dukani agiza unachotaka then unalipia.



Tumia huo utaratibu akikosa hela ya kumpatia huyo Mganga lazima atapunguza Mazoea nae na mwisho urafiki utakufa.
 
Kuwa mtulivu kijana, fanya mambo yako ya msingi, isaidie familia yako na ndugu zako kwa kiasi kilicho ndani ya uwezo wako. Kamwe usijaribu kumbadilisha tabia au mwenendo mama yako mzazi sababu hutaweza na utaishia kugombana naye tu.
Jitahidi na fanya bidii uchumi wako uwe sawa na mambo mengine yote yatakuja kuwa sawa bila kutumia nguvu. Puuzia mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako kuyabadilisha ili kulinda furaha na amani ya moyo wako. Mimi ningekuwa wewe ningejifanya kama sijui kuhusu hizo habari za mama na ningeacha kumfuatilia na kuziongelea.
 
Sasa inapotokea anahitaji msaada wa mahitaji nini tufanye
Pambaneni mumpe mahitaji hakuna namna nyingine ila msiache kumshauri na ana hiyari ya kupokea au kukataa kutekeleza ushauri wenu
 
Okay .


Nadhani ikiwa wewe ndo kiongozi wa Familia .

Jaribu kuongea nae kirafiki na Umwambie kuhusu hilo swala .
Akigoma na kuendelea kumpatia hela Mganga.

Basi unabidi kuwa mnampatia Matumizi na kumlipia bills Zane zote pasipokumpatia hela.

Na ikiwa mtapatia hela basi iwe katika Cashless .

Mfano umeme ukiisha unanunua then unamtumia.

Bills ya Maji unalipia .

Matibabu unamkatia Bima ya Afya .

Kila kitu unakiweka katika huo Mfumo then akitaka hela unamuuliza unataka Kununua nini then unamuambia nenda dukani agiza unachotaka then unalipia.



Tumia huo utaratibu akikosa hela ya kumpatia huyo Mganga lazima atapunguza Mazoea nae na mwisho urafiki utakufa.
Yes, no cash
 
Kuna mambo ya wazazi huumiza sana watoto kiasi hata cha kupunguza ile bond na mzazi.....pole sana mkuu.
 
Nisaidie namba ya mganga huyo Nina shida nae anaweza kuwa mshangazi wangu
 
Habari wadau, poleni na majukumu ya siku, kama kichwa cha mada kinavyosema mimi ni kijana wa miaka 31, na ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kati ya watoto sita. Baba alifariki miaka 7 iliyopita tumebaki mama,
Nimekuja mbele zenu waungwana nipate mawazo nitoke katika mtanziko huu.

Mama ana rafiki yake ambaye ni mganga wa jadi sasa mama ni haelewi familia tena, huyo rafiki amekuwa ni scheme ya maamuzi ya familia mpaka tunapitia wakati mgumu lakini mama kila apato pesa inatumwa kwa rafiki yake . Waungwana nawezaje kutoka katika hill maana nimeelewa na msongo wa mawazo.

Asanteh
Kwa hilo unaogopa kuzinguana na bimdashi?

Block connection zote na huyo mganga pia mfuate huyo mganga mpe vitisho vya maana tena nenda na panga ikiwezekana mchape hata ubapa mmoja.

Mwambie ole wake uone akimtafuta tena bimkubwa wako kua ukijua tu na yeye itakua alazwe mahala pema peponi halafu kabla ya kuondoka mchape ubapa mwingine wa kwaheri.

Usisahau kumwambia hunitishi na uchafu wako huu vuruga vitu vyake pale atakuogopa milele tena wewe na familia yako.
 
Unajua waganga ni wapumbavu Sana Mkuu .

Kuna Mama mmoja alifia kwa Mganga nilisikitika Sana kiukweli.

Yaani usipokuwa makini hata mama yako akiumwa Typhoid atakimbilia kwa Mganga.
 
Tatizo mdogo wangu umejipa uongozi wa familia ya baba yako wakati mama yako yuko hai. Hapo kiongozi ni mama yako... usijione baba kwenye familia isiyo yako. Naunga mkono hoja ya ndugu Adverse Effect kuwa jikite kwenye mambo yako. Kumbadilisha mama yako ni suala gumu ambalo lina risk kubwa.
 
Waganga wa kienyeji si watu wazuri, usiruhusu mganga wa kienyeji awe mshauri wa familia yenu, mtaharibikiwa.
KUna ndugu yetu mmoja alikuwa anaumwa, hali ilivyozidi kuwa mbaya mkewe na wanae wakamuita mganga wa tiba ya kienyeji. Baada ya mganga kuja ulizuka ugomvi usio na kichwa wala makalio. Zikaanza tuhuma za hovyo, mara fulani mchawi, mara yule mchawi.

Mwisho wa siku yule ndugu akafariki, amefariki huku nyuma familia yake haielewani na ndugu zake. Cha kusikitisha ile familia imekuja msibani na yule mganga mshenzi mshenzi. Tukiwa makaburini nikawa namuona anavyofanya mambo yake kwa kujificha jificha, nilitamani niwe na bastola nimlipue pale pale, maana mambo yake ya kijinga yamesababisha ndugu kugombana na kununiana kwa tuhuma za kufikirika.
 
Kama unamjua huyo mganga, mtokee na panga usiku usiku na mikwala mingi kuwa ukisikia tena amevuta hela unakula nae shani moja....
Atamwambia Mama mtu, kuwa Mwanao kaja hapa na Mapanga.

Watapanga this time around Mama awe anatumia pesa Kwa Siri....!

1. Wajinga/Washamba
2. Tamaa.
3. Waoga(Dhaifu)
Ndiyo hutapeliwa..... Huna kimoja wapo, huwezi kutapeliwa.
 
Mmeshqjua mama akipewa hela anapeleka kwa mganga.

Hapo ni nyie woote kukaa kikao na kuja na kauli moja. Hakuna kutoa hela kwa yeyote kati yenu.

Akimchek mmoja kati yenu akisema hana mboga, mnampelekea fungu la matembele tuone kama atapeleka tembele kwa shoga yake mganga
 
Kuwa mtulivu kijana, fanya mambo yako ya msingi, isaidie familia yako na ndugu zako kwa kiasi kilicho ndani ya uwezo wako. Kamwe usijaribu kumbadilisha tabia au mwenendo mama yako mzazi sababu hutaweza na utaishia kugombana naye tu.
Jitahidi na fanya bidii uchumi wako uwe sawa na mambo mengine yote yatakuja kuwa sawa bila kutumia nguvu. Puuzia mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako kuyabadilisha ili kulinda furaha na amani ya moyo wako. Mimi ningekuwa wewe ningejifanya kama sijui kuhusu hizo habari za mama na ningeacha kumfuatilia na kuziongelea.
Mkuu hayo mambo tunapitia wengi, ila huu ushaur ni mzur, as long as hainikwamishi kwenye mambo yangu na aliweza kunisomesha bas naona wafu wawazike wafu wenzao.
 
Bora mganga kuliko mama aliyetekwa na mchungaji/mtume au nabii wa kilokole. Kuna dada yangu karibia aachane na mumewe kisa mchungaji. Yule mchungaji alikuwa akimwambia kama huna hela leta hata sadaka ya sabuni na vitu vingine vya ndani. Ilikuwa balaa maana hela za familia mchungaji alizitafuna mno.
 
Back
Top Bottom